Sababu ya baadhi ya watu kuwa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu ya baadhi ya watu kuwa mafisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkisumuno, Sep 20, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Utafiti niliofanya kama mtaalamu wa saikolojia nimebaini sababu kadhaa za watu kuwa mafisadi au kujilimbikizia mali, mojawapo ya sababu kuu ni KUTOJIAMINI (low self-esteem).
  Mtu asiyejiamini pia yeye huwa hajitambui kama yeye ni nani, hivyo hujaa uoga na kuwa na wasiwasi. Ili aweze kusimama mbele za watu na kusema jambo akaeleweka anahitji vitu kadhaa ili kujenga kujiamini.

  Baadhi ya vitu hivyo ni kuwa na mali nyingi, Kuvaa nguo za gharama zaidi ili kuwafanya wengine wawe na attention kwake, Kunywa pombe na hata madawa ya kulevya.

  Kwa hiyo mafisadi wengi wenye utajiri usiosemeka leo wamefika hapo kwa vile wao hajitambui, hawajui wanishi katika nchi ya namna gani. Wanafikiri ili wapate vyeo zaidi lazima wawe na pesa na mali nyingi na mara nyingi hujipendekeza kwa baadhi ya makundi ya watu wenye ushawishi kama mashirika ya dini kama ngao yao ya kuwalinda.

  Tofauti na watu wanaojiamini, wao huamini wanakipaji mali kwao ni kitu cha ziada sana cha muhimu kwao ni kutumia vipawa vyao kwa ajili ya watu. Mifano michache ya watu wanaojiamini ni mzee Mandela licha ya kukaa gerezani kwa muda mrefu lakini aliachia madaraka kwa kipindi kifupi sana baada ya kuwa Rais wa Afrika kusini, kwa vile tu alijua alichokuwa akipigania utu na usawa wa mwafrika umepatikana. Rais Mgabe ni miongoni mwa watu wasiojiamini ndiyo maana anasema hayuko tayari kuacha madaraka kwa vile alipigania uhuru. Sifa nyingine ya mtu asiyejiamini ni kutowaamini wenzake kama yeye ni kiongozi atataka kila kazi afanye yeye.

  Mfano mwingine wa Mtu anayejiamini ni Hayati Kambarge Nyerere, licha ya kuwa madarakani muda mrefu hakujitajirisha kwake cha muhimu ilikuwa ukombozi na maendeleo ya watanzania na si familia yake. Mtu asiyejiamini anakuwa na tatizo la kuiga vitu vingi kwa watu wengine pasipokupembua madhara yak. Vijana na viongozi wengi hawajiamini ndo maana wanaiga mambo mengi ya magharibi kwa vile tu wanafikiri kila kitu wafanyacho wazungu ni kizuri.

  Nikipata muda nitatoa maada jinsi ya kumlea mtoto wako aweze kujiamini kisha tuwe na watoto wanaojiamini na kupunguza matatizo katika Taifa letu
   
 2. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280
  You could be right to some extent, ila siamini moja kwa moja kuwa hawa watu wanaiba kutokana na kutojiamini. Kwa mtazamo wangu, I think most mafisadi wanaiba kutokana na ubinafsi wao pamoja na loopholes zilizopo kwenye madaraka yao. Ubinafsi: viongozi wengi hujilimbikia mali za umma na kujijali wao pamoja na ndugu zao na kujiona kuwa wako entitled kuiba mali za umma. Loopholes: wengi huiba kutokana na loopholes zilizopo madarakani based on bad governance / administration. Kama hakuna ufuatiliaji, utaacha kuiba na kumtunza changuduo ama nyumba ndogo yako?
   
 3. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  i salute you bro Nkisumuno
  mada yako ni nzuri sana na ninaingojea hiyo nyingine kwa hamu sana kwani sababu kubwa ya mimi kuwa mnwana jamii ni kutaka kujielimisha zaidi na zaidi through this interaction.
  Mimi siyo mtaalam wa sosholojia lakini jee hudha kama jamii inachangia nayo. mfano mzuri ni wangu mimi mwenyewe kwani nilimlea mdogo wangu hadi high school halafu akaajiriwa idara nyeti tu ya serikali. lakini baada ya miaka 5 tuu ingawa mimi mshahara wangu kwake ni mara 2 lakini aliweza jenga nyumba 2 akakarabati ya mzee nyumbani na hivi sasa ana nyumba 4 wake 2 na magari 3. Nyumbani ninaonekana mimi kuwa ni mjinga kabisa na wala sifai [ninategemea mshahara] lakini bw mdogo ndiye sasa anayeonekana wa maana . sasa unadhani wadogo zangu watafuata nyayo za nani?
  mimi mwenye kajumba alichoniuzia mkapa ambacho hadi leo bado ninachechemea kulipa and huyo bwana mdogo???
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  wamekulia kwenye umasikini ulio topea
   
 5. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli, lakini ulichokifanya wewe ni kizuri zaidi, wewe ni mtu unayejiamini unachopaswa ni kuangalia ulichofanya bila wewe huyo mdogo wako asingefika hapo. Naomba zidisha kujiamini atakayekudharau hajui anachokifanya. Nyerere alishangazwa na wale walioamua kumjengea nyumba wakati yeye alikuwa anaona inamfaa. Ok mdogo wako kaoa wake wawili unafikiri hilo ni jambo muhimu sana. Kuhusu mipango yako ifanye si kwa pressure ya mtu utakujafanikiwa zaidi hapa duniani na baadaye hata anayekudharau atakuja jua wewe ni mtu mhimu sana.
   
 6. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli ila kwa vile watanzania wengi tunashughulikia matatizo baadala ya chanzo cha matatizo, Hizo loopeholes zinatokana na kiongozi wa juu akiwa hajiamini hawezi kukemea maasi kwanza yeye mwenyewe yuko hivyo hajitambui baadaye nfumo mzima na mifumo hujengwa mtu akiwa mdogo na ndiyo maana huko nyuma Tanzania tulikuwa tunaheshimiana, leo mwizi anaonekana mjanja mwenye kufuata haki anaonekana mjinga.
   
 7. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280
  nkisumuno, right on the point. Swali, je sisi watanzania hatujiamini na ndiyo maana tunamwachia mkuu wetu azidi kutukandamiza au vipi? Binafsi, sioni faida ya huyu mkuu kuwa kiongozi for he is incompetent na ni mwizi. Sasa anaiba because hajiamini au ni kwa sababu ana madaraka? Ahsante kwa kutujulisha na mafunzo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...