Safari yangu ya Rwanda


Kama nchi hatuwezi kuishi kwa woga eti kwa sababu ya majambazi basi hatuna haja ya kuwa Bureau de change au tawi la benki.
 

Huku ni kutishana Mkuu, viashiria gani vinavyoonekana vitakavyotupelekea sisi kupigana wenyewe kwa wenyewe, mfano wako wa Mmasai sio kabisa katika issue hii, fikiria upya mkuu
 

Napenda kukukosoa kidogo hapa. Nadhani malalamiko yako juu ya uongozi Tanzania yanakita zaidi katika uongozi wa sasa. Kama ni hivyo, naona tathmini yako juu ya JK wetu haiko sawa.
Mimi namwona JK ana moyo na uchungu wa nchi yake. Ni mzalendo (angalia kujitolea mabilioni ya Kikwete). Tatizo lake ni kutokuwa na ufahamu wa kina juu ya nini kifanywe (matamshi yake juu ya umeme kwamba yeye si mvua, bila kujua kuna nchi duniani hazina mvua kabisa na zina umeme saa 24) Infact, ukifuatia matamshi yake utaona kana kwamba anaamini Tanzania inaendelea vizuri sana. Ana upeo mdogo wa fikra(he does not think big)
Hii ndiyo maaana kwa kutatua tatizo la usafiri wa wanawake waja wazito akapendekeza kununuliwa 'Bajaji 400'! Akawaambia wazee wa Dar tumeendelea kwani siku hizi huoni mtu 'mvaa kaniki' n.k.
Tatizo, ukishakuwa na upeo huo mdogo, huoni rushwa kuwa ni tatizo kubwa la kuangamiza taifa. Huoni kuwa kutumia mabilioni ya fedha katika safari za nje na ufujaji ni tatizo. JK amegombania urais mara ya kwanza akidhania ni aina ya kupata uluwa. Kunako mwisho wa kipindi hicho akafahamu kuwa si hivyo. Mara ya pili amegombea kwa sababu ya kuona aibu kama ataishia awamu moja tu atakuwa kioja na kudharauliwa! Pengine pia kwa sababu ya kutaka kupata nafasi ya kujaribu kusawazisha baadhi ya makosa aliyoyafanya huko nyuma. Hii ameielezea hata yeye mwenyewe kwamba miaka 5 ya kwanza alikuwa anajifunza (dry run).
Nadhani hii ndiyo tathmini sahihi ya JK. Hafanyi ayafanyayo kwa kuichukia Tanzania, la. JK ni Mzalendo extremist katika uzalendo wake, kiasi aweza kukuuwa kama wataka kuidhiru Tanzania (kwa mantiki yake yeye ya kuidhuru)
Pia anadhania tumefika. Na si Rwanda wala Kenya wanaweza kufikia hata mavumbi yetu tuliyowaachia nyuma!
 
Ingawa sikubali Rwanda hamna nyumba za nyasi, naweza kusema kichapo mara nyingine huleta discipline. Wanyarwanda usawa huu hawana budi kutia akili tu kwani nchi ndogo, washauana sana, wafanye nini sasa?

Sie tunaojivunia amani na utulivu kila siku tunacheza lelemama.

Ulaya kabla ya Black death walikuwa wazembe sana, kilivyopukutisha watu, watu wakakosa imani na mungu, ikabidi kila mmoja akili kumkichwa, wakaendelea. Ndicho kinachotokea Rwanda sasa hivi to an extent.
 
Rwanda wanaimprove sana sekta ya elimu sana kwa upande wa ICT. ndio unasaidia sana kwa maendeleo. Hivi majuzi, walijaribu kkuajiri walimu toka Kenya

Source

 

Mkuu tathmini yako juu ya mkuu wa kaya inafurahisha na kusikitisha sana. Inasikitisha kwa sababu kiongozi wa nchi huwa na washauri wengi sana ambao kama watatumiwa vizuri huweza kuleta mabadiliko katika nchi. Hapa kiongozi inatakiwa awe msikivu na awe na umakini wa kuchagua ushauri uletwao mezani. Inafurahisha kama yeye anaona tumewatimulia vumbi la mbali Kenya na Rwanda sijui katika lipi.
 

Mkuu Sijali. ama kweli umetoa tathmini ya kisayansi na ya uhakika kumhusu JK. Nikubaliane nawe zaidi na sana katika hilo la UPEO WAKE MDOGO. Naihifadhi hii tathmini yako ili niisome tena mwaka October 2015 atakapomaliza kipindi chake.
 
Sasa hao wanapovuka na mitutu jeshi letu liko wapi? au kazi yao ni kuilinda ccm tu?
 
Ukweli kagame amaejitahidi sana kuiweka Rwanda up up up.

Yani hata mimi nilipofika pale sikuamini nilicho ona Rwanda.
 
Sasa hao wanapovuka na mitutu jeshi letu liko wapi? au kazi yao ni kuilinda ccm tu?

mkuu ule mpaka mrefu sana. jamaa wanavuka na mitumbwi. polisi wameshindwa kuwadhibiti. wanavukia sehemu inaitwa kashasha kila mkuu wa polisi anapajua. sana sana wanakamata Bunduki coz wakishaiba bunduki wanaficha hukuhuku. hadi serikali iliamua kuhamisha kijiji kizima cha kashasha na kuwahamishia kijiji cha mtakuja sababu ya hao majambazi. cha ajabu walihamishwa kifisadi. Mia
 

Mkuu nimeipenda tathmini yako sana angalau umeweka ukweli wa aina na vision za viongozi tulio nao
Hii yafaa sana itumike katika kutathmini kipi tumefanya katika uongozi wa JK kwa miaka kumi
Wapi tulikwama na kipi ambacho kimefanikiwa
Kwa tathmini yako kwa kweli naikubali sana "Upeo mdogo" na kila kitu kwa hawa viongozi wetu haswa kiongozi mkuu anakiona ni cha kawaida
Kujaa kwa nyumba za za udongo kilometa tano kutoka kati kati ya jiji la Dar, foleni za dar, mafuriko, ubovu wa miundo mbinu, rushwa inavyotawala kila sekta bado kweli tunahitaji kiongozi mwenye tathmini ya nini afanye kuyaondoa hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…