Elections 2010 Sababu 10 za kutomchagua Kikwete 2010

tikotiko

Member
Jul 9, 2010
26
0
Mimi nikiwa kama mpiga kura, nimeamua kutomchagua KIKWETE, hata kama kura yangu haitasaidia kitu bado nitafurahi kuweka alama ya NO kwake!! Sabau zangu ni hizi hapa:-

1. Chini ya uongozi wake uchumi umeshuka na thamani ya shilingi dhidi ya dola imezidi kuporomoka zaidi
2. Ameshindwa kuboresha maisha ya mtanzania wa kawaida (tofauti na kauli mbiu yake "maisha bora kwa kila mtanzania". Amepiga kelele ya KILIMO KWANZA huku tunaona dhahiri hana nia yoyote kukuza kilimo! Ni msaliti
3. Ameshindwa kuboresha miundombinu (barabara etc)
4. Chini ya uongozi wake, amefanya uteuzi wa aibu kwa Mkurugenzi wa ATC ambaye ni mshikaji wake, matokeo yake ameua kabisa ATC…Tanzania (kama nchi) inashindwa hata na mfanyabiashara binafsi anayendesha Precision Air kwa mafanikio
5. Akiwa rais wa Tanzania ameshindwa kusimama imara kutetea maslahi ya nchi dhidi ya wizi wa mali ya umma na kashfa ya mabilioni ya shilingi ya Richmond...JE NAYE ALIHUSIKA? PCB NA USALAMA MNAJUA WENYEWE...ENDELEENI KULINDA MASLAHI YENU!!
6. Yeye kama kiongozi wa Nchi amewakebehi hadharani wafanyakazi wa Tanzania na viongozi wao pale TUCTA ilipotaka kuitisha mgomo. Yeye kama kiongozi mkuu wa nchi hakuwa na taarifa sahihi kutoka kwa watendaji wake, akawanawa viongozi wa wafanyakazi mbele ya wazee wa CCM, cha ajabu yeye ndiye alikuwa hana taarifa sahihi! Kama kiongozi alitakiwa kuwajibika mara moja. URAIS NA USWAHILI WAPI KWA WAPI?
7. Katika kipindi chake cha uongozi amefanya uteuzi wa viongozi wasiokuwa na uwezo, wakiwemo baadhi ya mawaziri (washkaji) ambao wamekuwa wakiweka mbele maslahi binafsi na kutojali wananchi.
8. Katika kipindi chake cha uongozi RUSHWA IMEONGEZEKA na hakuna hatua madhubuti alizochukua zaidi ya kuwa msemaji saaaaana bila vitendo.
9. Katika kipindi chake cha uongozi matimizi mabaya ya fedha katika manunuzi ya magari ya kifahari na fanicha kwa viongozi wa serikali, wakiwemo wakuu wa mikoa, mawaziri na yeye mwenyewe AKIONGOZA UOZA HUO KWA KUNUNUA BMW X-5 kwa matumizi yake.
10. Ni kiongozi aliyesafiri mara nyingi zaidi ya waliomtangulia (katika awamu ya kwanza ya uongozi wao), safari hizi zimetumia mabilioni ya feadha za watanzania lakini hakuna faida tunayoiona kutokana na safari zake.

TUUNGANE KUSEMA NO KWA KIKWETE
 
kwa kuongezea tu, mbali na kuteua watu kwa misingi na dini, pia amekuwa akiteua mademu kwa misingi ya..(anaijua yeye mwenyewe na watanzania wengi tunajua ni kwa nini anakuwa anawateuwa mademu hao) ukizingatia kuwa wanakuwa hawana uwezo wa kushika nyadhifa hizo walizopewa...say NO to him please for the better tomorrow of the beautiful Tanzania.
 
Ni katika kipindi cha Kikwete ndo tumeshuhudia ujambazi wa kutisha wa kutumia silaha na mauaji ya watu ya kila kunapokucha. Amani ya nchi ilishapotea tangu huyu bwana alipoingia madarakani. Hana uwezo hata wa kulinda usalama wa raia wa Tanzania wala usalama wa nchi kwa ujumla. Katika kipindi cha miaka miwili tu, nimeshapoteza marafiki zangu wa karibu kabisa watatu kwa kuuawa na majambazi. Sina tena hamu na CCM wala Kikwete wake.
 
ni JK huhuyu ambaye ameshindwa kujipambanua ili kuonesha msimamo wake katika mambo ya msingi ikiwamo ufisadi na badala yake kuchekacheka tu tena kwa hila sana.
 
hawezi kufanya maaamuzi magumu... anapiga picha na Ma-selebriti wasio na faida na nchi hii, anagharamia matukio makubwa, yasio na faida kwa watanzania na kwa kutumia hela ya walipa kodi(Mfano-dhifa za timu za mpira)
 
mimi nikiwa kama mpiga kura, nimeamua kutomchagua kikwete, hata kama kura yangu haitasaidia kitu bado nitafurahi kuweka alama ya no kwake

kati ya vitu ninavyoenjoy ni kuinyima ccm kura yangu since vyama vingi vianze; ingawa wanashinda... It feels goooooooood

huyo jamaa ni msanii, ila at least wa tz wengi wameanza kumstukia.
 
11. Anadanganyika kiurahisi saaaana

12.hailipi kumchagua,watanzania wote tunaonekana wajinga hakuna kinachotekelezeka...na amini usiamini 2010 lazima mademu wataongezeka na ukitaka kuchaguliwa km wewe demu lazima uwe na reception ya kuvutia...Please say No to Jk.Yeye sio msanii ni nyumba ya Sanaa.
 
simchagui kwa sababu anapenda kucheka ovyo ovyo hata kama jambo ni nyeti,vilevile amewapa lungu wanaotoa ajira binafi kwamba eti wajipangie kima cha chini cha mishahara hakijua fika ni makapitalists(max prof and min cost
 
Nchi hii imejaa wageni wachina wasomali wakongo na sasa wameanza kuingia wa guinea tutaishiishi vipi jamani
 
halafu mi nahisi kama ana ka udictecta vile kutokana na kauli zake("hata mkiandamana hampati kitu)," hata mkija na watu wa haki za binadamu hakitaeleweka")
 
ndiye huyu huyu aliyewatukana viongozi wawafanyakazi na kusema hataki kura zetu na ndio maana simpi.
Ni huyu huyu aliyemteua kiongozi mmoja aliyeonekana hafai kwenye umoja wa wanawake akatimuliwa yeye akamteua hivyo kuonyesha dharau kwa viongozi wakuu wa umoja huo ikimaanisha wanawake wote wamedharauliwa kwani hii imeonyesha hana imani na uongozi wa umoja wa wanawake CCM
 
ndiye huyu huyu aliyewatukana viongozi wawafanyakazi na kusema hataki kura zetu na ndio maana simpi.
Ni huyu huyu aliyemteua kiongozi mmoja aliyeonekana hafai kwenye umoja wa wanawake akatimuliwa yeye akamteua hivyo kuonyesha dharau kwa viongozi wakuu wa umoja huo ikimaanisha wanawake wote wamedharauliwa kwani hii imeonyesha hana imani na uongozi wa umoja wa wanawake CCM

Kumbuka Wa-TZ walivyomchoka Sumaye, Mkapa akamteua tena katika kipindi chake cha pili, Wa-TZ tukanyea. Hiyo ndo technic ya Siasa TZ! Hata hivyo nina mashaka na sura ya TZ huyu jamaa akipita.
 
Kumbuka Wa-TZ walivyomchoka Sumaye, Mkapa akamteua tena katika kipindi chake cha pili, Wa-TZ tukanyea. Hiyo ndo technic ya Siasa TZ! Hata hivyo nina mashaka na sura ya TZ huyu jamaa akipita.

Hii ni sababu nyingine ya mimi kutopiga kura mwaka huu.
 
Kumbuka Wa-TZ walivyomchoka Sumaye, Mkapa akamteua tena katika kipindi chake cha pili, Wa-TZ tukanyea. Hiyo ndo technic ya Siasa TZ! Hata hivyo nina mashaka na sura ya TZ huyu jamaa akipita.

Ama kweli siasa kwa Tz ni Sihasa.....
 
Mdau una maana gani unaposema urais na uswahili wapi na wapi, mlitaka ikulu itawaliwe na non muslim peke yao? Iweje anapoingia muislam aitwe mswahili? Acheni majungu mtagawa nchi tumewashitukia na mkimwaga mboga tutamwaga ugali
 
Back
Top Bottom