Sadaka ya Elimu Tanzania (SAETA)

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Nashauri Watanzania kwa ujumla wetu, bila kujali kama mtu ana dini au hana, tuanzishe utoaji wa sadaka maalum kila siku au kila wiki ambayo inapendekzwa iitwe SADAKA YA ELIMU. Lengo liwe ni angalu kila mmoja wetu kutoa sadaka hii kwa angalau shilingi 500 kwa wiki. Iwapo tutafanikiwa katika hili kwa mwaka mmoja tu tutaweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 910. Fedha hizi zote chini ya Mfuko Maalum tutazielekeza katika kuboresha Elimu ya Msingi Mpaka chuo kikuu na pia kuanzisha Televisheni ya Elimu na Ujasiriamali hapa nchini ambayo itapendekzwa iwe na zaidi ya Channels 24. Pia tutawekeza katika ununuzi wa Matrekta ya kisasa kwa ajili ya kilimo na kuwakodisha wakulima katika sehemu mbalimbali hapa nchini.
 
Back
Top Bottom