Sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010

Siyo kwamba wapiganaji hawako tayari ila wanaogopa kukolimbiwa ndo maana hawagombei!
 
Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..

Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!


51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao!

50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake.

49: Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Ahadi hii haionekani kutekelezeka. Inaonekana ametimiza ahadi ya maisha bora kwa kila muwekezaji wa kigeni!

48:Alitangaza kuwa wizi umefanyika Benki Kuu kwa kukombwa mabilioni; badala ya kuacha uchunguzi wa jinai akaunda Kamati kuchunguza jinai. Matokeo yake ni kucheleweshwa kwa upatikanaji wa haki.

47: Serikali yake imeshindwa kutekeleza maazimio yote ya wananchi wa Tanzania kama yalivyoanishwa na wawakilishi wao Bungeni katika maazimio kufuatia Kamati Teule ya Kuchunguza Richmond. Matokeo yake ni kuchochea mgawanyiko mkubwa kabisa wa kimaslahi katika historia ya taifa letu.

46: Aliahidi kupitia mikataba yote mikubwa ya madini ili kutengeneza hali ya "win win win". Hadi hivi sasa hakuna mkataba hata mmoja uliopitiwa na kusahihishwa na badala yake serikali yake imetangaza kuwa mabadiliko ya sheria ya madini yataendelea kuwanufaisha wawekezaji wa sekta hiyo.

45: Akiwa ni Mwenyekiti wa Chama Tawala ameshindwa kuleta nidhamu ndani ya chama na matokeo yake wanachama wake mashuhuru wanatukanana na kuitana majina hadharani. Kile kilichoitofautisha CCM miaka ya nyuma sasa hakipo tena.

44: Aligawa fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa kile kilichojulikana kama "mabilioni ya Kikwete" Hadi hivi sasa haijaoneshwa ni kiasi fedha hizo zimeweza kubadilisha maisha ya waliozipata na kurudisha faida.

43: Aliahidi kuunda Baraza dogo la Mawaziri lakini matokeo yake Baraza lake limekuwa kubwa na lenye ufanisi mdogo.

42: Alidai hadharani kuwa anawajua vigogo wa kuuza madawa ya kulevya na kuwa amewapa muda wajirekebishe. Miaka minne baadaye hajatuambia kama watu wale wamejirekebisha au la.

41: Aliahidi kuwa hakuna mwanafunzi wa Kitanzania anayehitaji elimu ya juu ambaye atashindwa kuipata. Lakini serikali yake iliwarudisha vijana wa Kitanzania waliokuwa wanasomea shahada mbalimbali ikiwemo Uhandisi na Udaktari kutoka Ukraine kwa kudai kuwa serikali haina fedha. Vijana wale 30 ingewagharimu shilingi milioni 400 tu kwa muda wa miaka minne. Kiasi hicho ni sawa na kiasi kilichochangwa na serikali kuipongeza Taifa Stars kwa kuifunga Togo!

40: Amewaruhusu watendaji wake wakubwa kutumia vyeti vya kielemu ambavyo havitambuliki na vyenye utata. Miongoni mwao ni Waziri wa Fedha Bw. Mustafa Mkullo na Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT Bw. Emmanuel Nchimbi.

39: Licha ya kuahidi kutatua tatizo la nishati chini ya uongozi wake Tanzania imezidi kukabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kuliko wakati mwingine wowote huku nchi yetu ikiwa na vyanzo vya kutosha kabisa nishati hiyo ambayo serikali yake imeshindwa kuviendeleza.

38: Amekuwa akiendeleza safari za nje yeye na viongozi wa ngazi za juu ambazo zimegharimu zaidi mabilioni ya shilingi kwa safari, posho, matumizi ambayo hataki kuyaweka hadharani.

37: Ameendeleza fikra za uduni wa Mtanzania kwa kutukuza wageni na hivyo kuendeleza kuhukumu taifa letu kwenye utegemezi wa kudumu kwa kupokea misaada ya kiudhalilishaji ya mambo ambayo yamo ndani ya uwezo wa kuzaliwa wa Watanzania.

36: Serikali yake imeendelea kuwaficha wananchi wa Tanzania mambo muhimu yanayohusu serikali yao na hivyo kuwanyang'anya wananchi usimamizi wa serikali yao kwa kuficha mambo ya Meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, na Tangold.

35: Akionesha kutokujali sifa za watendaji wake amewateua watu mbalimbali wenye utata wa maadili, na elimu na kuwapa nafasi za kuongoza wizara, na idara nyeti. Miongoni mwao:

- Mustaffa Mkullo - Waziri wa Fedha
- Emmanuel Nchimbi - Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT
- Andrew Chenge - Alikuwa Waziri wa Miundombinu
- Peter Noni - aliyesimamia akaunti ya EPA ikichotwa na sasa kapewa Benki ya Raslimali (TIB)
- n.k

34: Serikali chini yake imevumilia vitendo vya uharibifu mkubwa wa mazingira na hata kutishia maisha kama yale yaliyotokea huko mgodi wa Mara ambapo watu wamerudhika kutokana na sumu inayotoka mgodini.

33: Alitangaza kwa wananchi kuwa msukosuko wa kiuchumi uliokumba dunia usingeleta matatizo ya kiuchumi kwa Tanzania; miezi michache baadaye serikali yake ikaidhinisha zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya "kusisimua" uchumi bila kuweka utaratibu wowote wa kupima mpango huo na kuonesha kitaalamu haja ya mpango huo zaidi ya kuongeza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali.

32: Ameshindwa kuliongoza Taifa kwa misingi ya Ujamaa ambayo imeanishwa katika Katiba ya Jamhuri na Katiba ya Chama chake na hivyo kuendelea kufanya kazi na kuendesha serikali kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuihifadhi.

31: Licha ya kupigiwa kelele dhidi ya uwekezaji wa kampuni ya India ya Rites Consortium kwenye shirika letu la Reli, aliendelea na kuhakikisha wanawapa mkataba huo. Matokeo yake ni yale yale tuliyoyaona wakati wa Mkapa; mwekezaji kashindwa na anaondoka tajiri!


30: Licha ya kubuni na kuhubiri juu ya umuhimu wa Kilimo, ameshindwa kuiongoza CCM kama chama na jumuiya zake kuwekeza katika kilimo kikubwa cha mfano kama chanzo cha mapato endelevu.

29:Kama ilivyokuwa kwenye sakata la Richmond, serikali yake imeingia mkataba na kufanya kazi na kampuni ya kitapeli ya Dowans ambayo iliingia nchini kinyemela na kuhalalishwa kwa kutumia maelezo ya uongo. Hadi hivi sasa hajakubali kuanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo.

Namba 36, 39, 43 na 48; ni kati ya hayo ambayo mimi nimezingatia kupima kufaa mtu kuwa kiongozi wa nchi yenye lengo la kujikwamua kutoka kwenye umasikini. Maana haiingii akilini mtu anayejiita kiongozi aachie watu wafuje mali kupitia TANGOLD, MEREMETA na dada zake ili tu kunufaisha wachache halafu akanyamaza na kusema nitagombea tena. Unagombea kwa ajili ipi, je ni kuwatumikia watanzania ama ni kwa sababu hujaridhika na ulichochuma awamu inayoisha. Je, ni kukosa uzalendo ama kutokuwa na uwezo wa kuongoza ndiyo tatizo? Lolote kati ya hayo mawili linatosha kunifanya niseme hafai kuwaongoza watu wanaoimba muda wote kuondoa umasikini kichani mwao.

Tunahitaji mtu mwenye machungu na kuona watanzania wanavyoteseka na ana moyo wa dhati kutumia uwezo wake wa kuongoza kubadilisha maisha yao. Watu wanaingia madarakani kulinda masilahi ya chama zaidi na kusahau walivyoviimba wakati wakitafuta kupigiwa kura. Yako wapi leo? Matokeo yake sasa mabaya yanayomeza rasilimali za nchi yananyamaziwa ili chama kisiaibike, kuna uzalendo hapo? Nani alisema endapo kiongozi atakemea mabaya CCM itakosa umaarufu? Vinginevyo, na wewe ni muhusika, huwezi kunyamazia udhaifu kama huu ambao tumekuwa tukiuona tangu miaka saba hivi iliyopita ndani ya nchi yetu! Tena maovu yanayofanywa na wanasiana yanazidi kuongezeka siku hadi siku na wakubwa wananyamaza tu na kupigiana kampeni wenyewe atagombea peke yake. Wakati huo wengine wakiagizwa kunyamaza kujipigia kampeni.

Tunapelekwa wapi jamani? Unapofika wakati wa kuongelea masuala yanayohusu maisha yetu nawaomba watanzania waache kutania. Tunatakiwa tuwe wanasayansi kuifanya nchi yetu kutoka hapa ilipozama (kwenye umasikini). Watu anashindwa kushughulikia masuala nyeti, wanakimbilia kukata rufaa za hukumu ya mgombea binafsi! Woga wa nini? Kama serikali iko makini kiutendaji kupitia wanasiasa wake, wanaogopa nini kuwepo mgombea binafsi? Sasa tunaendelea kupoteza rasilimali zetu (fedha) kuwalipa kamati za kuandaa rufaa kama hizi zisizo na masilahi kwa umma.

Tunashindwa kusimamia matatizo ya kuhakikisha fedha za TANGOLD, MEREMETA na mengine maovu zinarudisha kwa uwazi kwa kuwashughulikia wote waliohusika kuchelewesha fedha hizo kutumika kwenye miradi ya maendeleo (hospitali, shule na miundombinu mingine mingi ya kuturahisishia kupigana vita ya umasikini). Wako wapi hao wanaosema wangependa waone mtu mmoja akisimama kugombea URAIS? Lengo lao ni nini? Wana masilahi gani? Je, wana uzalendo ndani ya mioyo yao? Hata hivyo sishangai maana mmoja wao alishasema siku moja, yuko kufa akimtetea mtu mmoja. Siyo kuwatetea masikini watanzania watoke kwenye dimbwi la umasikini.
 
Jamani kuongoza nchi sio sawa na kampuni ambayo sheria na operating guidelines zipo wazi. Kuongoza nchi ni sehemu ya SIASA.

Hata akipewa yeyote miongozi mwenu humu bado mapungufu yaktakuwepo tu.
 
Jamani kuongoza nchi sio sawa na kampuni ambayo sheria na operating guidelines zipo wazi. Kuongoza nchi ni sehemu ya SIASA.

Hata akipewa yeyote miongozi mwenu humu bado mapungufu yaktakuwepo tu.

ni jambo moja kuwa na mapungufu; ni jingine kutokuwa na uwezo!
 
ni jambo moja kuwa na mapungufu; ni jingine kutokuwa na uwezo!

Pia ni jambo lingine kuwa na uwezo na kutumia uwezo kuleta uharibifu

Kutokuwa na uwezo ni subjective term, wewe unaweza kusema JK hana uwezo mwingine akasema ana uwezo

Kama quantity (number of voters) ina determine ubora wa mtu JK amewashinda wengi na atawashinda wengi....siku zijazo

Mapungufu ya JK yanavumilika sana kuliko mapungufu ya Mkapa
 
Back
Top Bottom