Kuna uwezeka akaandika mambo mawili au matatu hivi nisivyovipenda huyu ndugu lakini kwa ujumla Saed Kubenea ni miongoni mwao Wa-Tanzania wachache ambao UZALENDO WA KWA NCHI YETU HAUNA MASWALI na zaidi ni kwamba aina ya uzalendo wake (sawa na ule wa Jenerali Ulimwengu, Prof Shivji, Dr Slaa, Edwin Mtei, Bob Makani, Regnald Mengi, John Myika, Halima Mdee, Getrude Mongela, Tundu Lissu, Kamanda Lema, Mwakyembe, Double S, ...) haupindipindi, hauegemei maslahi ya muda mfupi wala hauelekezwi na 'fikra sahihi za tumbo'.
Hakika kama utakua haujamwelewa hadi leo Saed Kubenea na uzalendo wake kwa kutetea maslahi ya umma wa nchi hii kwa kutumia talanta ya kalamu yake basi hebu kaingie msituni huko kwenye maktaba walau kwa kipindi cha miaka miwili tu iliopita na baada ya hapo nadhani hutorudi hapa ubaoni kusumbua watu na mambo ambayo jawabu lake liko wazi.
Kwa ujumla Saed KUBENEA si wale akina 'NDIO MZEE'!!!!!!!!!! Ijue hilo itakusaidia zaidi.