Kwa miaka mitano mfululizo ya kipindi cha kwanza cha mbunge wetu Mnyika, alileta hoja mara nyingi bungeni dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasa Archard Mutalemwa kushindwa kutatua tatizo la maji Mkoa wa Dar es Salaam mbali na kuliongoza shirika hilo kwa zaidi ya miaka 30. Mnyika alipata kusema, mtu akiongoza shirika kwa kipindi kirefu hivyo anakosa mawazo na mbinu mpya za kutatua matatizo ya watu. Baada ya serikali kuwaagiza PCCB kuchunguza alivyopata mali zake, hizi ni sababu nyingine 10 zinazoweza kupelekea akatumbuliwa majipu.
1. Ni mkurugenzi mtendaji wa Dawasa kwa miaka 30 lakini kwa kipindi chote hicho hakuna kitu cha maana kilicho fanyika. Eti kazi ya Dawasa ni kuwasimamia Dawasco wakati watu hawana maji. Si haki fedha za walipa kodi kutumika kuendesha mashirika mawili yanayofanya kazi zinazofanana.
2. Amenunua ekari 200 kijiji cha Mapinga na kuepeleka mgogoro mkubwa wa ardi kati ya wana kijiji.
3. Ana tuhuma za rushwa mara nyingi lakini PCCB waliogopa kumchunguza kutokana na kuwa mshikaji JK. Mnakumbuka sakata la City Water na maneno aliyoyasema bosi Patrick Rubanzibwa?
4. Watoto wake wamegeuza ofisi ya Dawasa kuwa kijiwe chao kwa kujiona kuwa wana haki ya kushinda ndani ya ofisi yake huku wafanyakazi tukiwa tumesubiri nje kwa kipindi kirefu. Mtoto wake wa kike utafikiri pia yeye ni mkurugenzi mkuu kwa kutoa maelekezo kwa wafanyakazi. Ni sheria ipi inawaruhusu watoto kuendesha magari ya shirika?
5. Wafanyakazi wenzetu 20 walilipiwa nauli na Singasinga wa IPTL kwenda Zimbabwe kwenye harusi ya mtoto wake. Yeye na Singasinga wanafanya biashara gani?
6. Mtoto wake wa kiume alisoma shule ya sekondari St Mary’s international lakini akapata zero lakini amepa kazi Dawasco.
7. Muda wake wa kustaafu umepita miaka 4 iliyopita lakini bado anaongezewa mkataba kila mwaka.
8. Anasomesha watoto 12 ulaya kwa mshahara wa milioni tano kwa mwezi anaupokea kutoka serikalini
9. Amenunulia nyumba mbili mke wake Nancy na kumwamishia Malaysia. Mke wake anamiliki biashara lukuki zikiwemo tenda za serikali kwa niaba ya mume wake. Dawasa wanamlipia mke tiketi business class kwenda Malaysia
10. Ana nyumba jijini Dar es salaam zipatazo 30.