RUGE MUTAHABA ANASHIKILIWA NA POLISI.
Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba asubuhi ya leo kulikuwa na kikao cha wafanyakazi wa Clouds. Kikao hicho kiliitishwa na Mkurugenzi wao wa Vipindi na Uzalishaji bwana Ruge Mutahaba ambaye aliwaeleza wafanyakazi wote juu ya kituo chao kuvamiwa siku ya Ijumaa.
Baada ya hilo na mengine yanayohusu tukio hilo, Ruge alitakiwa kuripoti katika kituo cha Polisi cha Oysterbay. Mpaka sasa Ruge anashikiliwa Polisi hao.
Hofu kubwa imetanda kwa wafanyakazi wa Clouds na sasa mabosi wao wanaonekana kuwa mashakani baada ya kuvuja kwa video ya CCTV inayomuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akivamia ofisi hizo za Clouds.
======
UPDATES:
Ruge sasa inadaiwa amehamishiwa Central Police kwa mahojiano zaidi.