hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 3,247
- 6,769
Nafikiri ni wengi miongoni mwetu tumeshawahi kujiuliza hili swali, kwamba ikiwa mbu ana uwezo wa kuambukiza malaria kwa kukupa mate yenye vijidudu vya malaria pindi anapokung'ata, je itawezekana kuambukiza virusi vya ukimwi kwa kumng'ata muathirika na baadaye kumng'ata asiye mwathirika.
jibu ni hapana, mbu hawezi kuambukiza virusi vya ukimwi kutoka mtu mmoja(muathirika) kwenda kwa mwingine(asiyeathirika) kwa kumng'ata.
sababu zake ni kama ifuatavyo;
1.Njia anayotumia mbu kunyonya damu;
-mbu utumia sindano yake katika kung'ata mtu,sindano hii ina visindano/midomo midogo ipatayo sita minne kati yake huitumia kwa kupekechea ngozi ya amng'ataye na miwili iliyobaki; mmoja hutumika kufyonza damu na mmoja kuingiza mate kwa amng'ataye na kamwe mirija hii haina uhusiano wa moja kwa moja.
hivyo mbu anapomng'ata mtu umpa mate na kufyonza damu na kamwe hampi mtu damu.
2.kumeng'enywa kwa virusi ndani ya tumbo la mbu kunakopelekea kufa.
3.kiasi kidogo cha virusi vinavyopatikana kwenye damu ya muathirika.