Sakata la Dawa za Kulevya: Askofu Gwajima atema cheche, adai RC Makonda anatumika

Heshima kwenu wakuu,

Askofu mkuu Mkk wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima, atema cheche baada ya kutuhumiwa kuhusu madawa ya kulevya.

Soon nawapa Updates kinachojiri.

======

UPDATES;

======

View attachment 468791
Gwajima: Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media?

Gwajima: Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii.

Gwajima: Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi;

1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi

2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya.

Gwajima: Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote.

Gwajima: Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge Mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza makonda kwa sababu kafanya Vizuri. Makonda anaujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi Muu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya Hitilafu.

Gwajima: Makonda angeweza kunipigia simu au Kuwagiza Polisi wakaniletea samasi au kuniita.

Gwajima: Nia ya Makonda ni kutaka jina la Gwajima liharibike. Kama Gwajima hafanyi na hajihusishi na Madawa ya kulevya watu wa Usalama wanajua. Nmefanya hii kazi ya Uchungaji kwa Miaka 20.

Gwajima: Si kweli kwamba makonda anatumwa na Rais Magufuli, rais ana tabia ya kupongeza saa nyingine anapiga simu Clouds kupongeza pale wanapofanya Vizuri.

Gwajima: Sisi tunamuunga mkono Mheshimiwa rais hata kama kwenye uchaguzi hatujamuunga mkono, Lakini kwa kuwa amechaguliwa yeye tunamuunga mkono

Gwajima: Naamin Makonda hajajificha kwenye "Usukuma" wake.

Gwajima: Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya Serikali, ni hatari sana

Gwajima: Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze.

Gwajima: Chini yangu kuna Maaskofu 125. Kesho wataogopa nao watasemwa

Gwajima: Kuna siku Paul Makonda, Sitta na Mwakyembe walikuja kanisani kwangu hata CD ninazo na alihutubia hapa kwenye Madhabahu akinisifia sana, Leo ni kitu gani kimemfanya anichafue?

Gwajima: Je ikiwa Gwajima hahusiki, itakuwaje?

Gwajima: Mimi nlikuwa mkali sana juu ya utawala wa awamu ya nne. Miaka kwa miaka Tembo walikuwa wanakufa na hakuna hatua zilizokuwa zinachukuliwa.

Gwajima: Kuna Kipindi Ridhiwani Kikwete aliwapeleka Mahakamani Dr. Slaa na Mch. Mtikila akitaka wakanushe habari kuhusu utajiri wake, hiyo kesi sijui iliishia wapi.

Gwajima: Nani anamtumia Makonda?

Gwajima: Makonda ana nia ovu juu yangu na juu ya Wakristo. Anataka kuwaaminisha watu kwamba wokovu haupo.

Gwajima: Mimi nataka kununua ndege nyingine ili nianzishe chuo cha ndege, mbona sipongezwi kwa hilo?

Gwajima: Jambo hili alilofanya si sawa na si sahihi.

Gwajima: Wabunge wamepiga kelele juu ya jambo hili, sisi wananchi tusio na sehemu ya kuongea tufanyeje?

Gwajima: Namfahamu rais Magufuli, hawezi kumpendelea kwa kuwa ni mtu wa kwao (Msukuma). Rais anawapenda watu wote anawapenda Mawaziri wote na watendaji wote wa Serikali. Naamin rais hajamtuma Makonda.

Gwajima: Nguvu katika mikono isiyo sahihi ni hatari sana.

Gwajima: Juzi kati tulikuwa na mechi kati ya maasikofu na viongozi, Mimi nlikuwa namba tia yeye namba 10. Alikuwa ananiangalia jicho baya sana. Mimi, Makonda, kamanda Sirro Spika wa Bunge tulikuwa tunamechi si angenikamata hapo?

*Kuna watu walikuwa wanauza madawa ya kulevya, katika uongozi huu wale walikuwa wanauza madawa ya kulevya wamebadili majina na wanafanya biashara nyingine. Walikuwa na jina B sasa wamebadilisha jina.
Naona ananikanyaga sana mchungaji Gwajima maelezo mengi ya nini tuthibitishie unatumia/unauza au vinginevyo
 
Marofa na wapumbavu walisema sio tusi mkapa alitamka hili neno nyie ndio mlimtetea Leo huyu kondakta kuitwa hivyo unatoa mapovu acha upumbavu
Mkuu mzee wa liver
Sijawahi kutetea,pitia mabandiko yangu humu!Siwezi kutetea mtu kuitwa lofa kama ambavyo siwezi kumtetea mtu anayemuita mwenzake mpu,mbav.u

Bahati mbaya na wewe tena unaniita mimi mpu.mbavu bila hata kosa.Sio vizuri,tujadiliane bila kutukanana!!Huu ni mjadala tu,nia yetu ni moja
 
Hatimaye Mch Josephat Gwaajima amtaja NYANGUMI wa madawa ya kulevya Tanzania.

Tunasubiri kuona kama huyu NYANGUMI ataitwa Central Police kwa mahojiano na KIBUA!
 
Mkwanja wako tu mkuu, ila maana yake ni nn sasa kuwa na mawakili nane tn wawili wakizungu!!
Hapo mi naanza kuwaza kuna kitu kitamkuta makonda muda si mlefu,

Mawikiri sita wa kibongo hafu utakuta na wao ni wahusika na wanaijua bongo vizuri
Ongeza wawili wazungu wa kuja kuona namna inshu zilivyokaa
Hapo tutakaa tuuu



Nakumbuka tuu usemi wa mbunge mmoja

"" KAMA UNAZIJUA SHERIA ZA NCHI HII HUFUNGWI""

Tafasiri yake nini, ukiona umekosea na huzijui sheria na inaamini ukizijua sheria hufungwi, basi mkwanja ufanye yake,

Kwenda kutoa maelezo tuu mawakili nane,
Je!
Kuiendesha kesi itakua mawakili wangapi??

Hesabu hiyo jibu lake hata silitaki
 
Wito ni wito tu,waitwe kimya kwani kuna ajenda gani ya siri

Mkuu ww utakuwa ni zoba fulani. Mikataba ya nchi yenye maslahi na wananchi wote ni siri, lakini hilo la kuchafuliana majina ndio liko wazi tena kwa mtu unayemtuhumu tu!!
 
Askofu Gwajima ameshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumhusisha na issue ya madawa ya kulevya.

Pia kashangazwa na Mkuu wa Mkoa huyo kutotaja jina la Ridhiwani Kikwete. Amesema Ridhiwani katajwa na watu wengi mitaani na hata aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa alimtaja na kutoa evidence hadharani...

Mytake:.. Naona nchi sasa inawaka moto
Kwani ameambiwa list imeisha. Huo utetezi kachemka.
 
Mkuu MENGELENI KWETU kama sio kosa basi
Mimi nilifikiri inaweza kuwa ni kosa!Asante kwa kunielimisha

...Tatizo lingine la huyo RC ni lugha zake mbaya na za dharau...utasikia anawaita wafanyazi vichaaa, wapuuzi tena in public; mara useme wabunge ni kulala tuu na kuchekeshana...huu si uongozi na uelewe kila mtu ana utu wake. Ndiyo maana ukifuatilia na kutathmini operesheni zake zoote alizoanzisha zimeishia kwenye matamko tuu, nothing more; why? coz hapati support kutoka kwa watumishi, na possibly wanasiasa wenzake. Sijawahi kuona kikosi bora cha mpira kinachomtegemea mfungaji peke yake, it has to be team work.
 
Hivi Gwajima huwa hana Radio kama kina Mwingira?!Maana Manji licha ya kuwa katinga Polisi na mawakili 8 ,6 wa Tz na 2 wa nje,lakini amelitumia vyema gazeti la Jambo Leo,kurasa za mbele na nyuma ni yeye,Nafikiri alilinunua toka kwa kina Juma Pinto,au atakuwa na "share" kubwa kuzidi kina Juma Pinto.Japo kwa asili,hii Jambo ni kampuni ya Juma Pinto.

Juma Pinto!!Down Town kitambo....Mtoto wa mjini,ndio yule Camera za Airport zilimuonyesha ndio alimsindikiza Masogange mpaka dakika za mwisho pale Airport siku alipokamatwa O.Thambo International Airport na mzigo wa maana.

Dulu za uchunguzi zikaonyesha,kabla Masogange hajaondoka na South Africa Airways,Flight # 187 yenye usajili wa ZS-SJF,alitoka kwenye Mgahawa wa Juma Pinto ulio katikati ya jiji.Na yule dada aliyekamatwa na Masogange kule Bondeni,alikuwa ni mfanyakazi wa mgahawa wa Juma Pinto pale katikati ya mji.

Kwa hiyo wewe unganisha tu dots...huna haja ya kuanza kusema Manji katoa rushwa,sijui kanunua gazeti!!Anaweza tu kuwa anasaidiwa na wenzake kujisafisha,maana hujui yeye aliwahi kuwasaidia nini huko nyuma.

Hivi vita ni vuzuri tu,maana wengine tuna vijana wetu wa kuwalea na kuwakuza wamekuwa mateja,toka tunaanza kuwalipia ada za shule mpaka chuo,sasa tunalipa "ada" za Rehabilitation kwenye "Soba House".Ukisikia mtu ni muuzaji,unaweza mpiga makonde.

Lkn Manji awe mkweli tu,hatumiii??Maana watu wanajua huwa analala ofisini hata siku nzima kwa kubwia.Inajulikana pia kwenye ile "private jet" yake nini hufanyika ndani.Na namna anavyoweza kupita pale Airport kama VIP...na watu badala ya ku-concentrate kumkagua,basi wanatoa macho kwenye "tips",kuanzia walinzi mpaka polisi.

Kwa hiyo ushahidi tu wa moja kwa moja ndio tabu,ila kusema huyu bwana yupo "associated" na haya madubwana,sio jambo geni sana.

Huyu Mbowe,yeye ataitwa atoe maelezo tu.Ile Club yake ya Billicanas ni moja ya "soko" kubwa la dawa katikati ya Jiji.Je anaweza kujua wale wauzaji ndani ya Club yake wanapata wapi mzigo?Na alichukua hatua gani kujua sehemu ya wateja ktk Club anayomiliki wanafanya biashara hiyo!Japo sasa anaweza kusema hata hiyo Club "mlishaninyang'anya"...Na hata hivyo,mmiliki mwenza NHC naye ilibidi aitwe,atoe maelezo kama anajua moja ya jengo lake kunauzwa unga.

Bahati mbaya au nzuri kwa Mbowe,ushahidi wameufuta wenyewe serikali...Maana kile kieneo vijana walikuwa wakitafuna unga ili wapande vizuri stejini kuimba,kimepitiwa na tingatinga.Ushahidi kwisha...

Kavita hata ni kagumu sana!!!Leo naona hili gazeti mapaka habari za Michezo ni kumtetea tu Manji.Kuanzia Captain wa Yanga mpaka mfua jezi!!Na Manji anasema Makonda anataka kuiuwa Yanga,ile WanaYanga wanunuw ugomvi!!

Huyu kanjibahi "approach" yake mbaya!!Yule Ngosha hajaribiwi...Yaani kama ni "chizi" basi yule ni zaidi ya Manji...Atajilaumu bure ktk utawala huu!!Unamuita Mkuu wa Mkoa "Mpumb..avu?"

Huyu Gwajima asiropoke sana,maana biashara zake na wale Wakorea wanaokuja kwa gia ya utumishi inajulikana.Mitandao yake inaeleweka tu.Sidhani kama katajwa kimakosa,shida atakayopata Makonda ni ile kuthibitisha moja kwa moja!!Lkn si siri sana!Nasubiri Gwajima aongee halafu tuje tumuulize hapa maswali ayajibu.

Nimejaribu tu kuchambua uhusika wa hawa Watatu...Sio lazima uamini,lkn huu uchambuzi ni kwa uelewa wangu juu ya vita hivi
Loh.!!!
 
Halafu hawa watu ni waajabu sn, hayo wanayoyaongea kwenye media si ndo wameitwa wakayaseme huko!! akataje huko alikoambiwa aende Ijumaa, kwa akili ndogo kabisa huyu nae kuna linalomuhusu!....... . Mbona masogange hajakamtwa(in wema voice)[/QUOTE

Hao waliowaita kupitia media walishindwa nini kuwaita kwa kuwapigia simu?
 
Aiseee kwa utetezi huu wa Gwajima lazima ni aibu sana
Ungekuwa "huru kichwani" ungeona hoja za Gwajima. Pale hakuwa anafanya utetezi (ajitetee kwa lipi?), alikuwa anamlaumu Makonda kumtaja kwenye "press conference" kwa kuwa wangeweza tu polisi kumwita. Lakini ameongea pointi nyingine muhimu sana, na ambayo kwa wengi yuko sahihi-kwamba Makonda anafanya kazi sana lakini nafasi aliyopewa ni "over size"! Na amemtahadharisha mteule wake, kama umemwelewa Gwajima, kwamba atamvurugia. Hata hujasoma hoja ya "system ya serikali ku-paralyze"? Haya na mengine yanaweza kutafakarisha wale tu ambao "wanafikiri kwa uhuru"!
 
Back
Top Bottom