G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Hatimaye mmiliki wa kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd ndugu Said Lugumi ameibuka kutoka mafichoni na kuonya kuwa siyo kila jipu linatumbuliwa.
Aidha bwana Lugumi amewahasa watanzania waache kufanya mambo kwa hasira kwani kila jambo limepangwa vyema kwa wakati wake. Hayo aliyasema jana wakati akifanya mahojiano na gazeti la Tanzania Daima.
Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya ndani ndugu Charles Kitwanga ameonya kuwa mambo yote yanayohusu mkataba wa Lugumi yalitoka ngazi ya juu bila kufafanua ni ngazi ipi.
Ndugu Said Lugumi kupitia kampuni yake ya Lugumi Enterprises Ltd mwaka 2011 alipewa zabuni ya kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini inayogharimu Tshs bilioni 37 ambapo tayari amelipwa Tshs bilioni 34 huku utendaji kazi wake ukiwa chini ya asilimia kumi.