Sababu za kutorejesha fomu kwa Mawaziri

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,206
18,548
Kwanza ni kwamba mawaziri wote 4 na naibu waziri wamezirudisha fomu jana kabla ya saa 10 jioni.
Na kila mmoja alikua na sababu zake.

1. Makamba: Anasema huwa anamtumia mwanasheria wake kuzipeleka fomu zake kila anapo jaza lakini kwa wakati huu mwanasheria wake alikua na udhuru wa muda mrefu na aliye mtuma hakufanya hivyo.

Makamba amezipeleka fomu zote jana kwa kutumia mwakilishi wake kabla ya saa 10 jioni.

2. Dr Mahiga: Anasema yeye alibanwa na majukumu hasa safari za nje hivyo kushindwa kupata muda wa kuzipeleka fomu hizo tume japo amekiri kuwa agizo la Rais limetoa somo zuri kuhakikisha kila jambo linafanyika kwa wakati.

3. Kitwanga: Yeye anasema fomu zake alizipeleka toka tarehe 4 january na ameshangaa kwamba anatajwa japo jana baada ya tume ya maadili kuzitafuta zilipatikana.

4. Mpina: Yeye anasema ameshindwa kupeleka fomu kutokana na kuto jua mshahara wake.
Amekiri kuwa inaonyesha Rais pamoja na kujua sababu aliyo kuwa nayo bado alimpa masaa 12 kupeleka hizo fomu kiashiria kwamba sababu zake Rais hakuzikubali.
Jana hiyohiyo alimwita mhasibu na kujua mshahara wake na fomu akazirudisha.

5. Dr ndarichako sababu zake hazija patikana japo naye jana hiyohiyo alitima mwakilishi kuzirudisha fomu zote tume ya maadili.

Hapa kazi tuu..
 
Daaah hizo sababu si bora wangesema walijisahau tu(Ukitoa waziri wa mambo ya nje), ila huyu makamba ndo sijamwelewa,
  • mwenye mali ni yeye mwanasheria anahusikaje?
  • kwanini achukue tahadhari ya kisheria kama anajua anasema ukweli?
 
Eti nilikuwa sina nafasi kwa sababu ya kutumwa na rais, halafu huyu jamaa ndio msomi eti mwana diplomasia, halafu kiongozi mkubwa wa nchi, ni zaidi ya aibu, rais amefanya makosa kumpa kazi? Hii ni dhihaka kwa rais, ni sawa na msichana wa kazi asiangalie mtoto mpaka apotee aseme mwenye nyumba alimwambia apike chakula, huyo wa mshahara ndio janga nae, alichofanya mapaka akapeleka bila kumuuliza rais mshahara wake why hakufanya hicho kabla? Hawa walitakiwa wakae pembeni tu, mbona wengine wana tumbuliwa? Mwana sheria, ndio amekosea so January na e anatafuta wa kumlaumu, nchi ya maajabu.
 
Huyo luhaga mpina hajui mshahara wake? Haya ni matusi makubwa,hapati pay in slip?,haendi benki? Au mihela imejazana kiasi mshahara ukiingia haoni
 
Kulikuwa na sababu gani Waziri Mkuu kubwatuka hadharani katika suala ambalo serikali ingeweza kulimaliza kirahisi kwa mazungumzo ya ndani?
 
Daaah hizo sababu si bora wangesema walijisahau tu(Ukitoa waziri wa mambo ya nje), ila huyu makamba ndo sijamwelewa,
  • mwenye mali ni yeye mwanasheria anahusikaje?
  • kwanini achukue tahadhari ya kisheria kama anajua anasema ukweli?
Mkuu, hapo kwenye bold hata mi nimejiuliza sana; halafu pia kateuliwa uwaziri nadhani ana miezi 2 na anajua kua hajajaza form kwasababu mwanasheria wake hayupo, sasa muda wote huo hakua na alternative nyingine.
 
Kulikuwa na haja gani kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mawaziri wanne hawajarudisha form?Hilo ni suala lao la ndani na haiwahusu sana wananchi.Tunavyovitaka hawatuwekei wazi kama mikataba na tusivyovihitaji sana ndivyo wanatuletea.Waitangaze ns mikataba.
 
Wanataka kuonyeaha eti wanafuata sheria.Wakati wateuliwa wote ni wale wale waliokuwa raslimali zetu halafu eti tnapasua majipu.Sidanganyiki kamwe
 
Luhaga Mpina anasemaje? Hakujali kuwasilisha fomu kwa sababu hakuwa anajua analipwa mshahara kiasi gani? Huyu ni kupe, kuna mahali ananyonya damu bila gharama. Ina maana asingeshtuliwa na Majaliwa angeendelea kupiga kazi huku hajui mshahara wake? Huu ni mzigo mpya jamani .....
 
Kwanza ni kwamba mawaziri wote 4 na naibu waziri wamezirudisha fomu jana kabla ya saa 10 jioni.
Na kila mmoja alikua na sababu zake.

1. Makamba: Anasema huwa anamtumia mwanasheria wake kuzipeleka fomu zake kila anapo jaza lakini kwa wakati huu mwanasheria wake alikua na udhuru wa muda mrefu na aliye mtuma hakufanya hivyo.

Makamba amezipeleka fomu zote jana kwa kutumia mwakilishi wake kabla ya saa 10 jioni.

2. Dr Mahiga: Anasema yeye alibanwa na majukumu hasa safari za nje hivyo kushindwa kupata muda wa kuzipeleka fomu hizo tume japo amekiri kuwa agizo la Rais limetoa somo zuri kuhakikisha kila jambo linafanyika kwa wakati.

3. Kitwanga: Yeye anasema fomu zake alizipeleka toka tarehe 4 january na ameshangaa kwamba anatajwa japo jana baada ya tume ya maadili kuzitafuta zilipatikana.

4. Mpina: Yeye anasema ameshindwa kupeleka fomu kutokana na kuto jua mshahara wake.
Amekiri kuwa inaonyesha Rais pamoja na kujua sababu aliyo kuwa nayo bado alimpa masaa 12 kupeleka hizo fomu kiashiria kwamba sababu zake Rais hakuzikubali.
Jana hiyohiyo alimwita mhasibu na kujua mshahara wake na fomu akazirudisha.

5. Dr ndarichako sababu zake hazija patikana japo naye jana hiyohiyo alitima mwakilishi kuzirudisha fomu zote tume ya maadili.

Hapa kazi tuu..
hivi mkulu mwenyewe ameshajaza hizo fomu? na kama karudisha je!akitoka atatujulisha au yatakua kama ya watangulizi wake?
 
TUTAJUAJE KWAMBA WANACHAPA KAZI NA WAKO SERIOUS
Kama mnataka wachapa kazi na walio serious msingechagua serikali inayoongozwa na watu ambao hata mawasiliano ya msingi tu yanawashinda.

Mtu kawasilisha fomu, Majaliwa kamsema kwamba hajawasilisha.

Sasa hili dogo tu Waziri Mkuu anachanganya, makubwa mangapi ambayo hatuyajui kashachanganya?

Is your Prime Minister serious?

Kashamuomba radhi huyo waziri?
 
Back
Top Bottom