Hakuna kosa kubwa kama kuwaandaa watu kupambana na polisi.Matangazo ya viongozi wengi wa chadema yalionesha kuwa kutakuwa na mapambano siku ya uchaguzi.
Jambo hili limewaogopesha watu wengi sana kwenda kupiga kura.Wengi wana kumbu kumbu mbaya na majeruhi,mateso na hadi vifo vinavyotokea kutokana na vurugu za kisiasa.Kwa vijana ambapo wanaweza kuwa walengwa zaidi kwa kuhisiwa wanaenda kupigia kura upinzani,wengi wamesita wakiamini tu mgombea wao atashinda tu kwa vile anapendwa.
Pia ccm iliwekeza kwa akina mama ambao walipita nyumba kwa nyumba hadi usiku kuomba kura.Na hawakuanzia hapo tu,bali walianzia katika kuhamasishana kwenda kuhakiki taarifa zao.Ukweli ni kwamba wengi ambao hawakuhakiki,majina yao hayakuchapwa ingawa yapo kwenye data base.
Mwisho nawashauri mbadili approach.Nendeni tu mkihamasisha watu wawapigie kura na msihamasishe kabisa vurugu.Shusheni viburi,na mu mwamini Mungu na kumtegemea yeye tu.Kama ukuta wa Yeriko ulianguka bila matumizi ya nguvu,ccm ni nini iwapo Mungu atakuwa upande wenu?
Vinginevyo tukiri kuwa Mungu amewapa kibali ccm ndio maana wamefanikiwa katika kila walilolifanya,liwe zuri ama baya.
Kwa Zanzibar kuna mambo ya kutisha.Lakini Mungu atalipa kwa wakati wake.Damu ya mtu huwa haimwagiki bure.