Sababu 10 za kuichagua CCM

Sababu 10 za kuichagua CCM

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
*CHAGUA CCM*

Jumapili Novemba 26 ni siku ya kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye kata 43 sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Watanzania wapiga kura halali wa maeneo unapofanyika uchaguzi huo wana kila sababu ya kuchagua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na sababu zifuatazo:-

1. CCM ndio chama kilichoshika dola chenye Sera zinazotekelezeka na kukubalika na Watu wengi. Kuchagua upande mwingine ni kujichanganya na kujicheleweshea maendeleo.

2. Ilani ya uchaguzi (mkataba wa kimaendeleo) unaoongoza nchi kuanzia 2015 - 2020 ni ya Chama Cha Mapinduzi. Mwananchi hana sababu ya kuchagua chama (nje ya CCM) ambacho ilani yake haifanyi kazi. Kuchagua CCM ni kuchagua maendeleo.

3. CCM ndio chama pekee kilichoonyesha kwa vitendo kupitia Serikali iliyopo madarakani kupambana vilivyo na rushwa na ufisadi. Mwananchi CHAGUA CCM uonyeshe unaunga mkono mapambano dhidi ya maadui zetu rushwa na ufisadi.

4. Rais aliyepo madarakani ni wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ameonyesha kwa vitendo uzalendo wa kulinda rasilimali zetu (mfano madini). CHAGUA CCM ili kuonyesha unaunga mkono hatua za Rais Magufuli za kulinda rasilimali zetu kwa manufaa yetu.

5. CCM ni chama pekee kisicho na chembe ya ubaguzi wowote ule. Mfano Ukabila, udini, ukanda na urangi. CHAGUA CCM upate maendeleo ya kweli pasipo ubaguzi wowote ule.

6. CCM ndio chama pekee kinachowajali Wakulima, Wafanyakazi, Wafanyabiashara na makundi mengineyo kwa vitendo. Tofauti na vyama vingine vilivyojaa kila aina ya vituko vya kibaguzi. CHAGUA CCM yenye kujali na kuthamini kila Mwananchi.

7. CCM ni chama pekee kinachowatetea Wanyonge nchini. Kupitia Rais aliyepo madarakani Dk. Magufuli anayetokana na CCM ameonyesha kwa vitendo kuwajali zaidi Wanyonge. Leo hii yule aliyekuwa anaonekana mnyonge ana nguvu Kubwa kwenye vyombo vya kisheria, Mahakamani, kwenye huduma za kijamii. CHAGUA CCM uunge mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli za kumkomboa, kumtetea na kumjali Mnyonge.

8. CCM ni chama pekee ambacho Serikali yake iliyopo madarakani inatoa elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya msingi mpaka Sekondari. Na pia inatoa mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa na vigezo. Kama haitoshi imeboresha Huduma za kielimu kwa kuhakikisha kila shule ina Madawati, Maabara, Maktaba kwenye karibu kila shule. CHAGUA CCM kwa mapambano sahihi dhidi ya adui ujinga.

9. CCM ni chama pekee kinachohakikisha Serikali yake inatoa Huduma bora za kiafya. Leo hii hospitali zetu nchini zinatoa Huduma bora za kiafya ikiwemo kufanya upasuaji wa magonjwa makubwa hapa hapa nchini, kwanini usiichague CCM? Una kila sababu ya kuichagua CCM kwa mapambano dhidi ya adui maradhi.

10. CCM ndio chama pekee ambacho Serikali iliyopo madarakani inajenga uchumi imara wa nchi. Kupitia ujenzi wa viwanda, miundombinu, uboreshwaji wa kilimo na mengineyo umesababisha uchumi wa nchi kukua kwa zaidi ya asilimia 7 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Afrika yenye uchumi unaokuwa kwa kasi. Kwa maendeleo bora ya kiuchumi na mapambano dhahiri dhidi ya adui umaskini, CHAGUA CCM!

Shilatu E. J
 
11 CCM ni chama pekee kilichothubutu kutumia fedha ya walipa kodi kununua madiwani.
 
12.Ccm ndo chama pekee kilichotufikisha hapa tulipo *mnajua tupo wapi#
 
Kama maoni yako ni sawa" kwa nini tuwe na uchaguzi ? Tafakari zaidi.
 
12.Ccm ndo chama pekee kilichotufikisha hapa tulipo *mnajua tupo wapi#
Nimemwelewa sana mleta hoja tuko pamoja hakika cmm ni chama bora kinacho pendwa mno na wananchi hasa sisi wafanyakazi.kwani kinatujali mno
 
Ccm ni chama pekee kinawalazimisha TBC kurusha matangazo yao mubashara bila malipo.
 
CCM ni chama pekee kinachopiga wagombea wengine wa upinzani na hata kudiliki kuwakata mapanga wapinzani.
 
Ccm ni chama pekee kinachofikiri watanzania wote hawana akili .
 
Tuko katik nchi zinazoendelea kwa sabab ya kuichagua sisiemu,mleta mada nafikkir wamekulipa zaid ya buku 7 kam ilivyozoeleka
 
Nimemwelewa sana mleta hoja tuko pamoja hakika cmm ni chama bora kinacho pendwa mno na wananchi hasa sisi wafanyakazi.kwani kinatujali mno
Jana chama hiki makini kimewaongezea mshahara wafanyakazi takribani sh elfu kumi . ccm oyee chagua ccm
 
11 CCM ni chama pekee kilichothubutu kutumia fedha ya walipa kodi kununua madiwani.
Huna ushahidi. Lakini CHADEMA ni Chama pekee kilichompokea mtu waliyemtangaza kwa miaka 8 kuwa fisadi papa lakini wakamteua kugombea bila kushindana na yeyote. Rupia ilitumika
 
Back
Top Bottom