motonkafu
JF-Expert Member
- Dec 2, 2015
- 1,019
- 705
Sasa pamezuka ubishi.. Paleee kijiweni kwetu tunapokunywa kahawa. Watu wamebishana weee mi nkaomba breki nkaja kuandika huu uzi.
Akaongea mdogo wake fataki bwana ' mnajua kuwafukuza shule watoto wanaopata mimba ni hasara?' Nkamuuliza 'hasara ya nani?' Kanijibu bwana 'hasara ya jamii na taifa kwa ujumla ukiacha wazazi wa msichana' Nkasema 'haaaa ko unataka tuwaache wazalie shuleni?'
Akasema 'hapana braza' mi aniita braza si ni mkubwa kwake! Akaendelea 'ebu fikiria kila shule inafukuza wasichana wangapi kwa mwaka?? Nkamwambia sijui mi sio mwalimu, akasema 'pengine tufanye wasichana wawili kwa mwaka kwa wastani wanaweza kuzidi apo' enheee ' tuna shule ngapi katika kila mkoa?' Sijui pengine mia moja mia mbili. 'Fanya mia hamsini wastani zaweza zidi hapo' enheee 'tuna mikoa mingapi Tanzania?' Nkasema sijui labda tumuulize mkuu wa mkoa. Akasema 'iko ishirini na sita' weeeeee 'sasa unajua mikoa yote inafukuza wasichana wangapi kwa mwaka kwa wasitani?' Sijui ' fanya hesabu shule moja inafukuza wasichana wawili mara kwenye mkoa ziko mia hamsini mara mikoa ishirini na sita jibu ni ngapi?' Sijui akasema 'yalaaa ulirushwa darasa ebu leta kalukuleta; 2 mara 150 mara 26 jibu ni... ' sijui 'alufu saba mia naneee, kwa mwaka twafukukuza wasichana elufu saba mia nane kwa wastani waweza zidi hapo...jee kwa miaka kumi ????'
Nikamuuliza ' Fataki unaongea yote hayo au kwa sababu ukoo wenu mnapenda watoto wa shule, kumbuka kuna fimbo 30 za jela!!!!!'
Akasema 'kaka si hivyo tu kuna sababu nyingine lukuki..!' Enheeee ' kwanza kuwafukuza shule ni kuwanyima wasichana haki ya kusoma' nkamuliza weweee kwani hawarudi? Akajibu Warudi wapi wakifukuzwa ndo kwa heri. Enheee tena ' tunaongeza idadi ya watu ambao hawajasoma mtaani ' nkamwambia heeee lazima wasomi wawe wengi???? 'Ndio hasa wasichana wako nyuma kimaendeleo ukilinganisha na wanaume.
Enheee nyingine 'tunaongeza idadi ya watu wasio na ajira hasa wamama' nkamuuliza sasa nani anaajiri wajawazito???? Akajibu ' hata wakijifungua wanabaki mtaani tu wanazunguka bila ajira' Nkamwambia basi mi nna mashamba waje tulime, akasema 'Tanzania nzima utawaajiri wewe una hekari ngapi?????? Nkasema tatu, akasema 'umechoka ee!!!' Nkasema ndio labda nipe sababu nyingine....
Akasema 'ingine labda tujenge madarasa ya ziada kwa ajili ya wajawazito' nkasema acha kichaa tumejenga maabara hazijaisha, shule zingine hazina ata ofisi walimu wanakaa na wanafunzi darasani sembuse madarasa ya wajawazito.... Akasema ' nna sababu nyingine ' nkamuuliza ipi io??????
Akasema ' tujenge zahanati shuleni kwa ajili ya kuwahudumia wajawazito' nikacheka mpaka magego ya salasini na mbili na salasini na tatu yakaonekana, nkamwambia hivi kijijini kwenu ulikotoka kuna zahanati akajibu 'hapana' nkamwambia ndo tutaweza kujenga shuleni?????? Akaduwaa nkamwambia naondoka labda niambie unashauri nini ????
Akasema ' mi naona so kesi kama baada ya kijifungua warudi shule, nkamwambia subili nkaongee na walimu kama watakua tayari kuwapokea manaake nasikia wanaweka ngumu. Hivi ndo nimekuja kwenu walimu na wadau wengine wa elimu nyie mnasemajeee????