Saivi naanza kuwaelewa vinega vizuri

Wakwetu03

Senior Member
Sep 15, 2010
190
81
[h=6]Anselm Soggy The-Entertainer
[/h][h=6]‎-Jamani nakumbuka mwaka 98 au 99 nilimuandikia wimbo Florence Kassela maarufu kama DATAZ na nikashirikiana nae pia kuuimba huo wimbo na tuliurekodi kwa Enrico pale Soundcrafters na aliyelipa gharama za studio alikuwa ni Taji Liundi wimbo uliitwa SIKUTAKI TENA....Kuna ufisadi umefanyika wimbo umewekwa kwenye movie ya Wamarekani inaitwa SOMETIMES IN APRIL ikizungumzia mauaji ya Rwanda sasa mpaka leo huwa najiuliza ni nani aliuza huo wimbo na kwanini hatukupewa hata sumni...I HATE THIS COUNTRY[/h]
 
Watafute wakili wa kimataifa huenda wakaambulia chochote.

Maana huu ni zaidi ya unyonyaji na uporaji,ni zaidi ya ubakaji na kila aina ya ushenzi.Hope kwa jitihada zao walizokwishaanza watafanikiwa kwa hili.
ANGALIZO:kama wale jamaa wanahusika na hili wanaweza wakazunguka upande wa pili (kwa dataz) wakamrubuni ili ionekane kama aliafiki wakati mwanzo kakataa kwamba hajui lolote.
KWA HILI NAWAUNGA MKONO VINEGA.Pambana mpaka mwisho na kwenye vita ya HAKI ushindi ni lazima
 
umenikumbusha ile movie ya wale watoto inaitwa Africa united, kuna ule wimbo wa kwaya ya dini, kama sikosei kijitonyama wale waliimba 'hakuna Mungu kama wewe', sina hakika kama na wao wamelipwa
 
umenikumbusha ile movie ya wale watoto inaitwa Africa united, kuna ule wimbo wa kwaya ya dini, kama sikosei kijitonyama wale waliimba 'hakuna Mungu kama wewe', sina hakika kama na wao wamelipwa

aisee!!!!! halafu eti kuna serikali inayosimamia haki za sanaa inakatisha tamaa sana
 
Anselm Soggy The-Entertainer


‎-Jamani nakumbuka mwaka 98 au 99 nilimuandikia wimbo Florence Kassela maarufu kama DATAZ na nikashirikiana nae pia kuuimba huo wimbo na tuliurekodi kwa Enrico pale Soundcrafters na aliyelipa gharama za studio alikuwa ni Taji Liundi wimbo uliitwa SIKUTAKI TENA....Kuna ufisadi umefanyika wimbo umewekwa kwenye movie ya Wamarekani inaitwa SOMETIMES IN APRIL ikizungumzia mauaji ya Rwanda sasa mpaka leo huwa najiuliza ni nani aliuza huo wimbo na kwanini hatukupewa hata sumni...I HATE THIS COUNTRY

kwenye wimbo kuna haki za aina nyingi.
hebu pitia makabrasha yako na ukihakikisha kwamba
hakuna mahali umesign kugawa haki yako basi waweza idai.

hata dataz akidai amegawa haki zake haizuii wewe kudai haki yako
 
Back
Top Bottom