Sababu gani zilifanya Jay Jay Okocha asitwae Ballon D' or enzi zake?

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,773
7,275
Wakuu karibuni tujadili sababu zilizomfanya fundi wa soka toka Nigeria na Africa kwa ujumla, Austin Jay JAy Okocha kushindwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia enzi zake akisakata kabumbu licha ya uwezo na kipaji maridhawa cha hali ya juu alichokuwa nacho.
 
Kipindi hiko kulikuwa na wakali weengi sio kama sasa wanasemwa wawili tu Mesi Ronaldo........kipindi hiko Ronaldo de Lima,Roberto Carlos,Babangida......na wakali wengi tu hivyo asingeweza kupewa walikuwepo wakali zaidi yake enzi hizo ye alikuwa mkali ila si kwa kiwango hiko unachokisema japo kuna chenga ambazo alipiga enzi hizo hawakuweza kupiga.......mfano Ronaldo de Lima ye ilikuwa ni kupachika magoli tu na chenga au madoido kidogo sana
Okocha huwa namfananisha na kina Ronaldinho
 
Wakuu karibuni tujadili sababu zilizomfanya fundi wa soka toka Nigeria na Africa kwa ujumla, Austin Jay JAy Okocha kushindwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia enzi zake akisakata kabumbu licha ya uwezo na kipaji maridhawa cha hali ya juu alichokuwa nacho.
Sababu hakuwahi pata Mafanikio... i mean Makombe Makubwa na Pia kulikuwa na Wakali wengi Sana...
 
Afrika tuu alipata tabu kwa washindani wake Kalusha bwalya, Kanu,Weah,Hadji,Eto na wataalam wengineo wengi tuu waliokua na mafanikio kosa alilofanya ni kuchelewa kutoka PSG maana kipindi kile ilikua ni daraja la kupita yeye alifika wenzie wakina Gaucho walitoka mapema umri bado unadai bado...
 
Kupiga tu chenga haitoshi kuwa mchezaji bora, Denilson alikuwa anapiga chenga zaidi ya Okocha lakini hata namba Brazil ilikuwa shida. Okocha kuna vitu vingi vilimkwamisha mojawapo ni kuchezea timu ndogo, PSG then Bolton hizi timu zilikuwa dhaifu sana kwa kiwango cha Okocha, kama mnakumbuka Gaucho pia alikuwa PSG lakini mafanikio aliyapata baada ya kuhamia Barcelona Okocha yeye alienda Bolton. Ukiacha ngazi ya Club ukija timu ya taifa Nigeria pamoja na kuwa na golden generation ya wachezaji kama Sunday Oliseh, Taribo West, Rashid Yekini, Kanu, Babayaro, Babangida, Victor Ikpeba, Uche, Amokachi name wengineo lakini Nigeria hii haikuweza kubeba hata AFCON, world cup 1998 waliishia round ya pili wakapigwa 4-1 na Denmark. Sasa niambieni Okocha apewe uchezaji bora kwa kigezo kipi? Nwankwo Kanu alikuwa na mafanikio zaidi ya Okocha, alibeba Uefa na Serie A akiwa Intermilan, akaja Arsenal akabeba EPL na FA cup.
 
Wakuu karibuni tujadili sababu zilizomfanya fundi wa soka toka Nigeria na Africa kwa ujumla, Austin Jay JAy Okocha kushindwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia enzi zake akisakata kabumbu licha ya uwezo na kipaji maridhawa cha hali ya juu alichokuwa nacho.

Kaka naona unababaishwa na Ronaldo Xtian na Messi kuwa wanapokezana, ukweli ni kuwa kwa sasa hakuna mafundi wa soka Duniani, wako wachache sana na ndio kisa cha hawa wawili kupokezana,
Hebu kumbuka wakati Ronaldo de Lima, Rivaldo, Carlos, Mtume Gaucho, Decco, Figo, Zidane, Okocha, Chev nk hapo ilikuwa ni shughuli pevu kumchagua best player
 
Ina maana xavi,iniesta,Modric,Marcelo nk siyo mafundi

Ishu saizi ballon dor saizi wanatizama idadi ya magoli

Hata zizzou angekuwa enzi hii ballon dor angesikia kwenye bomba

Ballon dor ni kwaajili ya strikers siku hizi
 
Kaka naona unababaishwa na Ronaldo Xtian na Messi kuwa wanapokezana, ukweli ni kuwa kwa sasa hakuna mafundi wa soka Duniani, wako wachache sana na ndio kisa cha hawa wawili kupokezana,
Hebu kumbuka wakati Ronaldo de Lima, Rivaldo, Carlos, Mtume Gaucho, Decco, Figo, Zidane, Okocha, Chev nk hapo ilikuwa ni shughuli pevu kumchagua best player
Mkuu unataka kuniambia suarezi,neymar, aguero , Diego Costa, lewandosk , n.k hawajui?? Wachezaji wanaofunga 20+ goals per season unawasahau mkuu....

Ngoja nikwambie kitu sio kwamba recently hakuna wachezaji wazuri la hasha... Ni bahati mbaya wametokea kipindi cha messi na neymar .... Messi msimu juzi laliga alifunga magoli zaidi ya 40 kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu mungu kaumba huu ulimwengu ...
 
Ni Kama aThierry Henry, alikuwa Mkali kipindi cha wakali wengi sio Kama Siku hizi Messi na Ronaldo zaid ya Miaka 10

Mechi ya Mtoano World CUP 1998 Nigeria vs Denmark Jay Jay alionesha ufundi wa Karne lakin Mwishowe wakalazwa 4-1, naikumbuka sana hii Mechi Kama Jana vile
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom