Sababu iliyofanya watu wa zamani wasivae nguo

life coach

Senior Member
Apr 11, 2017
121
401
Sote tunafahamu ya kwamba hapo kale mababu na mabibi zetu wa kipindi hicho hawakuwa na tamaduni ya kuvaa nguo. Zipo nadharia nyingi ambazo hueleza kwanini watu hao wa kale wahakuwa wakivaa nguo, baadhi ya nadharia hizo husema kwamba kwa kipindi hicho wazee wetu hawakuwa na tekinolojia ambayo ingewawezesha kutengeneza nguo na hivyo kujisitiri kwa nguo hizo.

Nitumie nafasi hii kupinga nadharia hiyo ya uongo kwani wana historia wanafahamu ya kwamba teknolojia ya utengenezaji nguo ilikuwepo tangu zamani sana kwani kunakipindi wazee wetu wa kale walianza kuvaa nguo na wakaja kuacha tena baada ya muda.hivyo basi swala la wazee wetu hao kutokuvaa nguo halikutokana na kukosekana kwa teknolojia ya utengenezaji wa nguo hizo.

Sasa ni kitu gani hasa kiliwafanya wazee wetu kutotaka kuvaa nguo? Jambo kubwa ambalo liliwafanya wazee hao kutokuvaa nguo lilikuwa ni rangi za nguo hizo. Sasa ili kuelewe kwanini rangi za nguo ndo zilisababisha wazee hao kukataa kuvaa nguo itabidi nidadavue kuhusu rangi kwanza.

Mwanga na macho ndo vitu ambavyo vinatufanya tuweze kuona. Mwanga wa jua hua ni mchanganyiko wa kila rangi. Mwanga una tabia kuu mbili ambazo ni kuakisiwa au kusharabiwa. Kuakisi ni kitendo cha mwanga kutua sehemu fulani na kurudishwa ulipotoka. Kusharabu ni kitendo cha mwanga kutua sehemu fulani na kunyonywa.

Sasa ili tupate kuona rangi flani ni lazima mwanga upate kusharabiwa au kuakisiwa.
Hivyo basi kwa mfano mwanga wa jua umetua kwenye kitu chenye flani,basi rangi zote ambazo huunda mwanga huo husharabiwa(hunyonywa) na ni rangi moja tu ndo huakisiwa. Sasa binadamu tunakuwa na uwezo wa kuona rangi hiyo moja ikiyoakisiwa tu.kwaiyo tunavyoona kitu flani labda kina rangi nyekundu,basi humaanisha ya kuwa kitu hicho kimesharabu rangi zote na kuakisi nyekundu tu,kwenye rangi ya njano nk mfumo huwa ndo huo huo.

Ikitokea mwanga umetua sehemu flani alafu rangi zote zikasharabiwa basi tutaona rangi nyeusi na ikitokea rangi zote zimeakisiwa basi tutaona rangi nyeupe.
Sasa rangi huwa na maana na kila rangi huwakilisha tabia za mwanadamu.

Katika mfumo wa maisha ya mwanadamu,mwanadamu huwa na uwezo wa kufanya vitu vingi sana,lakini pamoja na uwezo wa kufanya vitu vingi, wanadamu huchagua vitu vichache tu ambavyo huvifanya na watu wengine wakapata kuona.

Hivyo basi mwanadamu hujajiwa au hujitambulisha kwa mambo anayoyafanya na wala sio aliyonayo kwa sababu watu hawana uwezo wa kujua kilichopo ndani ya mtu bali wanaweza kujua kile kinachofanywa na mtu mana ndo huonekana, hivyo basi mwanadamu pia kuna mambo anayasharabu na kuna mengine anayaakisi,so mambo ambayo anayaakisi ndo hutumika kumtambulisha mtu huyo kwa jamii husika.

Mfano tumchukue joti.inawezekana ya kuwa joti anavipaji vingi sana kama kuimba,kucheza mpira na kuchekesha, sasa kucheza mpira na kuimba huwa ndani ya joti lakini hajafanikiawa kuvitoa nje na alichofanikiwa kukitoa nje ni uchekeshaji hivyo basi joti hujitambulisha kama mchekeshaji kwa wanajamii mana ndo kitu alichokitoa nje na watu wakaweza kuona mana alivyonavyo ndani hakuna mwenye uwezo wa kuviona. Sasa nikirudi kwenye hoja ni kwamba rangi hubeba maana flani kwa mfano nyekundu uashiria madaraka, bluu huashiria upendo, zambarau huashiria ubunifu au akili,nyeusi huashiria uchoyo, nyeupe huashiria kujitolea na machungwa huashiria matamanio ya kimapenzi.

Sasa wazee wa zamani hawakutaka kuvaa nguo,kwani kila nguo huwa na rangi na kila rangi huwa na maana,so wazee hao walikuwa hawataki kuakisi matamanio yao nje ili watu wengine weweze kuyajua. Kwani kwa kuvaa nguo yenye rangi nyekundu kila mtu angekuwa anajua ya kuwa mtu huyu anatamani madaraka, kwa kuvaa nguo nyeusi kila mtu angefahamu ya kuwa mtu huyu ni mchoyo nk.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom