Sakata la bei ya mafuta kupanda. Serikali imekosa washauri sahihi

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wadau, tayari Serikali kupitia Latra imetangaza bei mpya ya nauli nchini ikipanda kwa asilimia karibia 20-22 tukio linalokwenda sambamba na ongezeko la bei ya mafuta iliyotangazwa na Ewura.

Kupanda kwa bei ya mafuta kunatajwa kuwa chanzo kikuu ni kushuka kwa uchumi wa dunia uliyosababishwa na gonjwa la Covid na vita kati ya Urusi na Ukraine, huenda ni kweli lakini yapo madai kuwa, chanzo kikingine ni serikali kukosa washauri sahihi kwenye swala zima la uagizaji wa mafuta ambalo kwa sasa linasimamiwa na serikali yenyewe kupitia mradi wa Bulk Procurement.

Hivi karibuni baadhi ya wafanyabiashara wakubwa nchini, wakiwemo waheshimiwa wabunge waliishauri serikali kuruhusu uagizaji wa mafuta uwe huru lakini vigezo na masharti vizingatiwe ili kupata kodi na taratibu zote zifuatwe.

Hata hivyo, kuna taarifa kwamba, serikali imeamuwa kuwapa vibali wafanyabiashara sita tu kwa nchi nzima ili waweze kuagiza mafuta jambo ambalo limezua sintofahamu na wadau kuhoji kama watu sita wanaweza kukidhi ukubwa wa soko husika.

Hata hivyo, habari za ndani zinadai kuwa, kampuni hizo sita zilizopewa vibali zinaundwa na baadhi ya mabosi wenye ajira hukohuko Bulk Procurement, hivyo serikali kusema imetoa vibali ni kiini macho cha mchana kweupeee huku wafanyabiashara wenye nia ya dhati na biashara hiyo wakitupiwa kwenye kapu la pembeni

Baadhi ya wafanyabiashara wakubwa nchini wameitaka tena serikali kutoa vibali kwa wafanyabiashara wanaotaka kuingizza mafuta nchini bila kujali idadi yao kwani bado udhibiti wa ubora wa mafuta utakuwa mikononi mwa serikali huku Bulk Procurement nao wakiendelea na zoezi hilo.

“Unajua, wafanayabiashara wakubwa wakirughusiwa, wataianiza mafutakwa wigi na kwa sababu ya ushindani, wengi watajikuta wakiuza mafuta kwa bei ya chini hata kama faida itakuwa ndogo,” alisema Abdul Karim Soni mfanyabiashara wa mafuta ya kula jijini Dar.

Jana tarehe 5,Mei baadhi ya wabunge walimtaka waziri wa Nishati, January Makamba kutoa ufafanuzi juu ya upandaji wa mafuta nchini jambo ambalo limesababisha kupanda kwa bidhaa zote tukio ambalo limeleta mtikisiko kila pembe ya nchi.

Baadhi ya wadau wanasema kuwa, bosi anayesimamia mamlaka ya mafuta nchini anaweza kuwa chanzo kwa sababu ya kutoishauri vizuri serikali kuhusu kuruhusu biashara ya mafuta kuwa huria kwa vile amewahi kufanya kazi Bulk Procurement hivyo kuitetea kwa njia moja au nyingine. Nawasilisha wadau, nini kifanyike, hali tete.
 
Hizi regulatory authorities i.e ewura na latra zifutwe. Zina ma-DG wanaolipwa zaidi ya 15m kwa mwezi kwa kazi ya kupanga bei ya petroli na nauli za mabasi tu.

Kitendo cha kumlipa 15m/mo DG ambaye hazalishi chochote, na sisi wananchi kukatwa 1% ya gharama zetu za maji au umeme au petrol ili kui-sustain ewura hakikubaliki.

Kama jiji la DSM lilivunjwa kwa kuwa lilikuwa kupe ya manispaa za ilala, temeke na kino, hivyo hivyo ewura na latra wafutiliwe mbali.
 
Back
Top Bottom