Sabaya ataachwa huru Februari 15, 2023

Sabaya ataachwa huru Februari 15, 2023

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,889
Reaction score
8,487
Hatimaye Rais Samia, ameguswa na maombi ya wana CCM na tarehe 15/2/2023 atamwachia rasmi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, kwani kusameheana kupo.

Kwenye mizani Sabaya na Mbowe wote ni wafungwa wa kisiasa na tuhuma za Mbowe ni nzito sana na ushahidi wake umetolewa na watu wakubwa ambao ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama lakini tuhuma za Sabaya ni nyepesi sana na ushahidi unatolewa na watu ambao tangu mwanzo wanajulikana wana chuki na Sabaya, Wengine wametamba waziwazi kwenye mabaa kuwa lazima wamkomeshe huyo kijana.

Mh rais haiwezekani ukubali kuingilia uhuru wa mahakama na kumsamehe mwana Chadema Mbowe alafu ukamuacha kijana na mtoto wako na mwana ccm mwenzako Sabaya akiteseka kwa tuhuma za uongo na uzushi alizotungiwa na wakwepa kodi na wauza madawa ya kulevya wa wilaya ya Hai.

Ni kweli chadema na wapinzani wengi wameshangilia sana kifungo cha Lengai Ole Sabaya cha miaka 30 jela lakini ukweli ambao hausemwi ni kwamba wana ccm wengi wamehuzunishwa na kuchukizwa mno na kifungo cha Sabaya.

Kwenye macho ya wazalendo wa nchi hii ,Sabaya ni mzalendo wa kweli aliyejitoa kuleta mabadiliko kwa vitendo na siyo maneno kama wanavyofanya wengi.

Bila Lengai Ole Sabaya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai haya yangeweza kutokea kwenye wilaya hii.

1. Wilaya ya Hai kupanda kwa ukusanyaji mapato kutoka ya mwisho hadi kuwa ya nne kitaifa. Kabla ya Sabaya wilaya hii ilikuwa imekithiri kwa rushwa na ukwepaji kodi.

2. Mbunge na madiwani wa ccm kushinda na kuongoza Halmashauri.
Wilaya hii ilikuwa ngome ya Chadema kwa miaka mingi na kila aliyejaribu alikiona cha mtema kuni kutoka kwa Mbowe na genge lake.

Lakini kupitia Sabaya sasa jimbo la Hai ni ngome ya ccm na itawachukua miaka mingi Chadema kulirudisha tena hasa baada ya Mbowe kuwa gaidi na kupoteza imani kwa wananchi wengi.

Lakini pia Mbowe ametangaza kuachana na siasa za majukwaani.
Kwa kifupi mbunge ,madiwani na wenyeviti mbalimbali wa wilaya ya Hai wanakula kupitia jasho la Sabaya.

3. Kurejeshwa kwa ardhi ya Waislamu iliyoporwa kwa miaka mingi.

Wilaya ya Hai wamepita wakuu wa wilaya wengi lakini hakuna aliyefanikiwa kumaliza mgogoro huo mpaka Lengai Ole Sabaya alipofika na kumaliza kadhia hiyo.
 
Nadhani sasa cha moto amekipata jeuri yoote kwishaa.

Akirudi sasa awe raia mwema tujenge taifa letu kwa umoja na upendo.

Ukipamba na Mbowe mwisho wako hauweze kuwa mzuri.
 
Sidhani kama atarudia tena ubazazi wake
Chuki za bure tu. Mumezoea vya kunyonga hadi mnaona ndio haki. Kesi zote alizozuliwa hata moja sio ya kweli ila wala vya kunyonga ndio wamemzulia.

Sina uhakika na taarifa hii, ila kama sabaya anatoka nina hakika wamangi mliochanga hela kuhonga mungu atawalipiza. Sabaya bila shaka amebaki mzalendo mtetezi wa haki na bila kua mtumwa wa sheria zinazosimamiwa na wauzaji na wanunuzi wa haki.
 
Nadhani sasa cha moto amekipata jeuri yoote kwishaa.

Akirudi sasa awe raia mwema tujenge taifa letu kwa umoja na upendo.

Ukipamba na Mbowe mwisho wako hauweze kuwa mzuri.
Kwa kua Mbowe ni gaidi.
 
Uzuri mmoja urais ni taasisi, hawezi kuja hapa JF na kuchukua bandiko lako hili la kipumbavu na kwenda kulifanyia kazi. Mkuu wa wilaya majukumu yake ni yapi kiasi kwamba ahakikishe hakuna mpinzani anarudi bungeni? Acha siasa za maji taka. Kwa bandiko hili huyu jambazi ataendelea kusota behind bar until further notice!
 
Kwamba ametangaza kwamba atamuachia kama nani? Subiri, tarehe 15/2/2023 sio mbali. Tutarudi hapa kwenye mrejesho. Yule msenge hatoki
Wewe ulikua na hisa kwenye mradi haramu upi? Hakuna hata mmoja wenu mwenye kisa cha kweli dhidii ya sabaya. Watu wabaya sana nyie. Sawa na wale wayahudi waliyopiga kelele yesu asulubiwe damu yake iwe juu yao wakati yesu hakua na kosa lolote ila kuwaambia waache dhambi.
 
Sabaya ana warembo wengi kumbe mtaani?

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Chuki za bure tu. Mumezoea vya kunyonga hadi mnaona ndio haki. Kesi zote alizozuliwa hata moja sio ya kweli ila wala vya kunyonga ndio wamemzulia.
Sina uhakika na taarifa hii, ila kama sabaya anatoka nina hakika wamangi mliochanga hela kuhonga mungu atawalipiza. Sabaya bila shaka amebaki mzalendo mtetezi wa haki na bila kua mtumwa wa sheria zinazosimamiwa na wauzaji na wanunuzi wa haki.
Leo nasikia Saa mbaya kachezea kichapo hatari.
Cheo ni dhamana.
 
Back
Top Bottom