Sadiki Awaamuru Wahanga wa Mafuriko: Yu hev tu GO!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sadiki Awaamuru Wahanga wa Mafuriko: Yu hev tu GO!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by alibaba, Jan 7, 2012.

 1. a

  alibaba Senior Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Mh. Meki Sadiki Amewaamuru Wananchi waliopewa hifadhi katika Shule za Jiji hilo na vitongoji vyake kuondoka haraka ili shule zirudi katika shuhuli zake za kawaida.
  Kwa wale waliouliza waende wapi?
  Mh. Sadiki alisema swali hilo ni Mchezo wa Redio, Kwani Serekali sio iliyosababisha Mvua kubwa na Mafuriko.

  Nami naomba nimuongeze Mh. Sadiki Maswali mengine ili mchezo wetu wa Redio ulete maana.
  Mh. Sadiki:
  1. Hivi Serekali kazi yake nini? Au Ipo kwa madhumuni gani?
  2. Nini wajibu wa Serekali kwa Mwananchi wakati wa kawaida?
  3. Nini wajibu wa Serekali kwa Mwananchi wakati wa DHARURA?
  4. Serekali ilishindwaje kuzuia ujenzi holela wakati ina Nguvu za Dola na Sheria?
  5. Ndani ya miaka 50 ya UHURU kwa nini Serekali haijawa na Mpango/mikakati madhubuti juu
  ya maswala ya NYUMBA kwa Wananchi wake?

  Picha na Maelezo kwa Hisani ya Wavuti.com

  Ni siku ya kila mtu kuuchukua mzigo wake aende! Wapi?


  Wananchi waliokuwa wamesitiriwa katika kambi za muda kufuatia mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wameondoka katika kambi hizo leo ili kuruhusu shughuli kusudiwa za kijamii kuendelea katika maeneo hayo.
  [​IMG]

  Wadau, nawasilisha.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nauliza tena, hivi wakigoma itakuwaje?
   
 3. M

  Makoko in UK Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alibaba
  Nimesikia hiyo lugha aliyotumia ni sawa na ile ya Magufuli, Hivi hawa viongozi wana matatizo gani?
  Ndio Siasa na Diplomasia za chuo cha wapi hizo?
  Yani wanashindwa hata lugha ya kiungwana na ustaarabu? Ati anaitwa Mheshimiwa! Ati na yeye ni kiongozi...............aibu...........!
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Serikali iliyo sahau wajibu wake ni hatari kama sumu!
   
 5. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo nyumba yako ikiungua, inabidi serikali ikuhifadhi?
   
 6. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si umeshasikia Kuwa wanajifunza katika semina elekezi jinsi ya kujibu,
  Hata mkuu wa kaya nae majibu yake ni kama hivi.
   
 7. M

  Moses msisia Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  acha wafukuzwe wao si walichagua ccm
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kazi kwelikweli
   
 9. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ndio watajua kama serekali ina mabomu na maji washa au haina
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  U people r nat serious,sasa mlitaka waendelee kukaa shuleni/madarasani mpaka ln?
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wawapeleke pale Kijitonyama kilipokuwa Chuo cha Simu (TTCL) kuna majengo yapo idle tangu 1996,kama kuna Chuo au jengo lolote lililokuwa/ambalo ni mali ya umma lilipo idle wapelekwe hapo nawasihi hawa waloweka nta maskioni mwao...
   
 12. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi wapangaji hawasthili kupewa hivyo viwanja ambavyo serikali iliahidi kuwapatia waliopatwa na mafuriko? Binafsi nadhani nao wangepewa kipao mbele katika suala la kupatiwa viwanja ili wawe na makazi yao ya kudumu na sio kupanga.
   
 13. a

  adoruta Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viongozi wa serikali mnaombwa mjipange pale mnapotoa kauli mbele ya raia. Kumetokea mkanganyiko pale ambapo Mh. Waziri mkuu aliposema kuwa waathirika wa mafuruko waliopanga mabondeni, watafikiriwa kwa ajiri ya kutafuta makazi mapya ya kupanga. Sintofahamu imekuja pale ambapo Mkuu wa mkoa wa DSM, aliposema kuwa wamepewa muda waondoke hawapewi chochote, na serikali imefanya usamalia wa kuwapa hifadhi wiki tatu tu! Je, hapo si ndugu zetu waathirika wanawekwa njia panda? Kumbuka kupanga au kupangisha nyumba au chumba ni suala la kisheria! Mpangaji na mpangishaji wote wana haki sawa kisheria. Tunaomba serikali izingatie sana jambo hili.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kauli za viongozi wetu siku hizi zina vichefuchefu!
   
 15. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwani tuna viongozi au marafiki wa JK wasiojua hata kiongozi anatakiwa afanye nini na aseme nini kwa watu anaowaongoza? huu uimla wanaoutumia utaendeleza migogoro na machafuko tu. Hatuna kiongozi kutoka Rais na wateule wake mpaka mjumbe wa nyumba kumi kupitia CCM
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,072
  Likes Received: 6,536
  Trophy Points: 280
  Nilimsikia hata mm jana. hivi huyo toz ni mtz kweli.
   
 17. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  umewasahau wazee wa FUNGUA FANTA UNYWE(FFU).
   
 18. M

  Mimi. JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 623
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  Huyu sadiki sio mtanzania naisi mtu mwenye huruma na akili timamu mwenye busara zake hawezi kuongea vile na wananchi tena mbele ya camera kwa kumlizisha kikwete huwezi kua na akili timamu ukawaambia watu waache chokochoko na serikali au kuwaambia kua serikali sio ilioleta mafuriko embu tyr to imagene jamani!? sasa kama nyinyi sio mlioleta mafuriko kwa nini mnawafata fata wananchi waacheni waendeleee kuishi mabondeni inawauusu nini sasa kuwaamisha kama mizoga huyu baba ni atakua ana mtindio wa ubongo
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Hujasikia Budget ya mabomu ya machozi na maji washa imeongezwa?:hatari:
   
 20. a

  alibaba Senior Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  mmbangifing,
  Yes we are....................We are demn Serious hatujasema waendelee kuishi katika hayo mashule.
  Serekali zinatakiwa ziwe na "CONTINGENCY PLAN" ie mipango ya kukabiliana na DHARURA zitokeapo. Viongozi wanapoteza kazi kwa kushindwa kuwa na mipango hiyo. Shule, Kumbi na Viwanja vya michezo viakuwa mahali pa mpito na serekali inatakiwa indelee kutoa huduma kwa muda utakaotajwa katika plani yake, na muda huo ulete maridhio kuwa kwa kiasi fulani serekali imejaribu kutekeleza wajibu wake.
  Tafadhali rejea hoja zangu huko juu:
  Serekali ina Wajibu gani kwa Wananchi wake??
   
Loading...