Safari ya Shibuda alipotoka na aendapo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya Shibuda alipotoka na aendapo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JOHN MADIBA, Jul 11, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SIKU alipotangazwa kufariki dunia baada ya kuwapo taarifa za kutosha za kuugua kwake na namna matibabu yanavyoendelea, watu wengi waliamini sasa ndiyo mwisho wa hali ya utulivu na maelewano nchini Tanzania.
  Watu waliamini hivyo kutokana na namna alivyoheshimiwa kwa uwezo wake mkubwa wa kunyoosha mambo, kiasi cha Tanzania kupewa jina la ‘Kisiwa cha Amani’. Ninayemsema hapa si mtu mwingine, ila ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
  Sasa ni zaidi ya miaka kumi tangu alipofariki na mambo hapa Tanzania yanasonga mbele, japo kuna tofauti nyingi tu. Si hoja sana kwani hata nyakati nazo ni tofauti.
  Lakini pamoja na mabadiliko yaliyopo, nguvu ya hoja ya Baba wa Taifa bado inaendelea kuonekana katika mambo kadhaa kwa mtu anayepata nafasi ya kusikiliza hotuba zake na kisha kuziakisi na yanayoendelea kutokea nchini hivi sasa.
  Na kutokana na ukweli huo, mimi naamini kifo cha Baba wa Taifa kilitokea wakati sahihi, kwani tayari alishatutengenezea misingi kwa utendaji wake; na alishatuachia urithi wa kutosha kupitia maandiko yake mbalimbali hasa vitabu pamoja na kumbukumbu hizo za hotuba.
  Kwa mwenendo wa mambo ya sasa, leo nimeikumbuka hotuba yake inayohusu ‘dhambi ya ubaguzi’ aliyowahi kuitoa alipozungumzia sakata la mjadala wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliounda Tanzania.
  Najua mjadala huo bado unaendelea, lakini hoja yangu leo si suala la Muungano. Ninachotaka kuzungumzia hapa ni dhambi ya ubaguzi nikiihusisha na sakata la Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA), ambaye hivi karibuni aliingia katika malumbano makubwa na chama chake.
  Kisa cha sakata hilo sote tunakifahamu. Mzozo wa posho za vikao wanazopewa wabunge. Wakati CHADEMA ikiimarisha hoja yake kutaka posho hizo zifutwe na badala yake fedha husika zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi, Shibuda, alishangaza wengi aliposimama bungeni si tu kupinga zifutwe, bali akataka waongezewe kabisa.
  Akichangua mjadala wa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2011/2012, Shibuda aliitaka serikali iongeze posho za wabunge kutoka Sh. 150,000 hadi Sh. 500,000 kwa siku, kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi.
  Kilichofuata hapo ni moto kukolea, maneno, malumbano na kashfa kadhaa kutolewa na mbunge huyo baada ya chama chake kusema kitamjadili na huenda akafukuzwa kwani kauli yake ya bungeni imetafsiriwa kuwa ni usaliti kwa CHADEMA na upinzani kwa ujumla.
  Shibuda ukimwangalia katika hili, unaweza kumwona katika pande mbili. Kwanza, shujaa. Kweli unaweza kumwona ni shujaa maana kusimama bungeni kupinga kile ambacho chama chake kinaamini kuwa ndiyo ‘mtaji’ wa sasa wa kisiasa, si jambo jepesi.
  Pili, unaweza kumwona Shibuda kuwa ni msaliti. Kama vile CHADEMA ilivyomtafsiri.
  Lakini mimi namwangalia Shibuda na kumwona kuwa ni aina ya viongozi wasiofaa. Ni mmoja wa viongozi mwenye umimi zaidi na hali hiyo ni zao la ubaguzi wa kifikra alionao moyoni mwake.
  Dhambi hiyo ya ubaguzi aliyonayo ndiyo inamtafuna sasa, kama Mwalimu alivyosema kuwa dhambi ya ubaguzi ni mbaya sawa na kula nyama ya mtu, kwani ukiila utaendelea tu.
  Kwanini nasema hivyo? Mwaka jana wakati wa vuguvugu la uchaguzi mkuu, kwa ngazi ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shibuda aliondolewa katika kinyang’anyiro hicho wakati wa mchakato wa kura za maoni. CCM ilifanya hivyo chini ya utaratibu wake wa kawaida.
  Lakini Shibuda hakukubali. Kutokukubali si dhambi kwani chama chake kina taratibu zaidi, akaamua kuondoka CCM huku akitoa maneno mengi ya kashfa.
  Aliituhumu CCM kupoteza dira, akisema uchaguzi huo umejaa rushwa na ufisadi na kwamba kulikuwa na mpango wa kumtoa yeye ili asiendelee kupigania maslahi ya wananchi wa jimbo lake.
  Pia katika moja ya mahojiano yake Shibuda aliwahi kusema ndani ya CCM kuna viongozi wanaoilewa vema misingi na maadili ya chama, lakini wapo wasiojua chochote kuhusu chama chao.
  Hao aliwaita ni wale waliovunwa kwa njia ya ufisadi na uanachama wa papo kwa papo. Hao ndio aliosema wanaivuruga CCM.
  Joto lake ndani ya CCM halikuanzia mwaka jana, mwaka juzi katika gazeti la Mwanahalisi la Septemba Nane, Shibuda aliwahi kukaririwa akisema CCM inapaganyishwa na viongozi wasio na elimu ya madrasa ya kukijua chama.
  Alisema wajibu wa kwanza wa mwanachama ni kutii kanuni na imani za chama. Haiwezekani kuhubiri kuondoa unyonge, lakini wakati huohuo unashabikia unyonyaji.
  Akaendelea kusema CCM hakitakuwa chama cha siasa tena, utakuwa ni mkusanyiko wa watu waliokutana katika basi moja, lakini wakiwa wanaelekea safari tofauti.
  Na ndiyo maana alipoondoka CCM mwaka jana kwenye joto la uchaguzi akaonekana shujaa. Akatua CHADEMA kwa mtindo wa uanachama wa papo kwa papo (aliouponda kwa CCM), amekaa huko kwa takribani mwaka na sasa amekorogana na hao pia.
  Kwa mujibu wa gazeti hili la Julai 3, Shibuda alikaririwa akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote.
  Alisema kwamba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto, wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho.
  Alisema sura ya CHADEMA ukiwa nje ya chama ni tofauti na sura ya CHADEMA ya ndani, ni tofauti kabisa kwa sababu yanayofanyika humo ni mambo ya ajabu.
  Amemtuhumu Mbowe kuendesha chama kibabe na anaungwa mkono na Zitto ambaye anaonekana kuwa na tabia ya ukuwadi na unafiki.
  Ndiyo maana nimesema mimi mimi namwangalia Shibuda na kumwona kuwa ni aina ya viongozi wasiofaa. Ni mmoja wa viongozi mwenye umimi zaidi na hali hiyo ni zao la ubaguzi wa kifikra alionao moyoni mwake.
  Najiuliza huyu Shibuda alipokuwa CCM alitujengea picha kuwa wenzake ndani ya chama hicho walikuwa wabaya, mafisadi, wala rushwa, wasiojali maslahi ya watu bali ya kwao tu.
  Kaenda CHADEMA na kwenyewe anawashutumu wenzake kwa hayo hayo baada ya kukaa kwa takribani mwaka mmoja, hivi huyu ni mtu makini kweli? Au anayetaka kutumia jukwaa la siasa kupata mkate na kusogeza siku mbele?
  Nasema hivi kwa kuwa naamini kiongozi wa kweli ni yule ambaye baada ya kubaini alipo kuna tatizo, basi kazi yake inayofuata ni kulishughulikia tatizo hilo akiwa ndani ili kusafisha uchafu.
  Kiu ya kiongozi wa kweli ni kuona analimaliza tatizo hilo akiwa humo humo ili akitoka nje atoke kifua mbele kuwa ameweza kutatua tatizo. Hiyo ndiyo sifa ya kiongozi.
  Hata katika nyumba, hivi baba wa kweli anayestahili kupewa heshima ni yupi kati ya hawa; Yule anayekuwa wa kwanza kukimbilia nje na kupiga kelele kwasababu kuna nyoka kaingia ndani mwake, au yule anayepambana na nyoka ili ammalize na watu waendelee kukaa nyumbani humo kwa amani?
  Alipokuwa CCM nyoka aliingia. Leo yupo CHADEMA nyoka pia ameingia. Na nyoka huyo si mwingine, ila ni kutofautiana kifikra.
  Hivyo mimi ningemwona Shibuda kuwa ni kiongozi makini kama angeonekana kushughulikia kutofautiana huko kwa kufuata misingi ya chama. Hakufanya hivyo alipokuwa CCM na sasa hafanyi hivyo ndani ya CHADEMA, vyama vyote hivyo vina taratibu zake za kushughulikia mambo kwa mujibu wa katiba zao.
  Hata waswahili wanasema unapomnyooshea kidole mwenzako kuwa ni mbaya, jiulize siri iliyomo kuhusu vile vidole vitatu ambavyo vinakuwa vimekunjika kukuelekea wewe.
  Na katika Biblia, kitabu kitakatifu kinachoongoza dini ya ukristu ambayo nashawishika kuamini Shibuda ni mfuasi wake, kuna mahali Yesu Kristu anasema kabla ya hujashughulika kutoa kibanzi katika jicho la mwenzako, hakikisha umetoa boriti katika jicho lako kwanza.
  Mifano hiyo miwili yote inatufundisha kujitathimini wenyewe kwanza kabla ya kuanza kuwashutumu wengine. Hivi Shibuda yuko sahihi wakati wote kweli?
  Alipoingia CHADEMA moja kwa moja akapanda jukwaani kunadiwa ili aupate ubunge, alikuwa ameifahamu falsafa na imani ya chama hicho? Ni wazi Shibuda hakupata muda huo. Yeye alikimbilia ubunge na si kutumikia chama. Ndiyo maana nasema Shibuda ni mbinafsi.
  Sasa ana tofauti gani na wale aliosema ndiyo wanaivuruga CCM kwa vile walichukuliwa kwa mtindo wa uanachama wa papo kwa papo. Na yeye leo si anaivuruga CHADEMA?
  Aliposema hawezi kuinyamazia CCM inayohubiri kuondoa unyonge, lakini wakati huohuo inashabikia unyonyaji kwa wananchi, kuna tofauti gani na anachokifanya sasa?
  Ni kweli wabunge kwa nyadhifa zao wana mahitaji makubwa kifedha, lakini mahitaji yao hayapaswi kuangalia na hali za wananchi?
  Wenzake wanasema angalau hizo Sh. 150,000 zikasaidie kununulia dawa, kusogeza huduma za maji, kununua vitabu vya mashuleni kwa kuwa wao wabunge wanamshahara mnono kiasi, yeye anataka wabunge walipwe Sh. 500,000 kwa siku ambazo ni mara tatu ya mshahara wa kima cha chini, huko ni kujali wanyonge?
  Hivi Maswa Magharibi jimboni kwake, wananchi wote wana huduma ya maji safi na salama, shule zao za msingi zote zina madawati, kila kijiji kina zahanati yenye dawa za kutosha, vifaa vya utabibu?
  Leo anaposema anapanga kuandaa mikutano kuanzia jimboni kwake kuwaeleza watu waliomchagua mabaya ya Mbowe na Zitto, kwani kujua mabaya ya wanasiasa hao ndiyo shida ya watu wa Maswa Magharibi?
  Shibuda alipaswa (alipokuwa CCM) na sasa anapaswa ndani ya CHADEMA kushughulikia mambo kwa misingi ya taratibu za kichama ili anyooshe palipopinda. Akifanya hivyo ndiyo watu wenye akili watamwona kuwa ni mwanasiasa safi na kiongozi makini.
  Lakini kukimbilia kupiga kelele nje na kusema haogopi kufukuzwa, ni silaha ‘makini’ kwa kiongozi dhaifu.
  Au naye anakiri sasa kuwa amepanda basi asilojua linakokwenda? Kwamba safari yake ilikuwa kusaka ubunge na kupata maslahi ya wadhifa huo, wakati wenzake wana jingine vichwani mwao?
  View attachment 33687
  ........................JE ATAFIKA MAONI YAKOOOOOOOOOOOOOOOO...........
   
 2. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 3. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni bora atemwe mapema c wa kuvumilia kabisa,mnafiki mkubwa
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  mie naona kumjadili huyu bwana ni sawa na kujitia wendawazimu tu.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  shibuda ni malaya wa kisiasa
   
 6. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  kweli nimeamini chadema hawajui demokrasia. huyu shibuda alipokuwa ccm alikuwa anasema hovyo sana sikuwahi kusikia hata wakimjadili. chama cha demokrasia kinataka kumnyamazisha shibuda akae kimya.

  hicho chama bila kumwabudu mbowe na baba mkwe wake weye ni mtu wa kupita tu.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo la Shibuda ni njaa

  CHADEMA mweleweni huyu Shibuda ana njaa kali sana
   
 8. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  makala nzuri...shibuda si riziki huyu bwana..
   
 9. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  who z shibuda???sina muda wa kumjadili huyu mropokaji!
   
 10. L

  Lua JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yaani ukimuona "kama amerogwa vile"
   
 11. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,825
  Trophy Points: 280
  Nawasihi chadema wampe nafasi ya kujisahihisha. Wasilete picha mbaya kwa wapinzani wao. Sasa hivi Chadema ni kioo cha jamii kisiasa, sasa wakianza kufanya hivi hawataeleweka.
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,710
  Trophy Points: 280
  Huyu dawa yake ni kumpotezea tu wasimpe ushirikiano wamtenge mpaka ajing'atue mwenyewe kwani wakimfukuza atakimbilai mahakamani.Huyu ni CHANGUDOA WA KISIASA.
   
 13. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni cd namba moja wa siasa na mpenda sifa mkubwa!
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  cdm watuonyeshe watanzania kutomvumilia mtu aliye kinyume na maslahi ya umma, bila hivyo watashindwa kunishawishi kuwapa ridhaa kuniongoza, wajitofautishe na ccm ambao wametujazia wezi kwa kuwalea wahalifu kama chenge, lowasa, karamagi, rostam, jk, ngeleja, polisi wauao raia, mawaziri wavunao wasichopanda...................
   
Loading...