Sababu kubwa ya wanawake kuzeeka haraka

Aurora

JF-Expert Member
May 25, 2014
7,308
5,270
Natumaini mnaendelea vizuri na ujenzi wa Taifa.

Kumekuwa na sababu lukuki zisemwazo kuwa chanzo cha wanawake kuchoka/kuzeeka haraka, kama vile kuzaa sana, tutojipenda/kujijali, kuanza mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo, unywaji sana wa ulabu/mnazi e.t.c

Lakini mimi naona zote hizo cha mtoto, funga kazi ni hii niliyoiona mimi ambayo huenda ndio inatufanya tuonekane vibibi kabla ya muda.

Hasira + vinyongo + chuki + ubinafsi + kutopenda maendeleo ya wengine ndivyo vinavyotufanya sura zitushuke mapema.

Nawasilisha
Msinichambe jameni khaaaaaaaa
 
Hivyo unavyovisema hupelekea mtu kufa ghafla na maradhi kama presha, ugonjwa wa moyo, na mengineyo. Maradhi hayo ukiwa wakike ama wakiume lazima yatakupata ukiwa una hasira+vinyongo+chuki+ubinafsi+ kutopenda mafanikio ya wenzako.
Kwa upande wangu kuchoka kunasababishwa na
Pombe+umalaya+vilevi(hapa naongelea bangi, nganda, kuberi, sigara)+kukosa muda wa kupumzika+ umaskini na kupoteza matumaini wa maisha+utumwa wa fikra duni.
Ukijumlisha hayo, miaka kumi na mbili tu lazima tukupe shkamoo
 
Naunga mkono hoja yako:
Binti unakinyongo na ex wako, miaka nenda rudi Kisa alimuowa dada mwingine. Chuki: Shost wako kachepuka na mumeo basi unataka kunywa sumu badala ya kutafuta muafaka unaanza chuki na huyo shost., kwanini usionekane kizee. Unatembea unaongea peke yako kwa hasira uliyojaza kifuani, Mimi nasema wanawake tujifunze kusamehe japo ni ngum sana ila ndio tujitahidi kwa afya zetu.
 
Mdogo wangu wa kike huwa anapata shida sana ya kujikausha akiwa na mimi! Pamoja na kwamba nimemzidi miaka 4 lakini tukiwa pamoja shikamoo zote anapewa yeye matokeo yake anashindwa kuitikia! Hata hivyo, tatizo lake yeye ni umbo lake kubwa!
 
Unywaji wa pombe kupita kiasi hupelekea upotevu wa kumbukumbu na matatizo mengine ambayo siyakumbuki vizuri.
 
Wanawake mnaongoza kwa kurudishana nyuma aisee duuh!!! Wengi wenu mna roho ya kwanini sana yaani hi ni nyie wenyewe kwa wenyewe hamuwezani kabisa.
 
Hata arbortion nyingi sasa wengine huua hata watoto kumi na kuendelea kwanini usichakae vitoto uvitupe halafu huli vizuri Ku recover ukiolewa ukipata watoto wawili mashavu yachuma mchichq. Wanawake wengi hutumika kingono sana na wanaume tofauti tofauti mana too much sex sio health kwanini usikongoroke. Watanzania wengi hawa afford balance diet na mipombe mikali ndo usiseme. Huko vijijini wamama wanazaa watoto kumi maisha magumu wao na wazalisha wakubwa na walezi majukumu yanawazidi lazima wachoke. All in all mwili nao unahtaji kuheshimiwa na kutunzwa
 
Back
Top Bottom