Saed Kubenea: Ndumilakuwili mbobezi

Kubenea ni mchumia tumbo, unategemea nini zaidi ya kuchumia tumbo lake na "kula matapishi yake"
 
People's......... People's...... CCM hoyeeeeee. Naomba kura zote za Urais mnipe. Za udiwani na ubunge, muwappe wagombea wa CCM.
People.... People... Mabadiliko?

Nyumbu bwana. By the way. Nilikuwa chadema damu hadi mlipoliuza chama kwa Mafisadi. Ndio maana siwezi kuwaamini tena

Kubali kataa ccm ni Nyumbu wakubwa tena wale wa Serengeti , angalia Serikali iliwagawia viwanja mabondeni ikapokea Kodi za viwanja na kuweka mawe huduma za maji , umeme na ofisi za ccm huko wamekula pesa zao miaka yote hawakujali kuwa wapo bondeni leo wamewabomolea nyumba tena wamevunja hata zile ambazo hazipo kwenye maeneo hatarishi sasa kesi zinaanza Mahakama , ccm wote ni Nyumbu ndiyo maana mmeshindwa kung'amua kuwa ili Nchi iwe na maendeleo lazima kuwepo na maadili ya kitaifa yaani kuanzia kwenye familia , mtaani nk, Wale wote ambao eti watakuwa viongozi wa kesho wanavaa milegezo kata k, vimini na vinguo vya hovyo Magufuli anaogopa kuthubutu kukemea Kama Uganda unategemea nini kesho? Ni vigumu Nchi kupiga Hatua Kama mila na desturi na maadili hakuna .
 
Last edited by a moderator:
Nyumbu at It's best..... Kweli si kweli?.

Wewe kijana wa Lumumba mshauri mwezio Seif Rashid awe anaweka na nyaraka ambatanishii..

Round hii hivyo vi buku7 vimefyekwa mnekua kama mapopo mnatafuta pakufiidia..jipangeni upya then mje tema..mai..ti
 
Last edited by a moderator:
Sasa mpeleke mahakamani ili tujue kwamba kweli Kubenea ni Ndumilakuwili. Sio unakuja kupotezea muda humu. Sisiemu yote imeoza wenye akili ndiyo wanaelewa. Mazuzu tu kama wewe ndiyo yamebaki.

Msukule huu, ewe Mwenyezi Mungu mjaalie akili zaidi ya zile za kufahanu msalani tu. Huyu nyumbu akili zero kabisaa mweupeee kichwa anafungia nywele.

Ni mpuuzi kuliko wapuuzi wote walio jf, Mungu msaidie.
 
Na Seif Rashid

SAED Kubena, Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ndumilakuwili. Ni kigeugeu. Haaminiki.

Anataka kupanda farasi wengi kwa wakati mmoja; lakini kwa barabara tofauti. Anasukumwa na maslahi binafsi na pia tamaa yake kubwa ya kusaka fedha na umaarufu.

Leo anaweza kusema hili, kesho akasema lile. Jana alisema hili, lakini keshokutwa atasema jambo ambalo alikuwa akilipinga jana, juzi na hata leo.

Pamoja na tabia zake hizi kujulikana kwa wengi, bado Kubenea anataka kujulikana kwa wengi kama mwandishi wa habari mzalendo, mpinga ufisadi. Amesahau ule msemo kwamba unaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati mmoja lakini huwezi kuwadanganya watu wote, muda wote.

Kwa hakika, Kubenea ni mtu wa hovyo. Kimsingi, katika historia ya Tanzania, haijapata kutokea kwa mtu wa hovyo kama Saed Kubenea.

Kuna watu hawamfahamu Kubenea. Kwa sababu ameanza kuishi maisha feki, akionekana wazi kutaka kutafuta umaarufu mpya kwa ubunge alioupata, umefika sasa wakati wa kumfunua Kubenea huyu ?aliyemwagiwa tindikali? ingawa uso wake hauna hata alama ya kovu moja.

Tindikali gani anayomwagiwa mtu na halafu asiwe hata na kovu?

Saed Kubenea ni nani?

Saed Kubenea ni mwandishi wa habari. Hadi leo, hakuna anayejua hasa kiwango chake cha elimu lakini inajulikana hakuwahi kumaliza kidato cha nne. Ana ndugu yake aishiye Bagamoyo mwenye jina la Said (sio Saed) Kubenea na yapo madai kuwa mmiliki huyu wa gazeti la MwanaHALISI anatumia jina la nduguye huyo (na vyeti?) ingawa amefanya ?usanii? wa kujiiita SAED badala ya SAID.

Alianza kufahamika mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati huo akiwa mwandishi wa kujitegemea na makala zake zikianza kuchapwa kwenye gazeti lililokuwa maarufu la RAI. Wakati huo, Saed Kubenea, alikuwa akijitambulisha kama mwana CCM kindakindaki.

Kwa vile hakuwa na ajira maalumu, Kubenea alikuwa akiishi kwa kutumia makala alizokuwa akiandikia wanasiasa. Ilivyokuwa ni kwamba akikuandikia makala, unamlipa kidogo. Na kwa vile wanasiasa waliokuwa na hela wakati huo walikuwa wa CCM, Kubenea akawa mwandishi wa CCM.

Wamiliki wa RAI, akina Jenerali Ulimwengu, walipata taarifa za vitendo hivi vya Kubenea na wakakasirishwa sana hasa ikizingatiwa alikuwa akijitambulisha kama mwajiriwa wa gazeti hilo jambo ambalo halikuwa la kweli.

Siku moja akafanya kosa la kitaaluma kwenye mahojiano na mmoja wa viongozi wa CCM Mkoa wa Kagera. Uvumilivu wa mabosi wa Kubenea ukawa umefikia ukomo na wakamfukuza kufanya kazi nao. Taarifa hiyo ilitoka kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la RAIA kwamba Kubenea si mtu wao tena.

Huo ukawa mwanzo wa maisha ya kubangaiza ya Kubenea. Kwa kipindi cha takribani miaka mitatu, Kubenea akawa anaishi kwa kuwapiga mizinga wanasiasa kama Salum Londa na Mwita Gachuma. Hawa ndiyo wafadhili waliomweka mjini Kubenea.

Ndipo Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akajitokeza na kumwokoa Kubenea. Akamchukua mwandishi huyo na kuwa msaidizi wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Baadhi ya wana CUF hawakufurahishwa na uamuzi wa Lipumba kumchukua Kubenea lakini Profesa alishikilia msimamo wake.

Hadi leo, wapo wana CUF wanaoamini kuwa Kubenea alihusika na tukio la Lipumba kuibiwa kompyuta mpakato yake (laptop) kwenye siku za mwisho za kampeni hiyo. Lipumba ndiye aliyekuwa mgombea tishio wa upinzani kwenye uchaguzi huo na laptop hiyo ilikuwa na kila taarifa.

Kwa sababu ya mahusiano ya nyuma baina ya Kubenea na CCM, iliaminika kuwa pengine Kubenea aliichukua na kuipeleka kwa chama tawala ili kijue taarifa za CUF. Hadi leo kompyuta ile haijawahi kupatikana.

Aliyewaunganisha Lipumba na Kubenea alikuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed. Baada ya kampeni zile, Lipumba alimpa Kubenea mtaji wa kuanzisha gazeti ambalo baadaye lilikuja kufahamika kwa jina la HaliHalisi na kutumika kama gazeti rasmi la kambi ya upinzani bungeni upinzani.

Baadaye, Kubenea na Hamad Rashid wakagombana na gazeti la HaliHalisi likafa. Hadi wakati huo, Kubenea alikuwa akijitambulisha kama mwana CUF wa kufa au kupona na aliandika makala nyingi za kukisifu pamoja na Lipumba.

Kufa kwa HaliHalisi na Kubenea kuhamia CHADEMA

Bunge la 2005/2010, lilimtambulisha Kubenea kwa wabunge wengine vijana kama Zitto Kabwe. Taratibu Kubenea, daima mtafuta fursa, akaona anaweza kupata hela CHADEMA kuliko CUF. Akaanza kujisogeza kwa akina Zitto, Mbowe, Wilbrod Slaa na Anthony Komu.

Alijisogeza kwa Komu kiasi kwamba akaamua kumuoa aliyekuwa binti wa kazi (House Girl) wa Komu. Kuna dhana kwamba Kubenea na Komu, ambaye sasa ni Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema) na mmiliki mwenza wa gazeti la MwanaHALISI, wameoa nyumba moja. Hii si kweli. Ukweli ni kwamba Kubenea amemuoa binti aliyekuwa akifanya kazi za ndani kwa Komu !

Baada ya kufa kwa HaliHalisi, Kubenea akarudu tena Kijiweni. Akaanza msoto. Kwa huruma, Zitto na mwenzake, Halima Mdee, wakampa mtaji wa kuanzisha gazeti la MwanaHALISI. Gazeti likaja kupaa kwa sababu ya taarifa ambazo wabunge hao wa Chadema walikuwa wakimmegea swahiba wao huyo.

Taratibu Kubenea akaanza kuwa mwana CHADEMA. Akajichomeka na kuwa mmoja wa marafiki wa karibu wa Zitto Kabwe. Hawa jamaa wakawa marafiki kiasi kwamba Kubenea akawa anakwenda kwenye vikao vya Bunge vya Dodoma kwa kutumia gari la Zitto.

Wakati wa urafiki wao, ilikuwa kawaida kwa Kubenea kulala nyumbani kwa Zitto. Zipo nyakati ambazo Zitto aliamua kuishi hotelini ili amwachie nyumba Kubenea aishi kwa ?kujiachia? atakavyo.

Changamoto mpya ikajitokeza. Ili Chadema ipae, ilikuwa lazima CUF iangushwe. Kubenea akajipa ?kazi ya kuibomoa CUF?. MwanaHALISI likaanza kazi rasmi ya kukibomoa chama hicho.

Kubenea akaanza kuandika makala za kumponda Lipumba, Maalim Seif na Ismail Jussa. Lipumba akaanza kuandikwa kama ?msomi asiye na mvuto?. Kubenea akasahau wema wote aliotendewa na Lipumba wakati akiwa ?kijiweni?.

Wakati huohuo, Kubenea akaanza kuandika makala za kuwapamba akina Zitto, Slaa na Mbowe. Umaarufu wa Chadema na akina Zitto ukaanza kupaa. Hatimaye, Kubenea akakaribishwa kwenye familia ya Chadema. Akaanza kujitambulisha kama mwana CHADEMA KINDAKINDAKI.

Kwenye kuelekea mwaka 2010, vita mpya ikaibuka ndani ya CCM. Ilikuwa ni kati ya waliokuwa wakiitwa MAFISADI na wapinga UFISADI.

Mmoja wa wafadhili wa kudumu wa Kubenea, Reginald Mengi, alikuwa kwenye kambi ya wapinga ufisadi. Kubenea naye akaingia kwenye hiyo vita baada ya kubaini kuwa pana fursa ya kujipatia kipato.

Akawa kwenye kundi la wapinga ufisadi na akajijengea ukaribu na watu kama Nape Nnauye, Benard Membe, Samuel Sitta na Harrison Mwakyembe.

Gazeti la MwanaHALISI likaanza kuibua kashfa za kifisadi na kuwaibua mafisadi. Katika namna ya kipekee kabisa, gazeti hilo likaanza kumshughulikia Edward Lowassa na Rostam Aziz waliokuwa wakionekana kama vinara wa kundi la walioitwa mafisadi.

Wakati huo, kila toleo la MwanaHALISI lilikuwa walau na habari moja ya Lowassa au Rostam. Kubenea akawa anaapa kwenye makala zake kwamba kwenye historia ya Tanzania, hapajawahi kutokea mafisadi kama Lowassa, Rostam na Andrew Chenge.

Siku moja, kwa ujasiri wa kifisadi kabisa, akaandika kwamba kazi ya kumsafisha Lowassa haiwezekani kwani hawezi kusafishika kwa ?mchanga wala dodoki?.

Mwaka 2011, Zitto akaanza kuonyesha dalili za kutaka kuwania Uenyekiti wa Chadema. Lakini wakati huo, Kubenea tayari alishajenga mahusiano ya kibiashara na kimaslahi na kundi la Mbowe. Akaona atafaidi zaidi akiwa nalo kuliko akiwa na Zitto.

Zitto alipotangaza azma yake hiyo, Kubenea akaingia naye vitani. Gazeti la MwanaHALISI likaanza kutumika kuandika mabaya yote ya Zitto. Mbunge huyo wa Kigoma Mjini sasa akawa hata akikohoa ni kosa kwa Kubenea.

Kama alivyofanya kwa Lipumba, Kubenea sasa akageuza dozi kwa Zitto. Anapolinda maslahi yake, Kubenea ni katili kuliko wanyama. Wakati mama mzazi wa Zitto alipokuwa kitandani kwa ugonjwa, Kubenea aliendelea kumshambulia Zitto na wakati mwingine akilitumia jina la mama huyo (mola amrehemu).

Zitto akageuzwa kuwa adui wa Chadema na Watanzania. Ni bahati tu kwamba mwanasiasa huyo wa chama cha ACT Wazalendo ni mbunifu na mahiri lakini bila hivyo leo angekuwa amepotezwa na Kubenea ambaye aliwahi kumfadhili huko nyuma.

Kubenea sasa anatumia
gazeti lake lingine la MAWIO kumshambulia Zitto. Inafahamika kuwa mashambulizi ya sasa ya Kubenea kwa Zitto yanatokana na kiu yake (SAED) kutaka kuchukua nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ana hofu Zitto ataitaka tena.

Lakini, wabunge hawawezi kuwa wajinga kumchagua mtu asiyejua kusoma Kiingereza kuwa Mwenyekiti wa PAC. Hivi, Kubenea atasomaje ripoti za CAG zilizo kwenye lugha ya Kiingereza? Atafanyaje uchambuzi wa ripoti za kitaalamu za masuala mengine ya ukaguzi? Atazungumza nini kwenye mikutano ya kimataifa ambayo Mwenyekiti wa PAC (Tanzania) ataalikwa?

Kubenea anatakiwa kwanza ajifunze KIINGEREZA kabla ya kutaka kuwania nafasi kubwa. Kama kuna mtu anabisha kuhusu hili, naomba leo aandae ripoti ya kurasa mbili ya Kiingereza na ampe Kubenea aisome hadharani ! Thubutu !

Kubenea na Lowassa

Kwenye kipindi cha miaka kumi iliyopita, hakuna mtu aliyemtukana na kumdhalilisha Edward Lowassa kuliko SAED KUBENEA na gazeti lake la MwanaHALISI.

Cha ajabu ni kwamba, Kubenea ndiye aliyekuwa mtetezi mkuu wa Lowassa baada ya mwanasiasa huyo kujiunga na Chadema akitokea CCM. Bila aibu, Kubenea alitangaza kwamba watu wenye ushahidi kuhusu ufisadi wa Lowassa wanatakiwa waende mahakamani.

Aibu iliyoje? Yaani leo Kubenea ni mtu wa kusema eti hakuna ushahidi dhidi ya Lowassa? Ina maana, kwa miaka minane iliyopita alikuwa anapiga porojo tu kupitia MwanaHALISI?

Kama huu si UPUMBAVU, tuuiteje?

Ninaamini kwamba dhambi hii ya Kubenea kwa Lowassa italipwa hapahapa duniani. Kuna kitu wazungu wanakiita KARMA. Kwa uovu na uonevu ambao huyu bwana kawafanyia watu hapa duniani, ipo siku naye atalipwa. Hapahapa duniani.

Kubenea na Dk. Slaa

Miaka michache iliyopita, Kubenea alikuwa mmoja wa watu walioweza kwenda nyumbani kwa Dk. Wilbrod Slaa na kuingia jikoni kuchukua chakula bila hata kuuliza. Mke wa Slaa, Josephine, alikuwa akimuona SAED kama mwanaye.

Slaa akafanya kosa la kuingilia maslahi ya Kubenea na kundi lake la akina Mbowe. Hiyo ni baada ya kukataa kumpokea Lowassa kama mgombea urais wa Chadema. Mara moja, akageuka kuwa adui wa Kubenea.

Hii leo, Slaa ni mmoja wa maadui wakubwa wa Kubenea. SAED amesahau wema wote ambao Slaa alimtendea kama binadamu. Anamshughulikia kana kwamba hawakuwahi kukaa mezani na kula. Kana kwamba hakuwahi kufaidi ukarimu wake.

Sasa Slaa atapigwa kila siku na MAWIO na MwanaHALISI hadi apotee kabisa kwenye siasa za Tanzania. Hiyo ndiyo kazi ambayo Kubenea amejipa hata kama kupotea kwa Slaa hakuna maslahi yoyote mapana kwa taifa.

Lakini, tangu lini Kubenea akajali maslahi ya Taifa na si yake binafsi?

Nasubiri kwa hamu siku ambayo Freeman Mbowe naye atageukwa na Kubenea. Huko nyuma, SAED ameonyesha uwezo mkubwa wa kuhama kambi na kusahau fadhila.

Inajulikana kwamba kimada wa Kubenea na mzazi mwenzake, Esther Daffa, ?amekatwa? kwenye kinyang?anyiro cha kutafuta Viti Maalumu kupitia CHADEMA. Hii si dalili nzuri kwa Mbowe na wenzake.

Mbowe afahamu kuwa Kubenea tayari amegombana na wote waliowahi kumsaidia huko nyuma. Hamad Rashid, Lipumba, Zitto, Mwakyembe, Membe, Nape, Sitta na wengine chungu nzima.

Ni suala la wakati tu kabla NDUMILAKUWILI huyu hajamgeukia Freeman Mbowe. Tusubiri tuone..

Seif Rashid ni mwandishi wa kujitegemea anayepatikana jijini Dar es Salaam

Mwisho

Huku ni kupoteza muda na energy. Ningemwelewa mwandishi wa makala haya badala ya kuandika angefanya usafi nyumbani kwake.
 
Mfumo wa ccm ni kulea Tabia mbovu kutetea Ujinga kupenda uchakachuaji slop nk , viongozi wengi wanapenda michepuko na hakuna Waziri wala katibu mkuu kiongozi anaweza kujitokeza hadharani akathubu kukemea Uvaaji wa hovyo hovyo unaokuwa Kwa kasi Nchini , Rais mseveni yeye kathubutu kupiga marufuku Uvaaji mlegezo kata K na vinguo vya hovyo hovyo , Hapa Tanzania Waziri wa Utamaduni anaogopa pia Magufuli hawezi kuthubutu Kwa sababu wanadai Wavaaji wa hovyo wote ni wapiga kura wao na wanawaandaa kuwa viongozi wa kesho. ! Hivi hapo unategemea maendeleo Tanzania ?
 
Msukule huu, ewe Mwenyezi Mungu mjaalie akili zaidi ya zile za kufahanu msalani tu. Huyu nyumbu akili zero kabisaa mweupeee kichwa anafungia nywele.

Ni mpuuzi kuliko wapuuzi wote walio jf, Mungu msaidie.

Ukishamaliza nenda Lumumba ukachukue buku saba yako. Unawafanyia kazi nzuri jitahidi wanaweza kukupandisha cheo.
 
Umewagusa Taco wenye mahaba na SK plus CDM. Ingawa sijafanya utafiti lakini mtiririko wa maelezo yako umejaa ukweli. Asante kwa kutuonyesha sura mbali mbali za Mr.Opportunist
 
Back
Top Bottom