"Safari hii risasi haitakukosa!"- ujumbe wa kitisho dhidi ya Trump kutoka Iran

"Safari hii risasi haitakukosa!"- ujumbe wa kitisho dhidi ya Trump kutoka Iran

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,323
Reaction score
11,762
Ripoti za vyombo vya habari vinavyoaminika zinaonyesha kuwa runinga ya serikali ya Iran ilionyesha ujumbe uliotajwa kama njia ya tishio dhidi ya Donald Trump ikisema “Safari hii risasi haitakosa tena shabaha”/“this time the bullet won’t miss the target.”

Hii ilionyeshwa sambamba na picha/video inayoonyesha tukio la jaribio la kuua Trump mwaka 2024.
images (40).jpeg


Matangazo hayo yalitokea katikati ya mvutano mkubwa baina ya Marekani na Iran, hasa baada ya Trump kuzungumzia uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran na hali ya ghasia ndani ya Iran.

Ujumbe huo umejibiwa kama tishio la moja kwa moja.
 
Kama ni kweli basi ayatollah Khamenei hana muda mrefu madarakani
 
Kama ni kweli basi ayatollah Khamenei hana muda mrefu madarakani
Marekani imehangaika sana na huyu jamaa kwa muda mrefu. Na kila mara "mawazo" hayo yameendelea kutawala kama njia ya kujipa moyo.
 
Ni kweli, Trump atapata anachokitafuta....kama si kutoka Iran basi kutika kwingine ila atakipata wallah,

Sasahivi ameshakuwa adui na Wa danish na nchi zote za scandinavia, Canada n.k kwsbb ya kuitaka ardhi ya Greenland ...Tayari Denmark imepeleka majeshi yake karibu na Greenland na wana support kutoka nchi zingine
 
Back
Top Bottom