Kessy Wa Kilimanjaro
JF-Expert Member
- Jan 23, 2016
- 327
- 208
Tangia mwaka 1990, Tanzania imepewa zaidi ya billioni $32.8 kama msaada kutoka nchi za nje. Ungefikiri kwamba na hela hii tusingekuwa na Tatizo la upungufu wa barabara, umeme, maji au hospitali. Lakini nyie mnaoishi Tanzania niambieni; Je, maendeleo kutokana ni hii hela ya msaada imewafikia?
Na chakusikitisha zaidi ni kwamba wote tunajua hii hela inaenda wapi wakati wanao ikusanya huko marekani wanatumia picha za watoto wanao kufa na njaa ili kuwasikitisha watu na kuwadanganya akati zinapofikia ni kwa wanasiasa wenye vitambi.
mada yangu inahusu hii misaada na jinsi inavyowawezesha maraisi wa kiafrika na vyama tawala kuto kuona uhalifu wa sera zao za kiuchumi.
Nchi isinge kuwa na misaada ya nje maraisi wangejua kwamba wakifeli kujenga uchumi hawawezi kuongeza tu matumizi kwasababu kusingekuwa na hela ya kufanya hivyo. Wangelazimika kuacha njia zao za kikomunist na wangelazimika kuacha ujamaa na kurahisisha uwekezaji na uhuru wa soko, sivyo nchi ingekufa njaa.
Lakini kwasababu kuna misahada ya kutumia kila pale ambapo raisi akishindwa kujenga uchumi, Raisi halazimiki kujenga uchumi wake mwenyewe bali kutegemea hiyo misahada. Na hela ya misaada inaenda kuimarisha nguvu ya Raisi tawala na chama chake kama ilivyotokea Ethiopia alivyofanya Mengistu. Vibaya zaidi viongozi kama mbutu wanatajiribu kwa mabilioni na hela zao wanaziweka swiss banks.
Alafu ukiona nchi zilizoendelea hazijajengwa na misaada bali na uhuru wa uchumi na urahisi wa uwekezaji. Ni mtu ambaye mpumbaavuu ndiyo anaamini kwamba misaada ya nje itaijenga nchi yake.