Nimekuwa nikifuatilia usajili wa wachezaji Simba toka Mwekezaji Mo aanze kuifadhili Simba kabla hajaingiza 20b.
Kwa miaka minne iliyopita usajili wa Simba ulijipambanua kama timu hasa inayohitaji Mafanikio ya Haraka kwa kusajili wachezaji wenye majina na uwezo mkubwa uwanjani.
Kwa kipindi kifupi Simba cha uwepo wa Bilionea, Simba imefanikiwa kutwaa Makombe ya Ligi kuu na shirikisho, sambamba na kushinda ngao za hisani na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Mwekezaji Mo, sasa ni dhahiri ameshakabidhiwa timu na jicho la mbali linamuona kama mtu ambaye ameshajipa uhakika wa kuendelea kuwekeza na ameamua hasa kufanya biashara ya Mpira kwa sababu zifuatazo.
Sababu ya Kwanza, timu imeuza key players wawili ambao walisaidia timu kwenye Mafanikio waliyonayo sasa.
Imeendelea kumaintain wachezaji waliosajiliwa kwa kipindi kirefu kilichopita kwa kuamini wamezoeana jambo ambalo sio sahihi kwa sababu kuna Kipindi watazoewa na timu pinzani na hatimaye kuanza kuambulia vipigo , mfano Barcelona ya Xavi na Iniesta .
Imesajili vijana wadogo ambao Malengo ni kuzidi kuwakuza na kufanya Biashara, hayo ndiyo malengo hasa ya Mwekezaji ila akumbuke kamari hiyo pia ilichezwa na TP Mazembe ambao sasa sio tishio tena Africa.
Naliona anguko la Simba kwa karibu sana. Sababu kubwa inaonekana sasa wamesharidhika na Mafanikio na natabiri Yanga na Azam kuibuka kama timu ambazo zitatawala Msimu huu wa ligi wa 2021/2022. Kutokana na ukweli mchungu kwamba usajili wa Simba sio mzuri kulinganisha na Timu ya Yanga na Azam, najua nitapingwa lakini huo ndio ukweli na utajidhihirisha kwenye Ligi.
Yetu Macho na tuombeane uzima tu, ila huo ndio ukweli.
Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app