Safari siyo kifo.......Babu DC !!

Mambo yanaenda vizuri babu,babu mwenzako asprin hajambo mzima kabisa ila bado hajaacha mchezo wake wa kujilimbikizia wajukuu.

Hilo tutalifanyia kaza kwa kasi mpya...nguvu mpya na....mpya! Serikali yooote itabidi iwekeze nguvu zake hapo...Naona linakaribia kuwa janga zaidi ya mgawo wa umeme wa Tanesco-Dowans-RA syndicate!
 
Karibu tena babu DC, tulikumiss sana hasa yule babu mwingine alipozidisha micharuko,,lol

Hili sasa naona linakuwa janga...Kamati ya wazee italifanyia kazi...Kijijini kwetu lazima kila kitu kiende kwa kanuni za Bunge na Spika wetu yuko makini....

Point taken!
 
Babu nakuona ndani, hapo napata mzuka
Tulidhani uko ndani, kumbe angani waruka
Karibu tupe kampani, mana tulikukumbuka,
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Wajukuu tulizongwa, nayo mengi majukumu,
Si kwamba tulihongwa, babu tusikusalimu,
Na wala hatukugongwa, gongo la mboto mabomu

Tulikuwa na darasa, la kutongoza kisasa,
Tulipata na mikasa, ya maisha na siasa,
Vingi vilijiri visa, vicheko hatukukosa,

Hongera zake mwenzio, subira amejaliwa,
Japo hakuna uzio, ye hakuchakachuliwa,
Angekuwa wa mwambao, sasa ungeshachachawa
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani
 
Hilo tutalifanyia kaza kwa kasi mpya...nguvu mpya na....mpya! Serikali yooote itabidi iwekeze nguvu zake hapo...Naona linakaribia kuwa janga zaidi ya mgawo wa umeme wa Tanesco-Dowans-RA syndicate!
Babu kuna haja ya kuunda kamati vinginevyo anaweza kuwa RA upande wa wajukuu halafu sisi tukakosa hata kupata mke.
 
Babu nakuona ndani, hapo napata mzuka
Tulidhani uko ndani, kumbe angani waruka
Karibu tupe kampani, mana tulikukumbuka,
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Wajukuu tulizongwa, nayo mengi majukumu,
Si kwamba tulihongwa, babu tusikusalimu,
Na wala hatukugongwa, gongo la mboto mabomu
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Tulikuwa na darasa, la kutongoza kisasa,
Tulipata na mikasa, ya maisha na siasa,
Vingi vilijiri visa, vicheko hatukukosa,
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Hongera zake mwenzio, subira amejaliwa,
Japo hakuna uzio, ye hakuchakachuliwa,
Angekuwa wa mwambao, sasa ungeshachachawa
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani
Miss Judith mzima wewe
 
Babu habari za asubuhi mpwa wako sijambo mzima kabisa niko kwenye mihangahiko ya kununua mbegu za mahindi kwa ajili ya msimu huu
We kweli sio mkulima, wenzako tunapalilia mahindi wewe ndio unanunua mbegu, zihifadhi hizo mbegu ni kwa ajili ya msimu ujao
Ndo maana nakupenda mkwe wangu ...yaani hapa mwanangu halali njaa hata siku moja kijana unasoma sana nyakati
Mwanao atakufa njaa......huu sio msimu wa kununua mbegu, huyo mtoto wa mjini......lol!!!
 
We kweli sio mkulima, wenzako tunapalilia mahindi wewe ndio unanunua mbegu, zihifadhi hizo mbegu ni kwa ajili ya msimu ujao

Mwanao atakufa njaa......huu sio msimu wa kununua mbegu, huyo mtoto wa mjini......lol!!!
Ahaa ahaa katavi unaharibu mingo zangu.
 
Back
Top Bottom