Sababu za watu kufa ghafla angali wanafanya mazoezi

Showio

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2019
Posts
254
Reaction score
482
MKURUGENZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof Mohamed Janabi, amesema sababu ya watu wanaofanya mazoezi kufariki ghafla ni pamoja na kutokupima afya zao kabla ya kufanya mazoezi ili kubaini aina ya mazoezi wanayotakiwa kufanya.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum, Prof Janabi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, alisema kwa kawaida mtu anaweza kuonekana hana tatizo lolote lakini kuna matatizo ambayo yanasubiri ufanye mazoezi kuliko uwezo wa moyo ndipo yaamke.

“Mazoezi ni kitu kizuri lakini asilimia kubwa ya watu wanafanya mazoezi bila kujua wanahitaji kufanya mazoezi ya aina gani, hii ni hatari ndiyo maana utakuta wengine wanapata matatzio ya ghafla.

“Shida ya moyo inatokea pale mtu anapokuwa na matundu moyoni, inasubiri siku utakapofanya kitu chenye nguvu zaidi kuliko uwezo wako, kuna watu moyo wao unamisuli mikubwa, hao ni kwamba njia inakuwa blocked na wengine wanakuwa na matundu kwenye moyo, watu kama hao wakifanya mazoezi magumu wanaweza wakapata madhara,”alisema Prof Janabi.

Aidha Prof Janabi aliwashauri watu wanapoenda kufanya mazoezi wapime kwanza afya zao ili waweze kuepukana na vifo vya ghafla.

“Ushauri wetu mkubwa kama madaktari kabla hujaenda kwenye gym, au kufanya mazoezi mengine makubwa kwanza upime afya yako kwasababu tunasikia wachezaji wanaanguka, wengine ni wanariadha awanaanguka wanafariki kwasababu hawajui wanatatizo gani.

“Mtu anaweza kupata tatizo la moyo au lingine, nakupa tu mfano timu yetu ya Taifa iliyokwenda AFCON (Kombe la Mataifa ya Afrika) walileta timu nzima ili kupima afya, wachezaji wawili walikutwa na matatizo makubwa kwahiyo wakaondolewa kwenye timu, hii imeweza kuokoa maisha yao maana unaweza kuanguka ghafla ukaambiwa eti umerushiwa jini mara, kafanyiwa hivi kumbe ni tatizo la moyo,”alifafanua Prof Janabi.

Licha ya kupima afya Prof Janabi aliwashauri watu kukutana na wataalam wa mazoezi ili waweze kuelezwa kuhusu aina ya mazoezi wanayotakiwa kufanya kulingana na afya au umri.

“Mazoezi wakati mwingine inategemea na umri, unaweza kuwa na miaka 70 halafu unaenda kukimbia mita 100, unajitafutia matatizo kwahiyo umri unategemea aina ya mazoezi, ni vyema ukapata mshauri akakwambia wewe kwa umri wako unatakiwa ufanye mazoezi ya aina hii,”alisema Prof Janabi
 
Ninachojua tu ni kwamba Wanaume wengi wanafanya Mazoezi siyo kwa Afya bali Kujazia tu Miili yao kama Mapipa ya SIMTANK ili Kutishia Watu hovyo, Kukaba, Kupora na pia Kuwavutia Wanawake ' Washamba ' ambao hudhani kuwa Mwanaume aliyejazia ndiyo anajua Mahaba au ana Pumzi kubwa ya Ufanyaji Mapenzi ( Ngono ) wakati kumbe wala si kweli.
 
Kuna uwezekano mkubwa ukawa na kitambi.
 
Mazoezi yameanishwa kabisa
1.kutembea
2.kukimbia taratibu
3.Aerobic
4.kuendesha baiskeli
Mazoezi haya yote yafanyike kwa mda wa dk 40 hadi 90mns.
Mengine huwa ni mbwe mbwe zaidi
Naomba source ya hii taarifa otherwise utakua umejitungia uongo wako kichwani.
 
Hapa huyu Bwana Janabi anatutahdhalisha watu wa mpira. Kuna wachezaji hawako salama kiafya. Je hao wachezaji wawili wa Taifa Stars waliokutwa na matatizo makubwa ya moyo ni kina nani? Je kwenye timu zao wanaendelea kucheza au wamesimamishwa kutokana na matatizo ya kiafya?
 
Naomba source ya hii taarifa otherwise utakua umejitungia uongo wako kichwani.
Maisha ya Africa yenyewe ni mazoezi tosha....lishe yetu niya hovyo kukuta mtu anaye kula kilo moja ya nyama kwa siku au lita 56 zamaziwa kwa mwaka as recomedation ya FAO ni nadra sana tunapata vitabi kwa sababu ya umuri mulnutration kwashako na hari ya hewa, so in short idont go for gym
 
Janabi leo amekuwa mtaalamu wa sports medicine....last time alikuwa urologist....akiwashauri wagonjwa wenye BPH wavalishwe pampers hahaha...baadae Nutritionist...watu wasile wanga..
Hakika ni professor wa aina yake
 
Ninachojua tu ni kwamba Wanaume wengi wanafanya Mazoezi siyo kwa Afya bali Kujazia tu Miili yao kama Mapipa ya SIMTANK ili Kutishia Watu hovyo, Kukaba, Kupora na pia Kuwavutia Wanawake ' Washamba ' ambao hudhani kuwa Mwanaume aliyejazia ndiyo anajua Mahaba au ana Pumzi kubwa ya Ufanyaji Mapenzi ( Ngono ) wakati kumbe wala si kweli.
wapga gym mtuache..
 
Back
Top Bottom