Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Hiyo ndiyo sababu ya kuona kwamba ligi kuu bora Duniani ni english premium, bidhaa bora Duniani ya ktk Uingereza, Elimu bora Duniani ni ya Uingereza, hakuna gari nzuri kama Range Rover, kiatu kizuri ni clarks cha Uingereza, suti bora Duniani ni ya Uingereza, Sheria bora Duniani ni common law sasa hivi vyote ni vya kawaida tu na havina upekee wowote ule Duniani ila kwa sababu mko kwenye kitu kinachoitwa ,,British sphere of influence" ndiyo maana mnaona hivyo!
Ukimuuliza Mwafrika wa Senegal atakwambia Elimu bora ni ya Paris École polytechnique, ligi bora Duniani atakwambia ni Ligue 1, gari nzuri na bora atakwambia citroen, ukimuuliza mfumo wa sheria bora Duniani atakwambia ni droit privé na droit public, ukimuuliza Mji mzuri Duniani atakwambia Paris, na sababu kubwa kama vile walivyo Waafrika mali ya Mwingereza ni kwamba Msenegal yuko kwenye ,,french Sphere of Influence" na hivyo chcochote kile french ndiyo bora Duaniani!
Ukienda kwa Muangola na Msumbiji ambaye yuko kwenye ,,Portugues sphere of influence" ukimuuliza ligi bora Duniani atakwambia Copa do Brasil, ukimuuliza mji mzuri Duniani atakwambia Rio au lisbon, ukimuuliza wanawake wazuri Duniani atakwambia wako Brazili, ukimuuliza mfumo wa sheria mzuri Duniani atakwambia súmula vinculante na yote hii ni kwa sababu yuko kwenye portuguese sphere of influence ndiyo maana haoni chochote nje ya huwo mfumo!

Hicho ndicho nilichokiona kwa sisi Waafrika!