Sababu kuu 7 za kwanini kila mwanaume anahitaji mwanamke sahihi

Sababu kuu 7 za kwanini kila mwanaume anahitaji mwanamke sahihi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,852
Reaction score
63,374
Kwangu kipindi ambacho kilinivutia sana ni kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Marekani.

Ni pale Obama akiwa katika kampeni kwenye moja ya majimbo kugombea duru ya pili ya uraisi aliposimamisha hotuba yake na kutambua uwepo wa mkewe Michelle.

Obama alisema, "Mke wangu amekuwa bega kwa bega na mimi tokea niko chuo, kuna kipindi nilishindwa kulipa ada ila yeye ndiye aliyenilipia"

Obama akaenda mbali zaidi na kukiri mbele ya jamii ya kimataifa kwamba asingekuwepo hapo alipo kama sio mke wake Michelle.

Hivyo basi, nashauri kwamba mwanamke ambae mwanaume atakua nae huenda akawa chachu ya mafanikio na baraka kwake au anaweza akamrudisha nyuma kabisa katika mipango yake.

Sababu kuu 7 za kwanini iwe isiwe mwanaume lazima upate mwanamke alie sahihi.

1. Kila mwanamke anao uwezo wa kukuridhisha kimapenzi ila mwanamke sahihi na bora pekee ndiue anaeweza kuku-challenge kiakili na kuwa 'intellectually inspired'.

2. Mwanamke yeyote anaweza kukuteka kihisia, ila yule sahihi pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuteka kiroho na ukamtumikia Mungu wako.

3. Mwanamke yeyote anaweza akakushawishi muandike mpango wa harusi (wedding plan), ila mwanamke sahihi peke yake ndie mwenye uwezo wa kukuandikia na kukushauri mpango wa biashara (business plan)

4. Kila mwanamke anaweza akakubusu tena 'French kiss' ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukutamkia maneno yaliyojaa busara na hekima.

5. Kila mwanamke anaweza akakupenda sana tu tena kama una pesa, ila mwanamke aliye bora pekee ndiye anaeweza kusimama na wewe hata kukuinua pale utakapokuwa huna kitu.

6. Mwanamke yeyote anao uwezo wa kukushibisha kwa kukupikia chakula kitamu, ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukulisha chakula cha ubongo.

7. Kila mwanamke anao uwezo wa kukushawishi chumbani ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukushawishi umrudie Mungu wako.

Mwisho ngoja nihitimishe kwa kusema hivi ukisoma vitabu vya kihistoria kuhusu Winstom Churchhill mpaka Abraham Lincoln, na kutoka kwa Nelson Mandela mpaka kwa Martin Luther King Jr lao moja kwamba “No matter how strong a Man is, he is only as strong as the Woman he marries” Kwa tafsiri yangu ya kuunga unga isiyo sahihi sana Wanamaanisha "haijalishi ni kwa kiasi gani mwanaume una nguvu, nguvu zako zina athiriwa kwa kiasi kikubwa na mwanamke utakaemuoa"

Hivyo bas kiushauri unatakiwa uowe mwanamke mwenye kumjua Mungu sana kuliko anaeijua Dunia saaana.
 
Ni somo zuri sana mkuu binafsi nimelielewa!!! Naongezea...Mwanamke mzuri ni bora ni yule atakayekulindia siri zako za ndani...

Ni yule ambaye atakunyanyua kipindi umeanguka huku ukiwa unachekwa na kudharauliwa, yeye atakuwa pamoja nawe katika tabu zote..

Ni yule ambaye huelewa maisha ni kupanda na kushuka.

Ni yule ambaye anayajua mapungufu yako na ni muelewa wa ule usemi wa Hakuna binadamu aliyekamilika
 
kwa dunia hii ya leo na Dar hii yenye wanawake watembea uchi na wengine warahisi kufyekwa kama majani basi mwanaume ukibaki na mke mmoja hata awe na hizo sifa zote hamna kitu utachepuka tu, na mwanzo wa matatizo yetu mengi ni uchepukaji..oeni wake wawili, waunganishe wawe marafiki, wapende na watendee haki ktk kuwatunza apo ndo utaona matunda ya maisha ya ndoa
 
Unapooa hakikisha Mkeo amekukamilisha katika yotee yaaaan awe mzuri moyoni ,,lkn pia bado nauzuri wanje ambao umeupenda weee hadi kuccha zake.

Kinyume nahapo ..utamuoa sababu anamoyo ,, lkn nje utakutana ma mwanamke kajazia balaaa ,, Kama huna akili utasema ivi "" Uzuri nmeoa ,,ngoja nionje ya huyu * nahuo ndio mwanzo wa utungu.
 
Msisahau pia wanaume tunatengenezwa pia. Mwanamke anaweza akaroga ili umuone yeye ni bora na sahihi kwako...!!

Na tatizo lingine ni kwamba, unaweza ukaonesha mapenzi mpk ya kuweza hta kumlamba miguu, ila tafsiri yake atakayokupa mbele ya public ni kwamba amekuweka kiganjani, wala huruki kwake. Na hapo ndo huwa tatizo...!!!
 
kwa dunia hii ya leo na Dar hii yenye wanawake watembea uchi na wengine warahisi kufyekwa kama majani basi mwanaume ukibaki na mke mmoja hata awe na hizo sifa zote hamna kitu utachepuka tu, na mwanzo wa matatizo yetu mengi ni uchepukaji..oeni wake wawili, waunganishe wawe marafiki, wapende na watendee haki ktk kuwatunza apo ndo utaona matunda ya maisha ya ndoa
Mhh! Wew kakuambia nan kunawanaume hata waoe wanawake 20 bado watachepuka tu
 
Nilitaka kusema hivyo.
Wanasahau kuwa kila leo humu mada zao ni kusifia wenye chura Halafu wanatuletea ngonjera hizi wakati sie huku tunahangaika na kumtengeneza chura, hawaelewi wanataka nini hawa wenye midudu rungu
 
Uwii eti Michelle alimlipia Obama ada jmn huu uongo sio wa nchii hii, wengine tunawajua Obamas kwa mengi hili la ada hapana aisee..watu wamekutana Ofisini ishu za ada ziliingiaje...em tupe reference??
Ushawahi soma vitabu alivyoandika Obama kweli wewe?,
 
Wanasahau kuwa kila leo humu mada zao ni kusifia wenye chura Halafu wanatuletea ngonjera hizi wakati sie huku tunahangaika na kumtengeneza chura, hawaelewi wanataka nini hawa wenye midudu rungu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wanasahau kuwa kila leo humu mada zao ni kusifia wenye chura Halafu wanatuletea ngonjera hizi wakati sie huku tunahangaika na kumtengeneza chura, hawaelewi wanataka nini hawa wenye midudu rungu
Hawaelewi kabisa nini wanataka.
 
Back
Top Bottom