Sabasaba special – mitandao jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabasaba special – mitandao jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jul 6, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  SABASABA SPECIAL – MITANDAO JAMII  Niko Ndani ya Viwanja vya JK Nyerere kwenye maonyesho ya Sabasaba kweli hali ni nzuri kampuni zilizoleta bidhaa zao kwenye maonyesho yaliyopita zimejitahidi kuboresha bidhaa zao na huduma zao zingine haswa kampuni za masuala ya mawasiliano kama SasaTel ambayo mwaka jana ndio ilikuwa inachipukia Leo nilivyofika nimeona tofauti .


  Kuna kampuni zingine ambazo mwaka jana zilikuwa na watu waliokata tamaa kwenye kujieleza kwa wateja naona sasa hivi hizi kampuni zimejitahidi kwa kiasi kikubwa pamoja na kuboresha huduma zao na kupunguza bei kwa baadhi ya bidhaa zao kama ZANTEL , ZAIN , TIGO ,VODACOM ,IWAY .


  Kampuni nyingi humu ndani ziko maeneo tofauti tofauti hata kama zinahusika na masuala yanayofanana mfano huduma za mawasiliano ya simu za mikono ningependa kuona kampuni zilizokwenye sekta inayofanana ziwe eneo moja
  Kabla sijaenda mbali na maoni yangu mengine hivi umewahi kujiuliza mtu aliyeko urusi au uchina anafuatiliaje maonyesho haya huko alipo na kwa mfano anataka kununua kitu kinachouzwa ndani ya uwanja awasiliane na nani ? Haya ni maonyesho makubwa ni kioo cha biashara na mambo yetu mbalimbali nchini lazima yaboreshwe kwa kutumia njia mbalimbali haswa za teknohama ili tuweze kufikia malengo  Ndani ya viwanja hivi kuna kampuni zaidi ya 5 za mawasiliano ya aina mbalimbali na vifaa vyake lakini kuna jambo nimeshindwa kiliona na hata kwa siku nyingi nimekuwa nalishangaa kwanini kwa mfano nilipoingia tu ndani ya viwanja nisipate ujumbe kwenye simu yangu ya kiganja kwamba sasa nimeingia viwanja vya sabasaba na kila ninapoenda labda kwenye banda namba 100 nipate ujumbe wa kunijulisha kilichomo ndani ? mpango huu ingefaa sana kwasababu watu wengi walio ndani ya viwanja hawana sehemu nyingine ya kutafuta na kupata bidhaa zao zingine kwenye eneo kama hili .


  Kwangu mimi hili ni suala muhimu sana ingawa inaweze kuonekana kama ni njia inayoweza kuingilia watu wengine uhuru wao wa kupata habari au aina nyingine ya taarifa naamini kukiwekwa taratibu nzuri kazi inaweza kufanyika na mamlaka ya viwanja hivyo pamoja na wafanyabiashara wataona faida zake siku za usoni  Ukiacha mambo ya Kupeleka Ujumbe mfupi kwenye simu za wanaoingia Kwenye viwanja wizara inayohusika na suala hili inabidi kubuni njia nzuri haswa zinazohusiana na mitandao jamii katika kutangaza na kuboresha maonyesho haya kwa siku zijazo na hatua hizi inabidi zianze angalau mwaka ujao mfano kungekuwa na tovuti maalumu kwa ajili ya viwanja hivi ambapo kampuni zote zinazoshiriki maonyesho haya zitatakiwa kuweka maolezo yao na walipo ndani ya viwanja hivyo kuna programu nyingi zinazoweza kutumika katika kufanikisha hili kama google earth tembelea www.earth.google.com kuna www.apps.google.com badala ya kubandika matangazo njiani ambayo yanaharibu mazingira yetu .


  Kama sasa unataka dunia ione vitu vingine zaidi kuhusu biashara na maonyesho kuna unaweza kufungua www.youtube.com ndani ya mtandao huu wizara husika kupitia tovuti yake inaweza kufungua channel ambayo itakuwa na video za maonyesho hayo ambapo watu wanaweza kutembelea popote walipo duniani – haya ni maonyesho makubwa nchini kwetu na ni vizuri yatangazwa kwa njia mbalimbali ambazo ni gharama nafuu au bure lakini inaweza kufikia maelfu kwa sekunde chache tu .


  Kwa kumalizia kuna haja ya viwanja hivi kuandaa mashindano kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambapo washindi wapewe nafasi kuleta bidhaa zao kwenye viwanja hivi bure na wawe na eneo lao maalumu na bila kusahau kuwa na vitengo vinavyohusu masuala ya teknohama inavyotumika hata watu waweze kujifunza mambo mbalimbali .


  Nawatakia maonyesho mema na tuzidi kuboresha bidhaa za ndani ili tuweze kuuza hata kwenye masoko mengine ya nchi jirani kama wao wanavyojaza bidhaa kwenye maonyesho yetu nasi tukajaze zetu kwao zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu .


  Yona F Maro
  0786 806028
   
Loading...