Reagan Carima
Member
- May 20, 2015
- 44
- 194
Nimepata wasaha wa kuingia kwenye tasnia ya biashara na kwakuwa mimi ni kijana bado basi nimetumia muda wangu kufanya tafiti mbalimbali juu ya biashara.
Leo nataka kuzungumzia suala la biashara kufeli.
Watu wengi wamekuwa na ndoto ya kumiliki biashara lakini kwa namna moja au nyingine wanashindwa kufikia malengo yao kutokana na vikwazo mbalimbali ambavyo wanakutana navyo.
Sababu kuu zinazowafanya watu kushindwa kutimiza ndoto hiyo ni pamoja na:-
1- Kutojua historia ya biashara husika
Hapa namaanisha kuna wale wanaoanzisha biashara either kwakuwa ameona fulani alifanya akafanikiwa au kwakuwa sasa nina pesa ngoja niweke kwenye biashara
2- Kukosa management
Asikudanganye mtu yeyote biashara yoyote ile kama haina management nzuri basi tegemea kuanguka na kufa au kugaragara kwa muda mrefu bila mafanikio. Hii ni kutokana na kuwa wewe unaanzisha biashara ukiwa na malengo fulani kisha unampa mtu mwenye malengo tofauti na yakwako aisimamie. Ni ngumu sana
3- Kutaka faida kwa haraka
Watu wamekuwa wakiweka matarajio yao kwenye kupata faida kubwa tena kwa haraka. Hii kwenye biashara ni mbaya sana, ila amini nakwambia wapo watu wamefanya biashara miaka mitano bila kuchukua chochote kama faida na mida wote wamekuwa wakitengeneza tu hivyo kwa wageni hapo wanafeli
4- Kutokuwa na uzoefu
Biashara ni kama mchezo ni lazima angalau uwe na uzoefu kidogo ili uweze kukabiliana na changamoto za humo ndani. Mfano ikiwa mtu anaanzisha biashara ya kuuza maziwa ni lazima awe na uzoefu namna ya kuyatunza na mazingira yakuishi nayo.
Mtu mzoefu atajua kuwa ili niuze maziwa fresh lazima pia nijuane na wanaouza maziwa ya mtindi au namna ya kusindika ili pale maziwa yanapokuwa yanafikia kipindi cha kukaribia kuharibika basi ayasindike au ayatume kwa mwenzake ambaye ni mhusika.
Mfani mimi nina rafiki zangu wameingia kwenye kilimo kwa sababu ya kuelimishwa ila wameshindwa.
Wanashindwa kwakuwa hawana uzoefu. Hawajui namna ya kuendesha kilimo ila katika darasa walielewa na wakaziona pesa kibao mbeleni.
Nitaendelea wakati mwingine ikiwa mada hii itakuwa na mashiko