Kyakya
JF-Expert Member
- Apr 24, 2009
- 398
- 23
Huwa nina sikitika sana ninapokuta watu, wabantu kabisa wa Tandika, Gairo, Mlalakuwa na sehemu nyingi nyingine za Tanzania wakijiita mara mimi Arsenal, yule Liverpool, mara ManU zaidi, tena unakuta wanafikia hatua ya kutaka kupigana.
Tatizo kubwa nadhani TFF wanachangia kwa kutozirusha mechi zetu zote za league hapa Tanzania, kwa kuhofia eti mapato yatakuwa madogo. Unajua mtu aliyezoea kwenda mpirani ata ukionyesha kwenye Luninga na tena umpe hela asiende uwanjani, ataenda tu.
Nashauri Msimu ujao watuonyeshe mechi sio lazima zote ata zile zinazousisha timu kama Simba, Yanga, Mtibwa na nyingine ambazo ni kubwa kwa mtazamo wetu na sehemu mbali mbali zitokazo. Tuwazoeshe watu wetu mpira wetu namna unavyocheza, naamini wanacheza vizuri sana, asa tukiwa na kamera pande zote za uwanja tutawaona vizuri tu. Unajua uduni wa vifaa uwanjani unaweza kukufanya uamini soka linalochezwa ni baya, alikadhalika ubora ukakufanya udhani soka linalochezwa ni safi.
Tuache kulea Ukoloni Mamboleo huo.