Safu ya ulinzi wa timu inaundwa na wachezaji wangapi?

Tsyamatsy

Senior Member
Sep 9, 2023
109
155
Naomba kujuzwa na Wabobezi, kwani katika Mpira wa miguu, safu ya ulinzi inaundwa na wachezaji gani? Na je, goalkeeper ni sehemu ya safy ya ulinzi?

Nauliza hayo Kwa sababu imekuwa ni kawaida Kwa hao wachambuzi kusema safu ya ulinzi ni mbovu, lakini kipa amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi na bila uhodari wa kipa basi Leo magoli yangekuwa mengi. Mimi nijuzeni je, kipa sio sehemu ya ulinzi wa timu ili goli lisiingie?

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
 
Inategemea. Mkiwa timu mbovu na mkawa mmezidiwa mchezo timu nzima mnageuka safu ya ulinzi.

Ila naturally safu ya ulinzi inaundwa na kipa, mabeki wa kati wa wiwili na mabeki wa pembeni wawili pamoja na kiungo ambaye anaweza kuwa mmoja au wawili.

Yote itategemea na mfumo wa timu.
 
Sawa, Sasa kama kipa ni safu ya ulinzi na ametimiza majukumu yake ipasavyo, inakuwaje nawasikia wachambuzi wakisema eti, "kipa amewaokoa wangefungwa sana Leo!"
Kwani hawana uelewa kuwa kipa anatimiza jukumu lake Kwa weledi?

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
 
Sawa, Sasa kama kipa ni safu ya ulinzi na ametimiza majukumu yake ipasavyo, inakuwaje nawasikia wachambuzi wakisema eti, "kipa amewaokoa wangefungwa sana Leo!"
Kwani hawana uelewa kuwa kipa anatimiza jukumu lake Kwa weledi?

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
Labda kama unazungumza wa wachambuzi wa nchi nyingine. Lakini kama unazungumza wachambuzi wa hapa Tz umepotea njia. Tz hatuna wachambuzi tuna wacha- MBUZI .
 
Huo muda wa kuwasikiliza wachambuzi wa hapa home unauoata wapi,,, kipa ndie mlinzi namba moja alafu beki na midfielders mmoja au wawili
 
Labda kama unazungumzia timu nyingine ila kwa timu yangu ya Yanga ina sifamoja kubwa inayojitofautisha na timu nyingine average. Safu ya ulinzi inaanzia kwa mshambuliaji mwenyewe halafu viungo inakuja kutamatishwa na mabeki. Same kwa ushambuliaji inaanzia kwa Goalkeeper, mabeki, viungo na washambuliaji.

Mpira ni science huwezi tu from no where ukapanga mabeki ukitegemea wao ndio watakaba peke yao sasa nini maana ya kuwa na DM, CM, AM, RB, LB, RW, LW hawa kazi yao sio tu kwenda kushambulia golini wanatakiwa pia wawe wepesi kuja kuziba mafasi zao ambazo zinaweza tumika na wapinzani kushambulia. Kama hapo itashindikana ndio yatatumika majini sasa.
 
Na kipa naye ni mlinzi tu ndio maana ukiwa na mabeki wabovu unarudi nyumbani mabega hoi kwa kuokoa michomo ili kulinda magoli yasiingie.
 
Labda kama unaxungumzia timu nyingine ila kwa timu yangu ya Yanga ina sifamoja kubwa inayojitofautisha na timu nyingine average. Safu ya ulinzi inaanzia kwa mshambuliaji mwenyewe halafu viungo inakuja kutamatishwa na mabeki. Same kwa ushambuliaji inaanzia kwa Goalkeeper, mabeki, viungo na washambuliaji.

Mpira ni science huwezi tu from no where ukapanga mabeki ukitegemea wao ndio watakaba peke yao sasa nini maana ya kuwa na DM, CM, AM, RB, LB, RW, LW hawa kazi yao sio tu kwenda kushambulia golini wanatakiwa pia wawe wepesi kuja kuziba mafasi zao ambazo zinaweza tumika na wapinzani kushambulia. Kama hapo itashindikana ndio yatatumika majini sasa.
MAJINI??

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
 
Na wanasemaga kipa nae ni mchezaji lakini katika formation zote za mpira huwa sioni kipa akitajwa, utaskia 4:4:2, 4:2:3:1 au 4:14:1 na nyingine nyingi..

Swali langu kwanini wasiwe wanaanza na 1:4:4:2 au 1: 4:3:3:1 au kwasababu yenyewe ni constant kwamba kipa lazima awe mmoja..?? Magolie wanabaguliwa Sana asee
 
Hahahahaha...umewaza vzr sana nadhani huko mbele wata introduce huo mfumo ukiwemo na golikipa, maana soka la sasa linahitaji kipa mwenye footwork ili awe sehemu ya mfumo ktk kuanzisha mashambulizi
 
walinzi kwenye mpira ni wachezaji amabo jukumu lao kubwa ni kukaba, Kipa sio mlinzi maama yeye hatoki golini kwenda kukaba. wachezaji wote wanaweza kukaba pia japo jukumu lao kuu sio kukaba, mfano washambuliaji jukumu lao kubwa ni kufunga japo huwa wanarudi nyuma kukaba
 
O
Naomba kujuzwa na Wabobezi, kwani katika Mpira wa miguu, safu ya ulinzi inaundwa na wachezaji gani? Na je, goalkeeper ni sehemu ya safy ya ulinzi?

Nauliza hayo Kwa sababu imekuwa ni kawaida Kwa hao wachambuzi kusema safu ya ulinzi ni mbovu, lakini kipa amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi na bila uhodari wa kipa basi Leo magoli yangekuwa mengi. Mimi nijuzeni je, kipa sio sehemu ya ulinzi wa timu ili goli lisiingie?

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
Inategemea na mfumo wa Mwalimu wa Timu Kuna waumini wa kuzuia mwanzo mwisho mbele anabaki mtu Moja , nyuma na katikati ya uwanja anajaza watu mfano Diego Simone wa Atlatico Madrid nyuma watu Saba. Mwingine Jose Mourinho naye anaweka watu zaidi ya Sita nyuma.
Kuna kina Pep Gurdiola yeye anacheza na watu watatu nyuma huku Beki wa kulia akipanda mbele.
Arteta Beki watatu , Beki wa kushoto anaingia katikati kumsadia Kiungo na kushambulia upande wa kyshoto
 
Na wanasemaga kipa nae ni mchezaji lakini katika formation zote za mpira huwa sioni kipa akitajwa, utaskia 4:4:2, 4:2:3:1 au 4:14:1 na nyingine nyingi..

Swali langu kwanini wasiwe wanaanza na 1:4:4:2 au 1: 4:3:3:1 au kwasababu yenyewe ni constant kwamba kipa lazima awe mmoja..?? Magolie wanabaguliwa Sana asee
timu yoyote duniani kipa ni mmoja

Lakini mabeki unaweza kutumia watatu, wanne ama watano

Viungo unaweza kutumia mmoja, wawili ama watatu

Washambuliaji unaweza kutumia mmoja, wawili ama watatu

Kwa kipa inajulikana ni mmoja tu hamna haja ya kumtaja kwenye mfumo
 
walinzi kwenye mpira ni wachezaji amabo jukumu lao kubwa ni kukaba, Kipa sio mlinzi maama yeye hatoki golini kwenda kukaba. wachezaji wote wanaweza kukaba pia japo jukumu lao kuu sio kukaba, mfano washambuliaji jukumu lao kubwa ni kufunga japo huwa wanarudi nyuma kukaba
utakuwa hujakutana na Neuer wa Bayern Munchen ndio maana unasema hivyo
 
Back
Top Bottom