Sabodo ataka mafisadi warejeshe pesa

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Festo Polea
MFANYABIASHARA maarufu wa jijini Dar es Salaam, Mustafa Sabodo, amesema kama viongozi wanaotuhumiwa kuhusika katika ufisadi wa namna yoyote nchini wanataka kusamehewa na Mungu na wananchi katika mwaka huu, lazima watoe fedha walizoibia nchi ili zielekezwe katika kusaidia wananchi.

Sabodo alitoa kauli hiyo jana ofisini kwake jijini Dar es salaam, wakati akitangaza kuchimba visima 1,000 katika wilaya zote nchini, isipokuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.


Katika hotuba yake, Sabodo aliitaka serikali isiingilie matumizi visima hivyo vyenye lengo la kuwasaidia wananchi kupata huduma za maji bila masharti.


Alisema ni jambo la ajabu kwa viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kuendelea kuhodhi fedha nyingi na kushindwa kuisaidia jamii inayowazunguka.

"Mimi ni tajiri na nina fedha nyingi kwa sasa na si fisadi, lakini nasaidia wananchi wa aina yote kwa kuwa naipenda Tanzania na watu wake. Kwa upande wao, mafisadi wanakumbatia fedha nyingi za kuiba lakini wagumu kuzitoa, halafu wanataka kusamehewa, hawatasamehewa kamwe," alisema Sabodo.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni muumini wa falsafa za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere, alisisitiza kuwa mwaka huu ni mwaka wa viongozi mafisadi kujisafisha kama wanahitaji kweli wanataka msamaha wa Mwenyezi Mungu na wananchi wa Tanzania.

"Mafisadi katika nchi hii ni kero, wana fedha nyingi, wameiba fedha na kuzificha halafu wanataka Mungu na Watanzania wawasamehe, hakika wakitaka kusamehewa watoe fedha walizoiba," alisisitiza
Kuhusu visima 1,000 atakavyovijenga katika wila zote nchini, Sabodo alisema kila kisima kitagharimu zaidi ya Sh5 milioni na ujenzi wake utakamilika Julai mwaka huu.

"Visima hivyo ninavyosaidia katika wilaya hizo sitapenda serikali iingilie kwa chochote kwa kuwa matengenezo madogo madogo yatafanywa na wananchi wenyewe. Hakuna yeyote atakayelipia katika kutumia visima hivyo," alisema.


Sabodo alisema visima hivyo vitachimbwa kulingana na mahitaji wa wananchi na wingi wao katika wilaya.


SOSI: MWANANCHI

WAZO LANGU:
JE YEYE SABODO SIYO FISADI MAANA UKIMNYOOSHEA MTU KIDOLE KIMOJA KUMBUKA VINNE VINAPOINT KWAKO
 
Afadhali yeye anaesaidiaa wananchi sio hao wanalimbikiza offshore account for ever.....
 
Mbona rostam anasaidia wananchi kupitia vodacom foundation ya vodacom?
 
Angekuwa fisadi asingejiamini kwa kuwa anajua watu wakiingia kwenye mafaili kiduchu tu unalo.
 
Wazalendo watano tuu kama Sabodo maeneo mengi Tanzania tungeweza kupata mahitaji muhimu, its a shame for a rich Tanzania to be this poor and primitive.
 
Visima 1,000 @ 5,000,000/=

Total: 5,000,000,000/= or TZS 5.0 Billions.

Hongera sana Sabodo. Wewe ni mfano wa kuigwa.

The only person kujitangaza kuwa yeye ni tajiri na ana fedha nyingi na si fisadi.
 
aliyechezesha Bahati nasibu ya Mwl J.K. Nyerere alikuwa nani mshindi tuliambiwa atapewa Scania lorry je fedha zote za tiketi ndio hizo tu? Fisadi ni fisadi tu ni sawa na aliyewapa wamasaai mitaji ya Saccos, kufungua vituo vya redio kila kanda, na Fisadi mbaya ni yule anayenunua viwanja katika kisiwa cha Dubai na kuwaacha wanaIgunga bila ya dawa, lami nk au wale wabunge wa Morogoro waliohamia Canada wakahamisha na pesa zetu.
km visima kweli 1000 vitachimbwa hapa TZ tunyamaze amalize kwanza, baniani mbaya kiatu chake .....
 
Mbona rostam anasaidia wananchi kupitia vodacom foundation ya vodacom?

Kamanda jambo usilolijua ni sawa na USIKU wa GIZA. Vodacom foundation bajeti yake inatoka VODAFONE na si VODACOM upo hapo. SO rostam hana msaada wowote kwenye Vodacom Foundation. Yeye ni Fisadi na atabaki kuwa fisadi Milele.
 
duu pesa nyingi sana huy saboda anazotaka kuzitumia kuchiimba visima kweli ameamua watu kama hawa niwakupewa pongezi
 
Afadhali yeye anaesaidiaa wananchi sio hao wanalimbikiza offshore account for ever.....


mkuu.... huyu babu ana asili ya kiasia lakini mimi naona huyu bwana ni mtanzania mzalendo...... walichakachua asili yake....... offshore bank accounts and offshore investments zipo nyingi sana ........ pale dohar kuna dozens of forbidden and hidden types of offshore investments
 
Mungu akuongezee mzee Sabodo.
Wewe Rostam utajiri ulio nao hata ungeishi miaka mia tatu wewe na faamilia yako na kutumia kila siku milion 1 huwezi kuumaliza!! sasa najiuliza unajilimbikizia mamilion yote hayo ya nini kama life expectancy yako haizidi hata miaka 80???
 
Back
Top Bottom