Said Fella muache Aslay huru

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
432
1,000
Niseme kuwa ni Fella na Diamond ndiyo waliosababisha Yamoto Band Kufa.

Kama ambavyo ilikuwa kwa Wanaume family kuvunjika, chanzo ilikuwa ni Said Fella mwenyewe. Na si Juma Nature kama ambavyo tuliamini ni bangi za washikaji zilizingua tu.

Fella wewe ni mtu mzima sana, Fikiria maisha ya vijana wadogo Yamoto Band kosa lao ni lipi. Hakuna anayetilia shaka umewakuza na kuwalea ndiyo ilikuwa nafasi yako kama Meneja.

Soko la muziki limetanuka kwasasa kuna platform mbalimbali za kuuza mziki hii wewe umechelewa sana, Geuka tena Fella uwezo wa kuamua nani awe Msanii mkali, haupo tena. Unachoweza kufanya ni kupanga Dj gani asicheze wimbo lakini huwezi kuzuia nani asisikilize.

Tusitumie nguvu ya Wasafi kuhakikisha tunazuia uwezo wa Aslay. Ndiyo maana bila aibu Diamond anamtumia Maromboso leo baada ya kuhakikisha Yamoto Band imekufa, Fella wewe ni sehemu ya mkakati huu na Diamond alikuwa mshauri wa Yamoto.

Ni Diamond huyu huyu anayemnyima nafasi Maromboso kukutana na wenzake wa Yamoto. Sallam na Fella hawana mikakati thabiti wamejawa hofu ili Wasafi waendele kutambua ni kugawa pesa kwa Dj nyimbo za Aslay zisichezwe.

Wahenga walisema kuwa ni wachache sana wanaoweza kuachana na hulka zao. Pamoja na harakati za Fella kugonga mwamba, kuna taarifa za kuaminika kuwa eti Fella anataka 10% ya malipo ya kazi za kina Aslay wakiwa nje ya Yamoto Band.

Kama ni majipu, basi Sallam na Tale ni moja ya majipu sugu. Wamekuwa tayari kuhakikisha kuhujumu wasanii wadogoo wanaong'aa. Ni Tale aliyeshindwa kuing'arisha Tip Top na Fella aliyeshindwa kuibeba Yamoto Band. Wameungana kumdondosha Aslay.

Fella geuka nyuma tena.
 
Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
3,891
2,000

Hizo nyimbo za Aslay unazosema zisipigwe ni zip, mbona zinasikika sana tu ? Au ndio mnatafuta kiki
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,584
2,000
Uswahili nao kama ugonjwa vile....namuangalia baba Dangote mbavu zinataka kufyatuka zilikokaa
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,335
2,000
labda huko nyuma ya pazia kuna mambo.....yakiwashindeni huko ndani tokeni nje mpumue lol
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom