tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 26,023
- 25,430
.
Serikali ya Chama Cha Mafisadi (CCM) ndiyo muasisi na kinara wa ufisadi hapa nchini. Hiki chama na serikali yake hawawezi kupambana na ufisadi kamwe. Mapambano dhidi ya ufisadi kwa CCM ni sawa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano, jambo ambalo katika hali halisi, haliwezekani katu. CCM na serikali yake wamezoea kufisidi mali za umma kiasi kwamba inakuwa vigumu kwao kuwasikiliza wale wazalendo wanaowakataza au kuwashauri waachane na ufisadi. Wanadhani kwamba kufisidi mali za umma ama ni haki yao ya msingi au ni haki yao ya kuzaliwa! Hapo ndipo serikali ya kifisadi ya Chama Cha Mafsadi ilipotufikisha.
.
Ili kuepukana na ufisadi wa CCM, hatuna budi kuwapiga chini kwenye uchguzi wa mwaka huu wa 2015. Hiyo ndiyo njia rahisi na sahihi ya kupambana dhidi ya ufisadi. Hii ni kwa kuwa huwezi kuitenganisha CCM na ufisadi. UFISADI na CCM ni kama kuku na yai. Ili upate yai sharti ufuge kuku; na ili upate kuku sharti uwe na mayai ya kutotolea vifaranga ambao wakishakomaa huwa kuku. Hivyo basi, ili kuepuka mayai (yanayotoa kuku), huna budi kuwachinja kuku wote na kuwafanya kitoweo. Vivyo hivyo, huwezi kupambana na ufisadi kikamilifu bila kuwang?oa CCM kutoka madarakani. Tukifanikiwa kuwang?oa CCM madarakani tutakuwa tumeumaliza ufisadi nchini.
.
Ndugu watanzania, hii sio hadithi wala ndoto za Ali Nacha hata kidogo. Tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na hawa kupe wasioshiba kamwe. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwafutilia mbali CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, ?If a person deceives you once, shame on him; if twice, shame on you?. Tafsiri isiyo rasmi ya maneno haya ni kuwa. ?Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako?. Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba mtu akikudanganya mara ya kwanza utakuwa na nafasi ya kumjua alivyo kwa tabia; na akija kukudanganya mara ya pili usikubali katu! Tumia uzoefu wa danganyo la kwanza ili kumkatalia. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!
.
Watanzania wenzangu, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?
Kuku wa kienyeji hupenda kujichakuria chakula mwenyewe kwenye vichaka bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watakudharau sana. Watakuona kama unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wachichakurie wenyewe chakula duni walichokizoea huko kwenye vichaka.
.
Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha punda mzigo mwepesi, humdharau sana na kumuona kama hampendi. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa (birth right)! Ukimbebesha punda mzigo mwepesi halafu ukakatiza karibu yake, hakawii kukupiga mateke ili kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Atakuchukia na kukuona kama mtu usiyemtakia mema katika harakati zake za kubeba mizigo mizito kupindukia.
.
Nadharia hizi mbili zinaelekea kufanana na namna ya maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu kama ambavyo punda na kuku wa kienyeji wamezoea kuishi kwa kuchakura na kubeba mizigo mizito mtawalia (respectively). Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wamekuwa mstari wa mbele kukiunga mkono na kukifanya kiendelee kubaki madarakani mpaka leo. Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?
.
Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi na mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Yesu Mwokozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kuendelea kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka huu wa 2015. Tukimbie tukatubu dhambi zetu kwa Yesu kabla huyu ibilisi hajatutoa roho!
.
Nimetumia hii nadharia rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hivyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kupiga vita UMASIKINI kwa kuwang?olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura. Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali naye. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa makupe (mafisadi wa CCM) walishakuwa sugu. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (miaka 54) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo aliyoyaleta mkoloni (pamoja na kwamba tulimuona mkoloni kuwa dhalimu na katili).
.
Nyayo na alama alizotuachia mkoloni zinaonekana zaidi kuliko alama zilizoachwa na CCM na serikali yake. Mtandao wa reli aliouacha mkoloni unaonekana hadi leo. Badala ya serikali dhaifu ya CCM kuendeleza hii reli, ambayo ni mkombozi mkubwa kwa usafiri wa mlalahoi, wao walichofanya ni kung?oa baadhi ya mataaruma ya reli ili kukata mawasiliano. Na hawakufanya hivyo kwa bahati mbaya. Lengo lao lilikuwa kuua usafiri wa reli ili wapate kuwakamua masikini kwa kuwapandishia nauli kwenye magari wanayomiliki. Huu udhalimu umetimia siku za hivi karibuni na kila mtanzania atakuwa ni shahidi.
.
Mbali na reli, mkoloni alijenga bandari, shule, hospitali, viwanja vya ndege na miundombinu kadha wa kadha ambavyo vimetelekezwa na mafisadi wa Chama Cha Mabwepande (CCM) na serikali yake, kwa gharama ya watanzania masikini, wanaoishi chini ya dola moja kwa siku, huku mafisadi wa chama na serikali wakiishi kama vile wako peponi na kama hawatakufa.
.
Mkoloni alituachia shule nzuri ambazo zipo hadi leo. Kwa mfano, kwa wale mliosoma Tabora Boys (zamani Tabora School) mtakuwa mashahidi wetu. Hii ni mojawapo ya shule iliyoachwa na wakoloni na ilijengwa kwa kiwango cha hali ya juu. Mifano ya shule ni mingi. Mimi nimesoma Mara Sekondari (zamani Musoma College); pia kuna jirani zetu Musoma Sekondari (zamani Musoma Alliance). Hizi zote ni shule zilizojengwa na mkoloni na zipo hadi leo.
.
Bandari ya Dar es Salaam ilijengwa na mkoloni mweupe. Baadaye Mwl Nyerere aliifanyia marekebisho kidogo. Tangu hapo haikuwahi kupanuliwa tena na mkoloni mweusi. Miaka 54 baada ya uhuru ndipo tunakwenda kujikomba kwa Wachina waje watujengee bandari mpya ya Bagamoyo. Yakhe, hamna khaya? Siku zote hizo mlikuwa wapi msijenge bandari mnakuja kugutuka leo?
.
Hospitali ya Muhimbili (zamani Sewa Haji Hospital), pamoja na hospitali kadhaa nchini zilijengwa na mkoloni. Sasa hawa wakoloni weusi wao wamefanya nini kwa hiyo miaka 54? Wametutia ufukara tu!
.
Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa kuleta ?maisha bora kwa kila mtanzania?, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kauli mbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 9 alizoziacha Mkapa hadi 35 za sasa! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi ?maisha bora kwa kila mtanzania?, tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Mchague Laigwanan Edward Moringe Ngoyai Saitoti Ole Lowassa atukomboe kutoka kwenye lindi hili la umasikini wa CCM.
.
Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajitokeza kumpgia kura LOWASSA wa CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA ili atuondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo lake kubwa akitaka kutumeza bila huruma. Hiyo ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi (Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).
.
Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ?wakata tamaa? ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing?oa CCM madarakani kupitia uchaguzi mkuu wa Jumapili, tarehe 25/10/2015!
:yield: