Safari siyo kifo.......Babu DC !!

Babu nakuona ndani, hapo napata mzuka
Tulidhani uko ndani, kumbe angani waruka
Karibu tupe kampani, mana tulikukumbuka,
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Wajukuu tulizongwa, nayo mengi majukumu,
Si kwamba tulihongwa, babu tusikusalimu,
Na wala hatukugongwa, gongo la mboto mabomu
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Tulikuwa na darasa, la kutongoza kisasa,
Tulipata na mikasa, ya maisha na siasa,
Vingi vilijiri visa, vicheko hatukukosa,
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Hongera zake mwenzio, subira amejaliwa,
Japo hakuna uzio, ye hakuchakachuliwa,
Angekuwa wa mwambao, sasa ungeshachachawa
Kweli safari si kifo, karibu tena nyumbani

Ahsante sana Judith,

Nimefurahi sana kupata mistari yako....Ndo maana nili-miss sana hili jukwaa!

Ubarikiwe sana tena sana....Ikiwezekana sala za Babu zisikilizwe na Mnyazi Mungu (Allah) akudondoshee mapacha kabla mwaka huu haujayoyoma!!

Babu DC.
 
Mambo yanaenda vizuri babu,babu mwenzako asprin hajambo mzima kabisa ila bado hajaacha mchezo wake wa kujilimbikizia wajukuu.
Huyu bila ajizi kanitaja hadharani!

Karibu tena babu DC, tulikumiss sana hasa yule babu mwingine alipozidisha micharuko,,lol
Huyu anajua anamaanisha babu gani. Me is watching tu!

Ngoja aamke ndo utamtambua shauri yako
Huyu ndio mtetezi halisi wa babu kikongwe! Anaandaliwa zawadi yake huyu!

Babu kuna haja ya kuunda kamati vinginevyo anaweza kuwa RA upande wa wajukuu halafu sisi tukakosa hata kupata mke.
Huyu akaamua kukufuru kabisa!
Hili sasa naona linakuwa janga...Kamati ya wazee italifanyia kazi...Kijijini kwetu lazima kila kitu kiende kwa kanuni za Bunge na Spika wetu yuko makini....

Point taken!
Na huyu babu wa makamo aliyekuwa kapotea njia akaingia kingi! Dah! Karibu tena hemani!

Anyway, babu kikongwe anarudi kitandani!
 
Huyu ndio mtetezi halisi wa babu kikongwe! Anaandaliwa zawadi yake huyu!

Huwa nakwambia siku zote mie ndo mtetezi wako unaona sasa walivyokuwa wanakusema wakati haupo
 
Yaani we njoo streiti Kingista ruum 106....kwenye godoro la comfy:rain:
 
Ahsante sana Judith,

Nimefurahi sana kupata mistari yako....Ndo maana nili-miss sana hili jukwaa!

Ubarikiwe sana tena sana....Ikiwezekana sala za Babu zisikilizwe na Mnyazi Mungu (Allah) akudondoshee mapanya kabla mwaka huu haujayoyoma!!

Babu DC.

haha mbavu sina mie, kinywani tele kicheko,
baraka sasa zinijie, kwa wake babu upako,
wenye wivu na wajipalie, makaa wawe ukoko,
zikujae nyingi heri, uwe wa afya buheri,

mema umeniombea, yanifikie mapanya,
ni lugha ya kulongea, yaweza moyo kuponya,
kondeni nitajongea, Baraka kuzikusanya

Ohhhhhhhhhhhhhhh Judith...kumbe kweli babu kazeeka!! Atakuombeaje mapanya? Ni mapacha bwana, tena triplets au zaidi!!
 
Huyu ndio mtetezi halisi wa babu kikongwe! Anaandaliwa zawadi yake huyu!

Huwa nakwambia siku zote mie ndo mtetezi wako unaona sasa walivyokuwa wanakusema wakati haupo
Khee kheee unaingizwa mkenge kama machinga
 
Huyu bila ajizi kanitaja hadharani!

Huyu anajua anamaanisha babu gani. Me is watching tu!

Huyu ndio mtetezi halisi wa babu kikongwe! Anaandaliwa zawadi yake huyu!

Huyu akaamua kukufuru kabisa!
Na huyu babu wa makamo aliyekuwa kapotea njia akaingia kingi! Dah! Karibu tena hemani!

Anyway, babu kikongwe anarudi kitandani!
Khee Kheee babu bepari anarudi guest
 
Yaani we njoo streiti Kingista ruum 106....kwenye godoro la comfy:rain:

Babu kaza buti................ huyo mjukuu amechanganyikiwa na kupotelewa na BE, na jana alisema kuwa TF ni serengeti boy hamtaki, nahisi kwa vikongwe ataridhia
 
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh FP, hapa kunani? Kumbe hii kitu inahitaji madalali pia?

Ngoja nikamtumtafute LD anipatie kikombe cha chai mie!
 
ooooooooooooppppppppps, kumbe nafanya udalala! ha haaaaaaaaaaaaa. namsaidia huyo binti anaonekana bila infii hawezi kusimama
 
Ohhhhhhhhhhhhhhh Judith...kumbe kweli babu kazeeka!! Atakuombeaje mapanya? Ni mapacha bwana, tena triplets au zaidi!!

haha bado umo babu, hayo mambo ya safari,
kama si ule ulabu, basi ni nyingi futari,
ni zaidi ya kutibu, mapacha tele fahari,
sasa ninalo jawabu, la uzazi wenye heri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom