Safisha safisha ya vihiyo ifike mpk sekondari za umma.

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Serikali ya awamu ya tano ina nia ya dhati ya kurejesha na kuimarisha ubora na hadhi ya Elimu nchini. Ndiyo maana imechukua hatua kali za kuwaondoa vilaza (vihiyo) pale udom na kukifungia chuo kikuu cha St. Joseph. Mwito wangu kwa serikali hii ipitie wanafunzi wote ktk vyuo vikuu vyote ili wale wote wasiostahili hata kama wako mwaka wa mwisho wa masomo yao waondolewe. Hatua hii itasaidia ktk kuokoa fedha zinazo wagharamia vilaza ambao huko mbeleni watakuwa na madhara makubwa ktk taifa letu.

Lakini ili lengo na dhamira njema ya awamu ya tano itimie na kufanikiwa ishushe rungu hadi chini kabisa yaani katika shule za sekondari za umma. Katika shule hizi tumeona kupitia vyombo vya habari kuwa wanafunzi wanaingia sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Sababu kubwa ya jambo hili kutokea ni kujipenyeza kwa siasa ktk elimu. Shule za sekondari za kata zilijengwa kisiasa pasipo kuzingatia mahitaji hivyo zikawa nyingi zaidi. Ili kuzifanya zipate wanafunzi vigezo vya ufaulu vilishushwa kupitiliza. Na bado haikutosheleza ikawa ni zoazoa.

Sasa jambo hili linawaumiza wananchi kwa kuwa Elimu ya msingi na sekondari inagharamiwa na kodi zao ndiyo maana ikaitwa bure. Tunataka tugharamie wanafunzi wenye sifa na wenye tija kwa taifa hapo baadaye.

Mchujo ukifanyika sawa sawa shule nyingi za kata zitabaki wazi. Hizi zigeuzwe kuwa vyuo vya veta vitakavyotoa mafundi mchundo.

Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom