Safari ya Tanzania kuelekea kujitegemea

Safari ya Tanzania kuelekea kujitegemea

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
869
Reaction score
1,282
Mapema baada ya uhuru mwaka 1961, Tanzania imekuwa ikiimba wimbo wa kujitegemea kiuchumi na kudumisha ujamaa.

Falsa na sera ya kujitegemea ilipamba moto zaidi baada ya kutangazwa kwa Azimio La Arusha mwaka 1967 ambalo lilizingatia mambo kadhaa ambayo waliamini yangetuwezesha kufikia malengo ya kujitegemea:

1. Kuwa huru kiuchumi: Hii ilimaanisha kupunguza sana kutegemea misaada kutoka nje, mikopo, na uagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi.

2: Elimu ya kujitegemea: Elimu inayopelekea watu kupata ujuzi na maarifa.

3. Maadili: Viongozi walitakiwa wawe na maadili ya kukataa rushwa, kulinda rasilimali za nchi, wasijilimbikizie mali, kufanya kazi kwa bidii, nk.

Miaka 64 tangu tumepata uhuru, Tanzania tuko wapi katika safari yetu hii ya kuelekea KIJIJI CHA KUJITEGEMEA?

Tuanze na uhuru wa kiuchumi:

ONGEZEKO LA DENI LA TAIFA: Tanzania tunakopa sana. Lazima tudhamirie kupunguza kukopa ikiwa kweli tupo serious kufika kijiji cha kujitegemea.

UZALISHAJI BIDHAA NCHINI: Hapa tunatia aibu sana. Tanzania tunaagiza kutoka nje ya nchi vitu vingi sana Mfano: Mchele, ngano, Nafaka, nyama, na bidhaa nyingi za viwandani.

ELIMU: Serikali imewekeza sana kwenye elimu. Tatizo lipo kwenye aina ya wasomi wanaozalishwa huko. Watu wana Vyeti na siyo ujuzi.

MAADILI YA VIONGOZI: Huku kuna janga la kitaifa.

Jana nilisikiliza hotuba nzuri ya rais SSH, alisisitiza tuache maneno na twende tukatende. Na dira yetu bado inalenga pale pale kwenye kujitegemea na uchumi wa kati.

Swali la kujiuliza, je tupo tayari kufikia malengo? Mipango siyo matumizi. Ila bado tunaweza kuvaa magwanda na kuingia vitani.

TUFANYE NINI SASA? TUWE NA:
1. Mifumo Imara itakayo simamia ipasavyo ukasanyaji wa mapato, matumizi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Watu walipe kodi na tuhakikishe inatumika kuleta maendeleo. Tuwekeze kwenye viwanda, utafiti, kilimo endelevu, nk.

2. Elimu (Ujuzi na maarifa): Watu wafundishwe theories kwa ajili ya kurejelea tu ila focus iwe ujuzi na maarifa.

3. Kubana matumizi ya serikali: Matanuzi na makubwa mnoo.

NB: Naunga mkono dira ya Taifa
 
Safari ya matumaini ambayo kila kiya inatakiwa iianze amazing inapenda au haipendi

Hamna alternative isipokuwa kupambana
 
Back
Top Bottom