Sakata la Lissu "Handle with care"

Popote duniani wlaipovunja katiba walikuja kushtakiwa baadae hata kama katiba zao haziruhusu. Huwa zinakujaga kubadilishwa ili ziweze kuwastaki.
 
Wapinzani wanasema mikutano na maandamano ni haki yao kikatiba na kisheria. Sasa rais angetuambia yeye anazuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
Mkuu hapo umenena. Na angekua amekata mzizi wa fitina...
Naamina wanachodai upinzani ni fact kabisa na kipo kisheria
Tatizo huyu na analeta zogoro
 

Nimekuwa nikiwaza kama wewe ulivyoeleza hapa kwenye uzi wako.Serikali itakuwa inafanya makosa makubwa kujaribu kufikiri Lisu ni mropokaji au bwatabwata tu.Huyo ni mtu anajua anachokifanya.Tatizo la CCM na Serikali yake siku zote imekuwa ni ukosefu wa uwezo wa kutumia mlango wa sita wa fahamu(6th Sense).Kwa namna tulivyoumbwa kuna watu kipaji chao cha kuweza kuona mambo yatakavyokuwa huko mbeleni ni cha kiwango kikubwa.Uwezo kama huo wa kuonya jinsi mambo yatakavyokuwa kabla hayajatokea watu wanao.Na wala tusifikirie labda kipaji kama hiki ni cha akina Lusekelo au Marehemu Sheikh Yahaya Hussein au TB Joshua.

CCM na serikali yake mara zote wamekuwa reactive kwenye mambo mengi sana.Wakielezwa wanakuwa wabishi lakini baadaye huja kung'amua kuwa kilichokuwa kinasemwa ni cha kweli.Hivi hata hili la udikteta kuna wakati watafika mahali waelewe kinachosemwa.
 
This may be too smart for them
 
Serikali inatumia kiasi gani kufukuzana na huyu jamaa??
 
his safi
 
Jambo kubwa linalohitajika hapa ni ''Busara''. Kuhimili mikiki mikiki ya kukosolewa na kukosoana, hata kama Serikali inaendeshwa na malaika lazima iwe na ngozi ngumu kuhimili kukosolewa.

 
Wapinzani wanasema mikutano na maandamano ni haki yao kikatiba na kisheria. Sasa rais angetuambia yeye anazuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?

Hakuna sheria yeyote inayomruhusu kufanya hivyo kama nchi haijatangaza hali ya hatari. JPM alijipambanua vizuri sana kupambana na ufisadi na tunamwunga mkono. Lakini hili la kupambana na upinzania au mtu yeyote anayetoa maoni ambayo yeye hakubaliani nayo, kamwe hawezi kuungwa mkono na wapenda amani ktk nchi yetu. Akumbuke kuwa hakuingia madarakani kwa mapinduzi, bali kwa njia ya demokrasia hivyo hawezi kupinga mfumo uliomwingiza madarakani na tukabaki salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…