sakata la misukule iringa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Mfanyabiashara, Anetty Ngulu maarufu kwa jina la Mama Mbilinyi akiokolewa na polisi asishambuliwe na wananchi.

LILE sakata la mwanamke mmoja mkazi wa Kitongoji cha Frelimo, Manispaa ya Iringa, Anetty Ngulu maarufu kwa jina la Mama Mbilinyi kudaiwa kufuga misukule na habari zake kuandikwa kwenye vyombo vya habari nchini, mapya matano yameibuka kuhusiana na
sekeseke hilo.​

Habari kutoka kwa vyanzo vyetu zimebainisha mambo matano mapya ambayo yamejitokeza mara baada ya tukio la awali.

LA KWANZA
Inadaiwa baada ya sakata la mama Mbilinyi ambalo mpaka sasa halijathibitishwa, baadhi ya watu wanaofuga misukule kwenye eneo hilo waliwachukua na kwenda kuwahifadhi jirani na Makaburi ya Makanyagio. Eneo hilo limepakana na Frelimo.

Habari kutoka kwa baadhi ya majirani zinasema kuwa wafuga misukule hao walilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya vurugu za nyumbani kwa mama Mbilinyi wakiamini aibu hiyo inaweza kuwakuta na wao.​

...gari la mfanyabiashara huyo likiwa yamevunjwa vioo kwa mawe.
LA PILI
Baadhi ya wakazi wa Frelimo ambao waliomba hifadhi ya majina yao, waliliambia gazeti hili kuwa ukiachilia mbali tukio la mama Mbilinyi kudaiwa kuwa misukule ilitoka nyumbani kwake, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaoishi kwenye kitongoji hicho wanafuga misukule kwa ajili ya kusimamia biashara zao.

“Hiki kitongoji ni kichafu tangu zamani, kwani tukiziacha tuhuma za mama Mbilinyi, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaoishi huku wamekuwa wakituhumiwa kuua ndugu zao na kuwafanya misukule ili kuimarisha biashara zao,” alisema mkazi mmoja.

LA TATU
Wafanyabishara wenye asili ya kabila moja maarufu mkoani humu ndiyo wanaoaminiwa kujishughulisha na mambo ya kufuga misukule.
Inadaiwa kuwa, wafanyabiashara hao huua ndugu mmoja kila mwaka na kumfanya msukule au ndondocha katika biashara zao, hali inayowaongozea utajiri (kwa mujibu wa imani yao).

...nyumba ya mama huyo baada ya kuvamiwa na wananchi wenye hasira.


Kwa sasa Mkoa wa Iringa wenye wilaya 6 ambazo ni Iringa Mjini, Ludewa, Njombe, Makete, Kilolo na Mufindi una makabila makubwa matatu, Wahehe, Wabena na Wakinga.

LA NNE
Wapo wanaodai kwamba Mama Mbilinyi alikutwa na mkasa huo kufuatia kisasi kutoka kwa mwanamke mwenzake aliyetofautiana naye kibiashara.

Inasemekana kuwa mwanamke huyo ambaye jina halijapatikana, ‘alitengeneza’ watu watatu ambao aliwavisha mashuka meupe na kuwaweka nje ya geti la nyumba ya Mama Mbilinyi na baadaye watu hao walitoka mbio kwenye geti hilo na kwenda kuingia kwenye gari, hali iliyowafanya baadhi ya majirani kuamini ni misukule iliyotoka kwenye nyumba hiyo.

LA TANO
Watu saba (majina yamehifadhiwa) wanashikiliwa mpaka sasa kufuatia kasheshe hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangala alisema watu hao wanashikiliwa na maafande wake huku uchunguzi ukiendelea.

...wananchi wakiishambulia nyumba ya mama huyo.

HARUFU YA DAMU
Katika sakata hilo, waandishi wa habari 10 na Mama Mbilinyi mwenyewe walinusurika kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya silaha mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wananchi.

Aidha, watu wanaokadiriwa kufikia 200 walidaiwa kuizingira nyumba ya Mama Mbilinyi wakitaraji kuiona misukule mingine ikitokea humo. Mama huyo alilala selo kwa siku nne kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

IMANI ILIYOSAMBAA
Imani ya misukule imekuwa ikichukua nafasi kubwa katika imani za kishirikina nchini ambapo miaka ya hivi karibuni, baadhi ya makanisa yamekuwa yakidai kuirudisha misukule katika maisha ya kawaida.​

...askari polisi aliyejeruhiwa katika vurugu hizo akipelekwa wodini.

Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God ‘Mikocheni B’, Dk. Getrude Pangalile Rwakatare amewahi kuwaonesha misukule (angalia picha kubwa mbele) kwa waumini wake akisema walirudia hali ya awali baada ya maombi yake yenye nguvu.

Msukule mmoja alipata ajira kanisani hapo huku mzee mmoja aliyedaiwa kumchukua msukule mtu huyo, akikata shauri na kuokoka.
juma: MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MISUKULE IRINGA
 
Haya mambo nadhani yapo. Mimi nilisoma Mkwawa sec kipindi hakijawa chuo hivyo nayafahamu mazingira hayo. Mtaa wa ilala zamani hizo kulikuwa na mamalishe wengi ikiwemo migahawa mbalimbali ya chakula. Tulikiuwa tukinunua chakula Makanyagio has kwa mtu maarufu kama Chuwa bila tatizo lolote au Mtaa wa ilala Kwa mtu maarufu kama Nelkon bila matatizo wala scandal yoyote. Zengwe lilianzia pale alipojitokeza Bibi mmoja hapo mtaa wa ilala akiuza wali na nyama nyingi kweli kweli. Vidume karibia wote toka Mkwawa tukahamia kwake na kuachana na Chuwa na Nelkon. Baada ya mda kidogo tukasikia yule bibi alikuwa akitulisha nyama za wafu toka makabulini kiuchawi. Kwamba aliyasema haya yeye mwenyewe baada ya kuokoka. Wachungaji wake walimkataza asiseme tena hayo maana atahatarisha uhai wake na familia yake. Basi hiyo habari ikaishia hivyo.

Lakini katika mazingira ya kawaida baada ya kukua nilijaribu kufanya tathmini ya bei ya chakula(Tsh 100 hadi 150) kwa sahani dhidi ya ujazo wa chakula chenyewe(hasa nyama) tena dhidi ya gharama halisi za maisha wakati ule niligundua kuwa huyu mtu alikuwa anastahili kupata hasara mara mbili hadi tatu. Lakini haikuwa hivyo. Sisi tulikuwa na sera isemayao bora Quantity na sio Quality matokeo yake yakawa hayo ya kuangukia mikononi mwa bibi huyo.

Nashangaa kusikia hayo mambo bado yanaendelea!!!!
 
Back
Top Bottom