Saddam Hussein na Quran

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,795
Reaction score
48,057
Wakuu wengi wetu tunamfahamu saddam hussein lakini leo nawaletea kisa cha saddam na quran (uislamu)

Dikteta huyu aliwahi kuagiza iandikwe quran kwa damu yake

Yaani alijitoa damu ikawekwa kwenye chupa na kwenda sehemu maharumu ambapo maneno ya quran yaliandikwa upya bila wino bali kwa damu yake

Hii ilikuwa ni mwaka 1997 ,

Baada ya kutolewa madarakani, quran hii ilipatikana
Serikali ikashindwa ifanye nini juu ya quran ile

Kwa kuwa ni haramu kuandika quran kwa damu,kuna watu wakadai quran ile iteketezwe either kwa moto au kuchanwa lakini pia ni haramu kuteketeza quran
Hivyo basi quran hiyo iliachwa hivo hivo

Saddam pia hakuishia hapo, aliwahi kuagiza kuwa awekwe kwenye family tree ya mtume, na kweli aliwekwa na watu waliaminishwa kuwa saddam ni direct descendant wa mtume

Stori hii huwa haisemwi sana
Blood Quran - Wikipedia
 

Attachments

  • Screenshot_2018-08-26-19-30-37.jpg
    52.6 KB · Views: 67
Hapo ni maharumu au maalum.
Qur'an Kwa WAUMINI hairuhusiwi kuchanwa au kuchomwa moto kuna utaratibu wa kuihifadhi
Kuhusu kuwekwa kwenye tree hii inaendelea mpaka sasa lakini kulingana na uislamu ilivyo strictly huwa halisambai sana. Mara nyingi hawa hutokea Asia(masharikk ya kati) na wengi wakibainika hukimbilia Ulaya ila hili alisemwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sadam Hussein ni kweli ni uzao wa Ishamael ila kama unavyowajua waarabu hawa ni mbwa mwitu ni wakali sana na wana visasi sana kama watutsi. Ndio maana napinga Iraq kuwa na amani maana ikiwa na amani basi tegemea vita duniani vya kidini maana tutarudi kwa kina Saladin na Abu bakr. Waarabu wakitulia basi tena ujue ni bomu kubwa linatengenezwa maana kwa walivyofanyiwa na mzungu hivi basi tutarajie kisasi kikali kitarudi kwao(wazungu na sisi fuata upepo)

Sishangai sana maana ni waarabu ukiwaelewa utanielewa
 
Kumbe .nilidhani ni kamba tu
Ila kweli hawa jamaa siku wakitulia marekani na uingereza watapata tabu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kamwe waarabu hawatatulia maana hawapendani wenyewe kwa wenyewe. Ni wasaliti mwanzo mwisho na dhambi ya usaliti huwa ahiishi.
 
Mheshimiwa, Qur'an mchanganuo wake upo hivi,

Qur'an ina herufi 320,015
Qur'an ina maneno 77,439
Qur'an ina aya 6,236
Qur'an ina sura 114
Masahafu ambayo ya wastani ipo kati kwa kati kwa ukubwa( tambua ya kwamba nyengine herufi zake zimepunguzwa ukubwa kwa maana ukubwa wa maandishi umepunguzwa) huwa zinakaribia mpaka kurasa 600+

Napata ukakasi na ulichokiandika si vibaya ukatufafanulia zaidi. Alitumia damu yake kuandikwa Qur'an, litre ngapi za damu?
 
Hiyo story inaweza iwe "Myth" kwani alitoa damu kiasi gani ya kutosha kuandika msahafu wote....!!!
 
Mkuu, hakuna pahali popote aliposema alitumia lita ngapi
Ila ushahidi wa hiyo quran nimeweka hapo juu .
Ukiangalia utaona yeye mwenyewe anaikagua
Pia huko google kuna speech yake ambayo anafunguka sababu za kufanya hivo anadai kuwa Allah kamuokoa san kumwaga damu(majaribio ya kumuua)
Ndio maana akatoa damu yake kama shukrani kwa Allah
Ukitaka ushahidi zaidi zipo videos youtube zinazoonesha hili swala


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa ufafanuzi; kama alifanya hivyo, Mungu ndiye shahidi wa hilo.

Damu katika Uislam ni najisi. Ndiyo ipo mwilini mwako lakini ikishatoka ndani ya mwili wako inakuwa ni najisi. Ni sawasawa na kinyesi, kipo ndani ya miili yetu ila kikitoka nje kinakengeuka kinakuwa si sehemu salama ya sisi na najisi vilevile.

Ki' fiqhi damu inaingia katika najisi ya "Almutawassitwat" kwa maana ni najisi ya kati kwa kati, na kuna ahadith ya Mtume inasema " atakayesali pamoja na najisi haitoswihi sala yake" imma najisi iwe kwenye vazi, mahala unaposalia na kiwiliwili chako maadam hiyo imethibiti sala yako haitosihi.

Aisee! Sina cha kuendelea kujibu maarifa yangu ya dini ndiyo yameishia hapo. Ngoja nikawaulize wajuzi wanisaidie wanipatie na ushahidi kwa sababu suala uliloandika ni gumu(Qur'an kuandikwa kwa damu) na ugumu wake unakuja kwa sababu limejikita kwenye "Fiqhi" na fiqhi ni somo gumu si jepesi, ni sheria hiyo.
 
Sawa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…