Sakata la Lissu: Wabunge wa Upinzani watoka nje ya Ukumbi wa Bunge

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Wabunge wote wa upinzani wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao kufukuzwa, pamoja na kitendo cha Tundu Lissu kukamatwa.


====
More:
====

Wabunge wasusia Bunge baada ya Spika kukataa hoja ya Zitto Kabwe ya kutaka kujadili kukamatwa kwa Tundu Lissu hapo jana. Hoja hiyo imeletwa na Mh. Zitto kabwe.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson Mwansasu, ameamuru kutolewa nje wabunge wa upinzani kufuatia vurugu zinazodaiwa kuanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee.



Wabunge wote wa vyama vya upinzani waliokuwa bungeni katika kikao kinachoendelea jioni hii wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao kufukuzwa bungeni pamoja na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kukamatwa.

Tulia%20mdee%20bulaya.jpg

Wabunge waliokuwa wameamuliwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ni pamoja na mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.

Wabunge hao watatu wamedaiwa kupinga uamuzi wa Naibu Spika kuhusu muongozo ulioombwa na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuhusu utaratibu uliotumika kumkamata mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mara baada ya Naibu Spika kutoa maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao watatu bungeni, ndipo wabunge wengine wa upinzani pia wakaamua kutoka kama ishara ya kupinga maamuzi hayo, pia ikiwa ni ishara ya kupinga utaratibu wa kukamatwa kwa mbunge Tundu Lissu.

Nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Mjini Tundu Lissu, amesema wamefikia hatua hiyo kuonesha kuwa uataratibu unaotumiwa kukamata wabunge wakiwa bungeni siyo sahihi, na kwamba kesho wataendelea na vikao vya bunge lakini mapambano yataendelea.

"Kesho tunarudi bungeni, lakini mapambano yataendelea, tunataka kuonesha kuwa utaratibu huu wa kuvizia wabunge kwenye milango ya bunge bila taarifa rasmi ya Spika na bila kuwaeleza wabunge sababu za kukamatwa kwao siyo sawa. Tukilifumbia macho litakuwa kumtokea mbunge yoyote hata wa CCM" Amesema Zitto.
 
Wabunge wasusia Bunge baada ya Spika kukataa hoja ya Zitto Kabwe ya kutaka kujadili kukamatwa kwa Tundu Lissu hapo jana.

Hoja hiyo imeletwa na Mh. Zitto kabwe

Nashindwa ku upload hii clip ya zito kabwe akihojiwa na jahazi..

Mwenye taarifa zaidi tafadhali
 
Wabunge wote wa upinzani wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao kufukuzwa, pamoja na kitendo cha Tundu Lissu kukamatwa.
huku naye mohammed ametimuliwa cuf
Tundu lissu kesho kupanda mahakamani
Source;TanzaSiasa facebook
 
Anayeongoza kikao ni Ndugai au Tulia?

BTW:Ndugai alibugi sana kipindi kile kujifanya Koffi Anan.

Inatakiwa kukaa kimya tu ili kuuona mwisho wake.
 
Back
Top Bottom