kama Tenga anaongea ukweli, kwa nini hawakufuata taratibu kama sheria inavyotaka, kusajili katiba mpya? wao wakaipitisha kinyemela? Natumaini FiFa inatambua kua katiba lazima isajiliwe, sasa ukimsikiliza Tenga anasema kama vile wao serikali wanatakiwa kupewa taarifa tuTenga ndio mkweli kwasababu amebobea kwenye maswala ya soka,tatizo la Tenga nikumpigia debe Nyamlani na fitina za kumwengua Jamal Malinzi....ila kwa Wambura sawa maana haeleweki mara siasa ,mara soka ni ulaji tu anatafuta
kama Tenga anaongea ukweli, kwa nini hawakufuata taratibu kama sheria inavyotaka, kusajili katiba mpya? wao wakaipitisha kinyemela? Natumaini FiFa inatambua kua katiba lazima isajiliwe, sasa ukimsikiliza Tenga anasema kama vile wao serikali wanatakiwa kupewa taarifa tu
lakini kwani FiFa imekataza vyama vya michezo kufuata sheria za nchi? hapa serikali inasema katiba haijasajiliwa si ndio ?Ni kweli kwa sheria za Fifa,serikali haipaswi kuingilia maswala ya utawala wa chama cha mpira,endapo chama husika ni mwana chama wa Fifa,na kama ni katiba wao Fifa ndio hupendekeza ni katiba ipi itakuwa muafaka. Tumeona Nigeria,kuna wakati serikali iliingilia utendaji wa chama cha mpira cha nchi hiyo,na matokeo nikwamba nigeria ilifungiwa kwa mda na Fifa.
Na hizi sheria si kwamba serikali haizielewi,ila kwavile serikali imeshazoea kuingiza siasa kila sehemu,kwahiyo wanalifumbia macho na kujifanya hawaelewi.
kwa hiyo hapa unasema hakuna mkweli kwenye hili sakata? nimemsikiliza mjumbe wa heshima wa Fifa Said El Amri, ameelezea vizuri hili sakata, ni kwamba Tenga kaona kakosea ila anataka kuleta ubabe wake ili serikali ishindweWaziri anajua katiba "imechezewa",hatukatai.Lakini,je hajui utaratibu wa kufuata kwa mujibu wa kanuni za FIFA? Hapo kuna walakini.
TFF wanasema marekebisho ya katiba ni kwa njia ya waraka baada ya kugundulika kuwa walitumia janja ya nyani kwa kudanganya kwa msajili kuwa marekebisho yalifanywa na mkutano mkuu.Lakini pia marekebisho hayo yamefanyika kabla ya waraka kutoka FIFA,kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba TFF wako up to date zaidi ya FIFA. Hapo napo kuna walakini.
Malalamiko ya katiba yamepata nguvu baada ya Malinzi na Wambura kuenguliwa ktk kinyang'anyiro cha uongozi wa TFF.Swali linakuja,je katiba imerekebishwa kipendele kimoja tu? Mbona malalamiko hayahusu sana vipengele vingine? Na sisi wadau wa soka tumejikuta tunazungumzia kipengele hicho hicho.Hapa napo kuna shida pia.
Ukiyaangalia mambo yote hayo utagundua kuwa,TFF ni kigeugeu,serikali ni kigeugeu. na sisi wadau wa soka pia ni vigeugeu..FULL STOP!
halafu ukimsikiliza Tenga, anang'aangania kua serikali kuwaambia watumie katiba ya mwaka 2006 ni kwamba tubarudi kule kule akisema kua kuanzia miaka ya 2008 mpka 2011 kuna mikutano mikuu imepitisha mambo mengi kwa hiyo eti haiwezi kutumika..halafu ukimsikiliza ni kama anatapatapa tu, ni kama hayupo tayari kukitetea anachoongea. Tenga amekuwa mjanjanja sana kwenye uchaguzi huu na kitendo cha kumfanyia fitna malinzi waziwazi ndicho kimembomolea heshima aliyojijengea
kwa hiyo hapa unasema hakuna mkweli kwenye hili sakata? nimemsikiliza mjumbe wa heshima wa Fifa Said El Amri, ameelezea vizuri hili sakata, ni kwamba Tenga kaona kakosea ila anataka kuleta ubabe wake ili serikali ishindwe
Kweli mkuu Tenga, kachemka ila kuna eneo kaona serikali imekosea kidogo ndo kaamua kokomaa nayo , Tenga kajishushia heshima sana kwenye hii ishuTenga amechemka sana kwenye hili ,alikuwa anaheshima kubwa sana kwenye soka tofauti na viongozi wengine ila hapa mwisho analikoroga .Ukimsikiliza utagundua ni mtu aliyetengeneza chuki na fitina pasipo kutumia akili ,sasa anatumia mabavu . Sio muumini wa kumtetea Wambura ila kwa Malinzi ni dhahiri kulikuwa na chuki na majungu ,hii ni very low kwa mtu wa aina ya Tenga.
Kinachotokea ni matunda ya kufanya mambo bila kujipanga kwa L. Tenga kuwazibiti hao wahasimu wake. Nimesikia El Amri ameonekana dhahiri kutokuridhika kwake na uchemkaji wa Tenga.
Nimekuelewa mkuu wangu, pamoja na kwamba serikali inajua hili lakini kukaa kimya na kumuacha Tenga afanye kila analotaka yeye nayo sio haki kwa kweli bora tunaanza kujua sakata hili chanzo nini..Hapana mkuu.
Sina kumbukumbu kama kuna mahali nimesema "hakuna mkweli" ktk sakata hili.Nilichotaka kusema ni kwamba pande zote zinazohusika(ikiwa ni pamoja na sisi) kuna vitu tunaviruhusu vifanyike bila kufikiria.
TFF wametengeneza katiba mpya kinyume hata na kanuni za katiba liyokuwepo.. wameisajili kisanii..
Serikali ikiwa inajua madhara ya kuingilia shughuli za utendaji wa TFF,bado imejiingiza kwenye mgogoro ambao kwa vyovyote vile,TFF kupitia mgongo wa FIFA imetunisha msuli...
Wadau wa soka bila kujua undani wa maudhui yaliyomo ndani ya hiyo katiba mpya,wamesombwa na ushabiki wa akina Tenga na Malinzi..
Hapo wewe unaona mkweli au asiye mkweli ni nani?
Kwao hiyo mkuu unataka kuniambia kua vipengele alivyotumia Waziri kua katiba sio halali, sio kweli ? kwamba TFF wamafuata taratibu?Tujiulize, TFF kuna unono gani? Kwa nini watu wanang'oa visiki kuhakikisha wanatua hapo? Je hizi ni dalili njema kwa soka la Bongo?
Kuhusu suala la waziri Mkandara kuingilia TFF halina ubishi. Ila lawama habebi yeye, amelishwa maneno na Amo Makala. Huyu mheshimiwa yupo kwenye kambi ya Malinzi na ndio maana anafanya kila mbinu kuhakikisha anagombea.
Kwao hiyo mkuu unataka kuniambia kua vipengele alivyotumia Waziri kua katiba sio halali, sio kweli ? kwamba TFF wamafuata taratibu?