VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,481
- 1,450
Kuondoka kwa wanajeshi hao, kunaweka kikomo kwenye mission ya SAMIDRC, iliyokuwa imeitikiwa na Tanzania, South Africa na Malawi. Baada ya kushindwa katika vita waliyokuwa wakipigana na M23, walisaini makubaliano ya kukarabati uwanja wa ndege wa Goma, ili utumike kuondoa wanajeshi na vifaa vyao. Hata hivyo, baadae, M23 iliituhumu SADC kuhusika na vitendo vya kutaka kuwapokonya mji wa Goma, na M23 ikaiomba SADC kuondoka mara moja.
Vifaa vyao na silaha zao, wariruhusiwa kuondoka navyo, ila silaha zilizokuwa za serikali ya DRC, zenyewe, na wanajeshi wa FARDC watabaki mikononi mwa M23. Pia, inasemekana SADC ilikuwa na madini mengi kambini, ambayo M23 ilisema yatabaki na kusaidia kukarabati miundo mbinu iliyohalibika wakati wa mapigano.
Taarifa zilizopo pia, zinasema huko waendako, kuna kundi la washilika lililopo kwenye mazoezi ya pamoja ya kijeshi.