Sadiki Awaamuru Wahanga wa Mafuriko: Yu hev tu GO!!

Hivi wapangaji hawasthili kupewa hivyo viwanja ambavyo serikali iliahidi kuwapatia waliopatwa na mafuriko? Binafsi nadhani nao wangepewa kipao mbele katika suala la kupatiwa viwanja ili wawe na makazi yao ya kudumu na sio kupanga.


mwaJ.
Na hapa hasa ndipo swali linapoingia. 50 years on baada ya UHURU Serekali iko wapi/inamipango gani juu ya NYUMBA kwa Wananchi wake??

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Mh. Meki Sadiki Amewaamuru Wananchi waliopewa hifadhi katika Shule za Jiji hilo na vitongoji vyake kuondoka haraka ili shule zirudi katika shuhuli zake za kawaida.
Kwa wale waliouliza waende wapi?
Mh. Sadiki alisema swali hilo ni Mchezo wa Redio, Kwani Serekali sio iliyosababisha Mvua kubwa na Mafuriko.

Nami naomba nimuongeze Mh. Sadiki Maswali mengine ili mchezo wetu wa Redio ulete maana.
Mh. Sadiki:
1. Hivi Serekali kazi yake nini? Au Ipo kwa madhumuni gani?
2. Nini wajibu wa Serekali kwa Mwananchi wakati wa kawaida?
3. Nini wajibu wa Serekali kwa Mwananchi wakati wa DHARURA?
4. Serekali ilishindwaje kuzuia ujenzi holela wakati ina Nguvu za Dola na Sheria?
5. Ndani ya miaka 50 ya UHURU kwa nini Serekali haijawa na Mpango/mikakati madhubuti juu
ya maswala ya NYUMBA kwa Wananchi wake?

Picha na Maelezo kwa Hisani ya Wavuti.com

Ni siku ya kila mtu kuuchukua mzigo wake aende! Wapi?


Wananchi waliokuwa wamesitiriwa katika kambi za muda kufuatia mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wameondoka katika kambi hizo leo ili kuruhusu shughuli kusudiwa za kijamii kuendelea katika maeneo hayo.
3994033.jpg


Wadau, nawasilisha.
Kauli hii angetoa Magufuli wangemwambia awaombe msamaha, nashangaa sana uzawa wa hao watu wa Dar, alafu ukiangalia hap Wazaramo wachache sana wanaojifanya wana uchungu na wananchi, haya sasa mwambieni Mkuu wenu awaombe msamaha wahanga wa mafuriko maana hata wao hawakutalka hali hiyo
 
Back
Top Bottom