Sababu zinazotupa maumivu baada ya kutendwa

Sababu zinazotupa maumivu baada ya kutendwa

zema21

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
619
Reaction score
257
Wengi wetu wameshakumbana na maumivu makali na wana madonda nafsini mwao pamoja na majeraha yaliyosabishwa na mapenzi. Haya yote hutokea baada ya wewe kutendwa. Umeshawahi kujiuliza kwanini hutokea hayo?

1.Kuruhusu akili/ubongo wako utawaliwe na Huyo mpenzi wako.
Sikatai najua kuna kupenda na hutokea automatic, lakini unapokuwa katika mapenzi ni kosa kubwa sana kuruhusu ubongo wako kutawaliwa na mpenzi wako.

Mwisho wa siku unajikuta ukimuwaza yeye kwa sehemu kubwa na kumuona yeye ni kila kitu kwako. Wengine huwaona wapenzi wao ndio miungu yao hapa duniani. Hili ni kosa kubwa sana kumbuka yule ni mwanadamu mwenzako mwenye akili na mawazo ya kibinadamu. Muda wote anawaza akawaza vingine juu yako.

2.Kumuamini kulikopitiliza
Usimwamini mtu kwa asilimia mia kwani huwezi kuona au kufahamu akiwazacho.

3.Kutokujiandaa psychologically
Unapokuwa na mpenzi lazima uiandae saikolojia yako pia kwa kuwa inaweza kutokea mkaachana na mkiachana ni jambo la kawaida. Hivyo ikitokea haitokuumiza sana.

Ukiweza kuufundusha ubongo wako juu ya haya basi mapenzi hayatakutatiza sana. Zaidi na zaidi jifunze kumtegemea Muumba wako zaidi ya vyote.
 
Umenena vema mkuu ila mapenzi ya dhati hujengwa na ukua automatic bila muhusika kujua ni lini kiwango cha kupenda kimefika % kubwa hivyo.....Unajikuta kila saa unataka kuwa na umpendae unahisi kummis kila muda na ikiwa jinsi unavyohisi kumpenda mwenzko na yeye anahisi vivyo hivyo basi shaka ondoa na jiachie mikonon mwa mwenzako kwa utakuwa kwenye mikono salama sana...Maisha ya mwashaka na kutabiri mabaya ndani ya ndoa huwa si salama sana.
 
Hivi inawezekana kutomuwaza umpendaeeee.

Naendelea kujifunza kwani kwangu imekuwa ngumu ila kwa thread hizi naona kama niko shule hivi.

Asante mkuu kwa hili somo acha nifanyie mazoezi aisee maana mhhhh kuna wakati hadi mapigo ya moyo huenda mbio ili hali najua kazi ya moyo ni kusukuma damu na sio kupenda.

Nice therapy and will work onto it to make my life better.
 
yaaaani kama upo akilini mwangu sijawah kuumizwa na mapenzi coz huwa natumia hizo technic 😉
 
Mkuu naomb ushauri, mimi ninatatzo la kupenda kila ninayekutana nae, demu wangu kanipeleka kwao nimependa nyumba nzima, dada, wadogo zake, mama mpk housegirl na taratbu moyo unahamia kwa majiran, wote nawawaza mda wote na kuwaamini.
 
Back
Top Bottom