GE2025 SACP Augustino Senga: Mkoa wa Songwe upo salama watu wakapige kura bila kuogopa

GE2025 SACP Augustino Senga: Mkoa wa Songwe upo salama watu wakapige kura bila kuogopa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amewahakikishia wananchi Mkoani humo kuwa Mkoa wa Songwe upo salama, wenye utulivu na amani

Akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi walioungana na majeshi mengine ya vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo baada ya matembezi ya pamoja yaliofanyika Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba Mkoani Songwe, na kuwaeleza maandalizi ya vyombo vya ulinzi na usalama yako vizuri na hakuna sababu ya wananchi kuwa na wasiwasi kabla, wakati na baada ya uchaguzi

Aidha, Kamanda Senga ameeleza kuwa tukio la uchaguzi si jambo jipya kwa taifa, kwani uchaguzi wa vyama vingi si wa kwanza upo tangu mwaka 1995, na katika kipindi chote hicho haijawahi kushuhudia matatizo makubwa yanayohatarisha amani, huku akiongeza kuwa kwa kuzingatia umoja, mshikamano na uelewa wa watanzania, anaamini uchaguzi wa mwaka huu pia utapita kwa amani kama ilivyokuwa vipindi vyote iliyopita

Kamanda Senga amewataka askari hao kuongeza umakini katika kipindi cha uchaguzi na kuhakikisha wanalinda usalama wa wananchi pamoja na mali zao, huku.akisisitiza umuhimu wa kila askari kutimiza haki yake ya kikatiba ya kupiga kura katika vituo watakavyopangiwa, akisema kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya wajibu wao kama raia wa Tanzania


 
Back
Top Bottom